Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA | Page 9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by DxR, Jul 27, 2015.

 1. D

  DxR Member

  #1
  Jul 27, 2015
  Joined: Jun 5, 2015
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu.

  Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais?

  Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma.

  Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

  Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.

  Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

  Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala.

  Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
   
 2. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #161
  Jul 30, 2015
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 10,356
  Likes Received: 7,461
  Trophy Points: 280
  hawa CHADEMA walikuwa wanamtukana Lowassa bila kujua ukweli wote. na hawakukosea, watu wangesema wajue ukweli wote ndiyo waanze kusema hakuna kashfa hata moja ingeibuliwa. lowassa katoka na katuambia mwizi wetu ni nani hakuna haja ya kumsakama tena. wanaopinga lowassa kuingia CHADEMA, kwanza hawajui siasa kwa kuruhusu emotional na personal ishu zicloud maamuzi yao. pili ni wale wanaangalia CCM NA upinzani kwa mtazamo wa simba na yanga, ni mashabiki wa siasa.
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #162
  Jul 30, 2015
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
 4. B

  BUKONGO Senior Member

  #163
  Jul 30, 2015
  Joined: Feb 26, 2014
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuko pamoja Tundu Lisu tutashinda tu
   
 5. tol

  tol JF-Expert Member

  #164
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 18, 2014
  Messages: 216
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mbona nyie maccm mnatoka povu jiwe mlilolikataa sasa limekuwa jiwe kuu la msingi
  ni rahisi kumbadilisha mwovu mmoja ailyeingia ktk kundi la watakatifu lakini ni ngumu sana mtakatifu mmoja kubadilisha kundi la waovu mafisadi na Mal aya ila yeye ndo atabadilishwa kwani wao ndio waliomweka hapo
   
 6. m

  msikivu66 JF-Expert Member

  #165
  Jul 30, 2015
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 253
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Kinachotafutwa na Ukawa/Chadema ni kuifanya CCM kuwa chama cha Upinzani, Lowasa ana influence kubwa ya kusababisha CCM kuwa chama cha Upinzani, hivyo basi aijalishi kama aliyekua na tuhuma za ufisadi atatumika kuuondoa mfumo Fisadi wa CCM, nakupa mfano: jambazi aliekubali kushirikiana na Polisi katika kuutokomeza ujambazi urahisisha sana kazi kwa Polisi, napata shida kuamini kama jambazi huyo ataurudia ujambazi tena.
   
 7. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #166
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 5,701
  Trophy Points: 280
  Hatari: unaingiza nyoka shambani mwako ili aweze kumaliza tatizo la panya. Kwa muda, unafanikiwa maana panya wanaisha lakini nyoka lazima aendelee kupata mlo. Anahamia kwa kuku wako. Wanaisha. Baadaye unaanza kumwona ni adui naye analitambua hilo.
  Hatari? Inabidi akugonge wewe ili kujihami!
   
 8. m

  msikivu66 JF-Expert Member

  #167
  Jul 30, 2015
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 253
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Kwa mfano wako iweke hivi: naingiza njoka shambani amalize njoka, kitu ambacho hakiwezekani hivyo mfano wako si sahihi, mbona logic yenyewe ni rahisi sana, AU ndio kujifanya hutaki kuelewa?
   
 9. j

  jobless tycoon JF-Expert Member

  #168
  Jul 30, 2015
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 676
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Kaka acha mbwembwe, mfano unaofit hapa ni kenya, zambia na hata south africa kidogo inakuja, acha kutisha watu ili kutetea kitumbua, wakati wa kuitoa ccm ni ss na kuanzia mwaka huu ndo mwisho wa chama au watu fulani kujipa hati miliki.
   
 10. uyui kwetu

  uyui kwetu JF-Expert Member

  #169
  Jul 30, 2015
  Joined: Oct 23, 2013
  Messages: 902
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  we bibi hulali
   
 11. P

  PATCHO Member

  #170
  Jul 30, 2015
  Joined: Sep 30, 2013
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Noted Mughway...great lawyer
   
 12. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #171
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 5,701
  Trophy Points: 280
  CDM wameeleza wazi. Lengo ni kumtumia EL kufanikisha malengo yao. Kubwa ni kupata idadi kubwa ya wabunge. Lakini naye EL kaingia pale kwa manufaa yake binafsi. Nani atafanikisha lengo lake?
   
 13. Rapha

  Rapha Tanzanite Member

  #172
  Jul 30, 2015
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 633
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  The answer was simple, "cash"
   
 14. e

  electrical Member

  #173
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 29, 2014
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ww unajielewa mkuu
   
 15. festroby

  festroby Member

  #174
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 61
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  ivi inawezekana kutumia nyongo ya mamba kumuua kenge? kama inawezekana basi lowasa ndo nyongo ya mamba na ccm lazima ife ukubali ukatae ukweli ndo huo
   
 16. n

  ngudengude JF-Expert Member

  #175
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 2, 2015
  Messages: 1,181
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  tena madini tema madini mkuuu, well saidi, tuliambiwaga hawa jamaa huwa wanachukua hela nje ya nchi kuleta chaos mpaka ya kulipua vibomu sasa tumeanza kuamini. Kwa tamaa hii hawa chadema hata watu waliokuwa wanadhurika ktk mikutano yao walikuwa nyuma yake
   
 17. mankaga

  mankaga Member

  #176
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 84
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ww soma vizuri histori viongozi wote wa cdm wametoka ccm bata slaa . pili ktba ya chd haisemi mgombea pekea ni slaa. Katiba ndio muongozo.
   
 18. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #177
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,684
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Vyovyote iwapo,CDM haiwezi kuiombea mema CCM..hali kadhalika CCM kwa CDM..hiki tunachojadili hapa kwamba kwanini CDM wamegeukia matapishi yao hata wao walijua tutasema hivyo..yet CDM wamempokea..pengine tunaoshangazwa na uamuzi huu kuna kitu tunamiss..Kitu cha msingi hapa ni je,watanzania tunamhitaji loswasa au la? Na je lowasa ni fisadi?

  Nauliza hivi kwa kuwa,pande zote CDM na CCM wana maswali ya kutujibu watanzania..huyu mtu fisadi kwenye list of shame ameingiaje kwenye list of fame? lakini pia huyu fisadi anayeomba kila siku kupelekwa mahakamani kama ushahidi upo,inakuwaje anafumbiwa macho? Lakini pia huyu fisadi amehudumu kwa kuda mrefu kama mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya usalama wa nchi..na sisi kwa nafasi yetu kama wananchi tulifanya nini tulipoambiwa jamaa ni fisadi?
   
 19. Jumaki50

  Jumaki50 Member

  #178
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  huo ndiyo ukweli kwa mtu aliyo zunguka tanzania hii
   
 20. Mr.Venture

  Mr.Venture JF-Expert Member

  #179
  Jul 30, 2015
  Joined: Jan 2, 2014
  Messages: 1,551
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  NAONGEZEA MAJIBU:
  Tulimwita fisadi kwa 7bu alitajwa na kamati ya bunge kuhusika na ufisadi. Kumbe alitolewa kafara na "mamlaka ya juu". Sisi sio malaika kung'amua hilo kwaiyo ilikuwa ni jukum lake kukataa kutolewa kafara kumtaja mhusika halisi, jambo hili ndio amelifanya sasa na kwahiyo hatuna ugomvi naye tena. Makombora tunayaelekeza kwa "mamlaka ya juu" na vibaraka wake. Pole Ndg.Lowassa utiifu wako kwa boss wako ndio uliokuponza kwa miaka yote. Sote tunajua hata escrow wametolewa kafara waliopata vijicent kupitia mkombozi bank wakti mabwanyenye waliopata "big cake" kupitia stanbic wakilindwa na "mamlaka ya juu". Mwenye akili amefahamu.
   
 21. Omulasil

  Omulasil JF-Expert Member

  #180
  Jul 30, 2015
  Joined: May 5, 2015
  Messages: 612
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 60
  Mbinu chafu za Chadema zitaiangamiza
  Miaka ya 70 Marekani ilikuwa inamtumia sadam kujaribu kudhofisha nchi ya Iran, baadae Sadam alikuja kuwa mwiba kwao
  Inajulikana kuwa mfuga jini baadae litamuua
  Chadema haioni kuwa sisi tulioitegemea inatuondolea imani? Fikria "eti Lowassa yuko kwenye chati kuuia ccm" ili hali yafuatayo yataiua Chadema;;:
  1. Kitendo cha KUKATWA Dr Slaa ni hujuma na UTESAJI WA KISAIKOLOJIA kWAKE NA WAPIGANIA HAKI
  2. Kuingia kwa Lowassa ni kuingiza ngenge la wezi wazee wa visenti mhindi wa pale mfanyabiashara. Je chedema nao ni watafutapesa?
  3. Ni kupoteza muda badala ya kuishambulia ccm na mfumo wake wa kifisadi "sasa ni KUSAFISHA NA KUMTAKASA FISADI possibly No 1 kama sio 2
  3. Ni kukubali kuwa na watu wasio wazalendo wala jasiri kutetea nchi au kuifia kama Lowassa ambaye alikuwa tayari kupoteza wadhifa akificha ukweli kuwa yeye na swahiba waliiba bila kupepesa macho hakumtaja hata kufa
  Najiuliza mbona hana spirit ya Sokoine?
  angepewa urais ccm asingesema na Cdm wangeendelea kuita Fisadi
  4. Kupitisha Lowasa ni kusema kuwa Chedema nia ni Ikulu iwe kwa Wizi au Ukweli , ni kutangaza kuwa wanataka nao wakaziibe safari hii wakiwa na Professional
  Iko wapi Nccr ilikuwa tunasukuma gari ikwa na shehe na mwanasheria. Najaribu kuhisi kuwa there are PLANTED GUYS WITHIN CHADEMA tutegemee kifo chake na huenda JESUIT na Masoni theoty zinztumika na kuniaminisha kuwa hakuna chama cha upinzania
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...