Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA

Lissu na Slaa ni wanasiasa wote wakiwakilisha CHADEMA,

Lissu na Slaa wako karibu katika utendaji wao wa kazi wa kila siku za chama chao.

Labda tungekuwa tumemsikia Slaa kalalamika maneno yako yangekuwa yana mashiko, mtu ambaye labda mwenye uwezo wa kusikia malalamiko ya Slaa ambayo wengine hatuwezi kusikia ni mchumba WAKE, je UMEMPINDUA? UMEKUWA MWANDANI WA SLAA? kama siyo kaa kimya kwanza umeanza lini kuitakia mema CHADEMA!!!
 
Wanaukumbi.
https://www.facebook.com/pages/Tundu-Antiphas-Lissu/510837455738370?fref=nf

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
Asante kwa taarifa mkuu tunakusubiri kwa utekelezaji hujachelewa
 
Mpekuzi blog
Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa hapo chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 
Vita vya Iraq, Marekani na washirika wenzake walikuwa wamepania kumtoa Sadam, na kweli walifanikiwa, lakini hawakuwa na plan ya maana juu ya Iraq baada ya kumuondoa Sadama, nini kimetokea Iraq? Vivyo hivyo Libya, nini kimetokea baada ya kumuua Gadaffi?

Turudi Tanzania, kwa miaka 20 sasa CHADEMA wamekuwa wanatueleza jinsi ufisadi unavyotuangamiza. Na ni miaka 7 saba tangu Dr Slaa ataje majina ya watu aliowaita vinara wa ufisadi. Leo hii wanatuambia kuwa wanataka kuondoa CCM kwa sababu ndiyo imelea ufisadi, lakini hapo hapo wanaanza kusajili watu wale wale waliowaita vinara wa ufisadi kutoka chama kile kile wanachokiita cha mafisadi. Tena wanasijili walioawaita vinara wa ufisadi. Hivi CHADEMA wana mpango gani ni hii nchi baada ya kuiondoa CCM? Post Sadam era or Post Gadaffi style?

Jambo la pili, Watanzania tuendelee kuamini kuwa CHADEMA wanaweza kuwamudu 'vinara wa ufisadi? Nasema hivyo kwa sababu, ndani ya wiki mbili, Lowassa ameweza kubalisha karibu kila kitu cha CHADEMA, amebadili mgombea, amebadili misingi ya waliyokuwa wanajivunia (anti ufisadi) na mbaya zaidi hata ndimi za viongozi wa CHADEMA kazibadilisha, sasa hivi wanamuita mtu shupavu, kiongozi safi! Kama amefanikiwa hayo ndani ya wiki mbili tu, kwanini tusiamini Lowassa atawapigisha deki na kuwapangia zamu ya kuosha vyombo hao CHADEMA?
 
Mbinu waliyoitumia chadema ni mbaya na chafu, kama lengo ni kuing'oa ccm halafu wao washike usukani wa ufisadi sawa. Ukweli utajisimamia. Hata kama viongozi wakajaribu kupamba maneno ukweli utabaki palepale.
 
Lowassa kashaibadilisha Chadema.
1. Kabadilisha ratiba yao ya uchaguzi.
2. Kabadilisha mgombea wao. Dr. Slaa anakatwa kwa sababu ya Lowassa.
3. Kabadilisha bajeti yao ya uchaguzi.
4. Kabadilisha kauli zao kuhusu ufisadi.
5. Kabadilisha ilani yao ya uchaguzi.
Sasa tujiulize, nani anayebadili mwenzie? Chadema itambadili Lowassa au Lowassa anaibadili Chadema?
Lowassa yuko kwenye siasa muda mrefu kuliko umri wa Chadema. Kuamini kuwa Lowassa atabadilika ghafla ni kujidanganya kulikopitiliza.
Mpaka sasa Chadema haijabadili chochote kwa Lowassa, yeye ndio anawabadili.
Chadema badala ya kuleta mabadiliko, yenyewe ndio inabadilishwa... (Stolen somewhere)
 
Watzd na siasa za maji taka, kila mwana ccm anataharuki, ccm hawa amini kilichotokea wanaona kama ni movie, walichezea shilingi karibu na tundu la choo, sasa imetumbukia, wanahaha huku na kule, kawada tunasema majuto mjukuu, na sio masihara neno hili, sasa wasubiri real movie hapo october, ccm imekwisha habari yake, na hiyo inatukumbusha kanu huku kwetu, nao walifanya hivyo hivyo kama walichokifanya ccm, hawakuamini yaliyo tokea, Lowasa will walk the talk, talk ambayo ccm walishindwa kuitekeleza, walikuwa wanaongea tu, lakini walishindwa kuweka wanachoongea kwenye vitendo.
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Mmh haya, but let us wait & see, October 25 is around the corner
 
Ni bahati mbaya mambo yamekuwa hivi yalivyo sasa. Ngano na magugu vinamea pamoja. Muda wa kubadili hali hiyo kabla ya uchaguzi haupo. Walio husika kumwaga mbegu za ngano na magugu kwenye shamba wanajulika.

Acheni ngano na magugu vimee, kukua pamoja. Ila wakati wa kuvuna magugu na ngano vitatengwanishwa. Baada ya uchaguzi magugu yataenda sehemu yake stahiki. Sio uamuzi mwafaka sana kila wakati kuhama chama kama hukurizishwa na maamuzi, subira ni muhimu sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote.
 
My friend the world of politics is a complex world. In politics you don't have permanent friends or enemies. The paramount choice is often a result of a calculated strategy to win the biggest prize. The biggest prize in this case is to get CCM out of power. If Edward Ngoyai Lowassa can deliver that, so be it.

My friend, what is happening here and what we are witnessing is Chadema's ingenuity and tactical maneuvering in the face of an "enemy" who has vowed to remain in power by hooks and crooks. Even by the "hand of God".

To see Chadema as falling prey to the whims of "mafisadi" is to be narrow minded and myopic. It is to miss the bigger picture.

I can see the opposition gaining and increasing their presence is local councils and the national parliament. I can see increased participation and respect of the opposition views in parliament. I can see a more responsive and responsible government. I can see finally the downing of a new era in Tanzanian politics. THAT IS THE BIG PRIZE. THAT IS THE BIGGER PICTURE. A luta continua until final victory.
 
Hii itakuwa kutumia njia haramu kufikia lengo halali!!!!

Hata unapokua ktk swala la upelelezi unaweza ukamchukua dem na ukamseti vzr kuwa we ni wake ili malengo yako yatimie,big up ukawa inamtumia mtoto wa jambazi ili kumnasa jambazi.
 
baba yangu aliniambia kuwa kinywaji chochote chenye cola ni sumu, ila kwa utamuu huu wa pepsi cola acha niagize na pakti ya 5,000 ya korosho kutoka mtwara niendelee taratiiiiiibu. tutaelewana hapo October
 
Lowassa kashaibadilisha Chadema. 1. Kabadilisha ratiba yao ya uchaguzi. 2. Kabadilisha mgombea wao. Dr. Slaa anakatwa kwa sababu ya Lowassa. 3. Kabadilisha bajeti yao ya uchaguzi. 4. Kabadilisha kauli zao kuhusu ufisadi. 5. Kabadilisha ilani yao ya uchaguzi. Sasa tujiulize, nani anayebadili mwenzie? Chadema itambadili Lowassa au Lowassa anaibadili Chadema? Lowassa yuko kwenye siasa muda mrefu kuliko umri wa Chadema. Kuamini kuwa Lowassa atabadilika ghafla ni kujidanganya kulikopitiliza. Mpaka sasa Chadema haijabadili chochote kwa Lowassa, yeye ndio anawabadili. Chadema badala ya kuleta mabadiliko, yenyewe ndio inabadilishwa... (Stolen somewhere)
kama chadema ndio inabadilishwa na wewe ni ccm basi jiunge na chadema vinginevyo utakuwa usemi kweli
 
ukawa hawawezi kushinda uchaguzi kwa sasa bila ccm kupasuka vipande. huo ndo ukweli.kwa sasa itakuwa ngumu sana kuelewa kilicholengwa na cdm.but muda utasema.
 
Back
Top Bottom