Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA | Page 10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by DxR, Jul 27, 2015.

 1. D

  DxR Member

  #1
  Jul 27, 2015
  Joined: Jun 5, 2015
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu.

  Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais?

  Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma.

  Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote.

  Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.

  Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

  Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala.

  Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
   
 2. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #181
  Jul 30, 2015
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,942
  Likes Received: 2,422
  Trophy Points: 280
  They don't call you "Learned Brother" for nothing! Thank you, my learned brother, Lissu!
   
 3. Jumaki50

  Jumaki50 Member

  #182
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  huo ndiyo ukweli kwa mtu aliyo zunguka tanzania hii
   
 4. k

  kayumba JF-Expert Member

  #183
  Jul 30, 2015
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa kukumbusha tu kuhusu Iraq pia; Marekani anashirikiana na Iran kwa sasa kupambana na ISIS. Ni ajabu na kweli labda ndiyo ule usemi maarufu wa "Enemy of your Enemy is a Friend"!

  Nilijiuliza maswali kama yako wakati wa uchaguzi uliopelekea kuondolewa KANU madakarani kwani akina Prof. Saitoti ambao walikuwa watuhumiwa wakuu katika kashifa ya Goldenberg walikaribishwa kwenye NARC but later i came to realise it was for the best though morally I still question the idea.

  Lowassa may not be able to clinch the top sit coming October but his supporters might alter the ratio of ruling party MPs Vs opposition MPs, and to our nation, this will be a positive step. You are not alone in questioning CDM's decisions on this and i did too! If doing so will come with positive changes in our politics for the better nation then we will say the end justifies the mean as usual!

  With that in mind i will give CDM and UKAWA the benefit of doubt for the time being!
   
 5. n

  nkikiki Senior Member

  #184
  Jul 30, 2015
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata muuaji aliyekamatwa kwenye tukio kama alitumwa na mtu mwingine huyo ndiye atakuwa muuaji mkuu!
   
 6. yaramazlik

  yaramazlik Senior Member

  #185
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Huwezi jadili mfumo bila kuwajadili waliouharibu huo mfumo
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #186
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  CCM wanajikanyaga sana ..yaani mwaka huu sijui kama kuna rangi wataacha kuona
   
 8. gwakipanga

  gwakipanga JF-Expert Member

  #187
  Jul 30, 2015
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Kwa technique hii chedema wasahau kishika Dora, wamesahau usemi usemao "mwendo kasi unaua" watakachokipata October hawato amini hii inadhiilisha kwamba tunasafari ndefu sana kuelekea kwenye mageuzi ya kweli.
   
 9. yaramazlik

  yaramazlik Senior Member

  #188
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Naona UKAWA wameamua kuuondoa Ufisadi from List ya Maadui wa Nchi yetu so tumebakia na Maadui walewale wa enzi za kupigania Uhuru(Magonjwa,Umasikini na Ujinga)
   
 10. kson m

  kson m JF-Expert Member

  #189
  Jul 30, 2015
  Joined: Jan 24, 2014
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Ni Lowasa.sasa nyie mnayemwona fisadi miaka yote mmemlinda sasa ndio mpaaze sauti? Mtakoma
   
 11. d

  damn JF-Expert Member

  #190
  Jul 30, 2015
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mafisadi wa CCM utawajua tu....unachowazo ni kuhongwa tu
   
 12. J

  Jonathantindwa Member

  #191
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wao walimtumia Mzito Kabwela kuisambaratisha CDM. Nao wanamtumia El kuisambatisha COM. Ngoma inogile, fainali 25/10/15
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #192
  Jul 30, 2015
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 37,389
  Likes Received: 16,353
  Trophy Points: 280
  Msimamo ni upi? Kuwa mpinzani wa kudumu?
  Hizi ni feelings za kimmu haziapply kwenye politics.

  Tujifunze kwa Taifa kama Marekeni linavyoendesha mambo yake ni maslahi ya kudumu ndio yanaangaliwa.
   
 14. m

  muembeni Member

  #193
  Jul 30, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ccm wacha ianguke kwanza for any cost halafu tutakamatana wenyewe kwa wenyewe
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #194
  Jul 30, 2015
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,141
  Likes Received: 22,410
  Trophy Points: 280
  Naona wewe umeandika upo usingizini.
   
 16. Rapha

  Rapha Tanzanite Member

  #195
  Jul 31, 2015
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 633
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Hivi kuna democracy kweli? How comes mtu anachukua form mnatangaza kwamba ndiye mgombea!? Tena sio kwa chama kimoja, bali kwa vyama vyote?
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #196
  Jul 31, 2015
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,462
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145

  Bora useme wewe mkuu...
   
 18. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #197
  Jan 10, 2018
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,660
  Likes Received: 14,687
  Trophy Points: 280
  Napita tu
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #198
  Jan 10, 2018
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,660
  Likes Received: 14,687
  Trophy Points: 280
  Mkuu umekuwa kimya sana
   
 20. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #199
  Jan 10, 2018
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 18,790
  Likes Received: 21,184
  Trophy Points: 280
  Nani tena huyu kafukua huku hahahahahah
   
 21. Tajirimsomi

  Tajirimsomi JF-Expert Member

  #200
  Jan 10, 2018
  Joined: Jan 12, 2017
  Messages: 4,646
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Kumbe nawe unafatiliaga aya mambo
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...