Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Mhe.Tundulisu amethibitisha Chadema kuanza kupokea Ruzuku kuanzia mwezi huu Machi 2023.

Na.
Abdul Nondo.

Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, ndug.Tundu Lissu jana Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.

Akisema “Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020".

“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu.

Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa 2020 waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi na najisi.

( ushahidi soma link : March 5, 2023 – Demo Krasia

Nina mambo machache tuu juu ya hili.

Kwanza huu ni ushahidi mwingine wa wazi na tukubaliane ya kwamba ACT wazalendo ni chama kiongozi nchini ,chenye uwezo wa kuona mbele maili 100 kabla ya wengine kuona. Hii ina maana ya kwamba ACT wazalendo ni chama chenye viongozi wenye maoni,fikra yakinifu na tunduizi katika kufanya maamuzi ambayo wengine watakuja kuyafuata baadaye,hii ndiyo maana ya chama kiongozi.

Walisema hivi hapo nyuma "Uchaguzi ulikuwa najisi, hao ACT wazalendo sio wapinzani wao kuchukua ruzuku na kuingia GNU na kupeleka wabunge ni dhahiri wana halalisha najisi,sisi Chadema kamwe hatutachukua Ruzuku inayotokana na uchafuzi na najisi ya uchaguzi wa 2020".

Ninachopishana na hawa ndugu zetu ni kitu kimoja tuu ni uharaka wao wa kushambulia vyama vingine na viongozi wa vyama vingine wakidhani wao ni malaika kutoka mbinguni huku wakiwa hawana njia mbadala wala suluhu yeyote na hatimaye hujikuta wakiangukia katika njia ile ile ya waliowatukana na kuwapinga kufuata njia hiyo .Vyama hivi vya siasa ni vyama tofauti,vyenye uongozi tofauti, itikadi tofauti,mipango tofauti ,vikao vya maamuzi tofauti ila hawakuwahi heshimu maamuzi ya chama chetu yaliyotokana na vikao vya ndani na maamuzi ya wanachama wetu mbali ya sisi kuheshimu maamuzi yao na vikao vyao .Wajifunze sasa hili ni funzo kubwa kwao.

Tulipoamua kama chama kuingia serikali ya umoja wa kitaifa (GNU) ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu ,tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Leo hii wanataka peleka wabunge wa viti Maalumu Bungeni hatimaye wamepita njia yetu.

Tulipoamua kuruhusu wabunge,wawakilishi na Madiwani kwenda kuapa kuendelea na majukumu yao na kuchukua Ruzuku ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu ,tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Leo na wao wameamua kupokea Ruzuku , hatimaye wamepita njia yetu.

Tulipoamua kutafuta maridhiano na kushiriki Mikutano miwili kule Dodoma, wa tarehe 16 na tar.17 Desemba 2021 na ule wa tar .05 April 2022 Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano ambao Mh. Rais @samia_suluhu_hassan alikuwa mgeni Rasmi.

Ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) @tcdemokrasia_hq chini ya Mwenyekiti wake Mh. @zittokabwe kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu wa chama Mh. @zittokabwe na chama chetu kwa kushiriki wakisema hatuna bargain cheap ya kufanya mazungumzo na Rais ,ambaye ni Mwenyekiti wa CCM matusi yalikuwa yote dhidi yetu tukiitwa CCM-B. Tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu. Leo hii wao kutwa kucha Ikulu na hadi kumualika Mh.Rais na Mwenyekiti wa CCM katika mkutano wa BAWACHA .

Tulipoamua kuingia kwenye kikosi kazi kilichoundwa wao walikataa wakisema kikosi kazi kilichoundwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM hakina maana na hakitaleta Matokeo yeyote ,kamwe hawakuheshimu maamuzi yetu kama chama walitutukana na kumshambulia kiongozi wetu Mh. @zittokabwe na Chama chetu .Tulikaa kimya tukijua watapita njia yetu tuu.Hatimaye kikosi kazi cha Zanzibar kilichoundwa tar. 10 Oktoba 2022 na wao Chadema walishiriki na wakatoa mjumbe kuwa katika kikosi kazi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wao wa Zanzibar ndug. Said Issa Muhammed. Hatimaye wamepita njia yetu.

Kikosi kazi huku bara kikakusanya maoni na kigawa maazimio ya utekelezaji katika makundi matatu mambo yanayohitaji utekelezaji wa muda mfupi,muda wakati na mrefu.Mikutano ya hadhara ni jambo lililohitaji utekelezaji wa muda mfupi ,bado ndugu zetu hawa wakaibuka wakatukana na kutushambulia tulikaa kimya sababu tulijua matunda ya maridhiano na kikosi hata wao watapongeza na kufurahia na kunufaika ,tulijipa muda sababu tunaona mapema kuliko wao.

Hatimaye tar 3/Jan/2023 Rais Samia akatengua zuio la mikutano ya hadhara akirudia mara zote kusema "Jambo hili ni katika maazimio ya kikosi ya muda mfupi na nina kipongeza kikosi kazi". Ndugu zetu katika hili wakajitokeza kusifu ikiwa walipinga kikosi kazi na mchakato wake wote.Tulijua matunda haya ni wote kwa maslahi ya wote hata kwa waliotukana na kukashifu .

Leo hii wamefuata nyayo za ACT WAZALENDO katika kila tulichoamua kukifanya licha ya wao kututukana leo hii wamegeuka kukifanya wao leo wanahubiri maridhiano ambapo walitutukana tulipo hubiri,wamepokea ruzuku ambapo walitutukana tulipopokea ,wamekuta na Rais ambapo walitutukana tulipokutana nae, wanataka wapeleke wabunge Bungeni viti maalumu ambapo walitutukana tuliporuhusu wabunge wetu kwenda Bungeni na wawakilishi, sasa wanawatambua madiwani wao wote nchini waliotokana na uchaguzi na uchaguzi wa 2020 ,ambapo walitutukana tuliporuhusu madiwani wetu .

Maswali kwao.

Je,unajisi wa uchaguzi wa 2020 umeisha lini? hadi kupokea Ruzuku waliyokataa wakisema inatokana na najisi ya uchaguzi wa 2020 wakitukana ACT wazalendo kwa kupokea Ruzuku. Na waaminiwe kwa lipi lingine watakalogomea?

Je, wanaonaje matusi yote waliyotukana ACT wazalendo sasa wajigeuzie wao? .kama kweli wanapenda haki na usawa.

Maswali hayo yakikosa majibu iwe ni somo kwao kujifunza na kuheshimu maamuzi ya vyama vingine na wakubali ACT -wazalendo ni chama kiongozi.

Ahsante.

Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT-wazalendo Taifa.
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huu uliopita.

Makamu huyo nguli wa sheria na siasa bora Tanzania ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watanzania waliokiunga mkono chama hicho kikiwa katika hali ngumu ya kifedha.

"Wanachama wetu na wafuasi waliendelea kufanya kazi za chama bure kabisa bila malipo, na hii inaonesha kuwa Chama chetu ni chama cha watu."

===


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku waliogoma kuichukua baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu leo Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.

“Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020

“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu

Hata hivyo mwanasiasa huyo alisema hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika au Mwenyekiti, Freeman Mbowe atatoa taarifa rasmi.

Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi.

Kwenye kauli za chama hicho walisikika wakisema kuwa wanaukataa uchaguzi na mazao yake.

Ikumbukwe chama hicho pia kilikataa kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni kwa sababu ya kutoutambua uchaguzi huo.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na Serikali.
Hiyo kauli kama imetoka Kwa Tundu ujue wana tofauti zao huko za hela na mwenyekiti wao, sasa anataka wananchi wajue, ye hajuagi kama chama ni cha familia
 
Ni bora wachukue hizo ruzuku iwasaidie kujenga chama chao kuliko wasaidiwe na wazungu ambao hela zao zimejaa masharti kibao. Na kama wanamtambua Rais Samia kama Rais wa Tanzania hapo kuna nini tena?
 
CCM na CDM vipo katika maridhiano wa yale madhila yaliyotokea wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tano. Kila mtu anatambua kuwa mengi yalitokea huku wahanga wakubwa wakiwa ni viongozi, wanachama na hata wapenzi wa CDM.

Katika maridhiano ni lazima itokee "win - loose situation" kitu ambacho inavipasa vyama hivi vyote viwili vikubaliane nayo. Ndiyo maana unaona baadhi ya hatua zikichukuliwa, mitizamo hasi ikibadilika, misimamo ikilegezwa, na hata maamuzi magumu yakifanyika.

Hali ya "win - loose" ni njia sahihi na salama ya kujipima na kuangalia pale ulipo jikwaa na wale siyo pale ulipoangukia. ACT Wazalendo waangalia msimamo huu mpya wa CDM kwa dhana ya pale walipoangukia, wakati CCM na CDM wanaangalia maridhiano yanayoendelea kwa dhana ya kuepuka kufikia pale walipojikwaa hapo awali hali iliyopelekea kuwa ni chanzo anguko lililotokea.

Huwezi kuhitimisha eti kwa kusema kinachofanyika hivi sasa kuwa ni ndoa imefungwa, wakati hutambui hata ajenda zilizopo katika mchakato wa maridhiano. Hata kama suala la kuondoa marufuku ya shughuli za hadhara za vyama vya kisiasa lilikuwa ni sehemu ya maazimio ya kikosi kazi, hii haindoi uwepo wa ajenda hii katika maridhiano kati ya CDM na CCM kiasi kwa ACT Wazalendo eti idai kuwa ina hati miliki katika suala la kuondolewa kwa marufuku hiyo haramu.

Ni lazima kuna mfanano wa ajenda za kikosi kazi na zile za maridhiano. Mathalani, madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, hata kama nayo yalikuwa ni sehemu ya ajenda ya kikosi kazi, haindoi uhalali wa CDM kuyaweka kama sehemu muhimu ya ajenda za maridhiano na CCM, kwa kuwa wao hawakuwa sehemu ya kikosi kazi.

Ni hoja muflisi kuanza kuona matokeo ya maridhiano kuwa CDM imepoteza muelekeo. Ni dhahiri CDM kuna vitu itabidi ivipoteze kwa kulegeza msimamo, lakini kuna vitu itavipata kwa kuwa hiki ndicho kiiini cha maridhiano. Ukitaka kujenga hoja nje ya kanuni hii ya kufanikisha maridhiano ni kutaka kujigeuza kuwa kituko cha mwaka mbele ya watu makini, wajuvi na waelewa wa mambo ya kisiasa.
 
Kwa Sasa CDM wamekuwa chawa wa CCM mpaka sisi chawa wa miaka yote wanataka kutuzidi na kuchukua nafasi zetu
 
Kinachowasumbua Ni wivu tuu! Cdm kukaa na watawala, mlipenda Sana cdm kijitenge na serikal(CCM) kitu ambacho manguli wa siasa Akina kinana wamekiona Ni vigumu kurusu siasa Tz halafu cdm ukawatenga. Lkn kwa sababu wengi wenu humu jf Ni wachanga kisiasa hamuwezi kujua akili ya CCM.
 
Kathibitisha badala kadhibitisha, sasa umefurahi! Pesa zile serikali ilikuwa inataka wazichukue ili watimize lengo lao batili ila Chadema walizikataa, kama sasa wamezichukua hii inatokana na maridhiano na maridhiano si dhambi kwa waungwana na si utashi wa upande mmoja, baada ya maridhiano yaliyopita yamepita huwa hayarejewi.
Sawa
 
So uchaguzi wa 2020 ni halali ama sio halali? Ruzuku inatokana na kina Mdee? So ni wabunge halali?
Mkuu unahitaji kupata elimu ya namna ruzuku inavyopatikana. Japo inawezekana ukweli unaufahamu ila maandishi yako yanalenga kusukuma hoja fulani dhaifu
 
Hapa Chadema wamekosea. Hii taarifa alitakiwa aitoe Mnyika mara tu alipopokea hundi. Kwa kuchelewa inaonekana kama walikuwa wanaficha jambo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom