Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Kinachowasumbua Ni wivu tuu! Cdm kukaa na watawala, mlipenda Sana cdm kijitenge na serikal(CCM) kitu ambacho manguli wa siasa Akina kinana wamekiona Ni vigumu kurusu siasa Tz halafu cdm ukawatenga. Lkn kwa sababu wengi wenu humu jf Ni wachanga kisiasa hamuwezi kujua akili ya CCM.
Mkuu, mambo muhimu kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi, na mustakabali mwema wa taifa, watu wanayachukulia kama mambo ya mzaha. Mchakato unaoendelea wa maridhiano haya una baraka zote za vyombo vya ulinzi na usalama.

Vyombo vya dola vinatambua kuwa CCM na CDM vinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na makundi yote muhimu ya Watanzania. Ukiruhusu chuki miongoni mwa vyama hivi vikuu viwili ni kutaka kulipasua taifa.

Licha ya rafu za kisiasa katika chaguzi za 2015, 2019 na 2020, lakini nguvu za CDM kutwaa dola bado ni tishio kubwa kwa CCM, achilia mbali vyama ambavyo vipo kwenye balehe kama ACT Wazalendo. Ushauri mbaya ulitolewa na wahafidhina ndani ya CCM ili kukidhoofisha na hata ikiwezekana kukiua CDM, lakini haikuwezekana.

Makada wa CCM waliojificha ndani ya mamlaka tofauti za kiserikali, kimahakama na kibunge, walijaribu kila wawezalo, lakini ikashindikana. Kuna msemo mmoja unasema aliyekushinda nguvu, yakupasa kuungana naye.

Naiona kesho ya taifa letu kupitia mchakato unaoendelea wa maridhiano, CCM na CDM vikienda kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Uchaguzi ujao ukiendeshwa kwa uhuru na haki, na huku mamlaka husika zikifanya yalw yapaswayo kutendwa kwa haki, nauona ushindani kama ule uliokuwepo nchini Kenya kati ya Ruto na Odinga.
 
Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Kumbuka hapa unaridhiana na mtu mwenye msumeno kwenye mpini wewe umeshika makali. Lazima busara itumike
Mkuu, hayo ya Katba/Tume Huru siyo ya CHADEMA, hayo ni yetu, waTanzania wote.
Hapa haitengenezwi katiba ya CHADEMA au CCM, ni katiba ya nchi; na ukiangalia ni wazi kabisa kwamba hata hiyo Katiba CHADEMA hawana tena msukumo nayo. Umesikia ikitajwa hata kwenye mkutano mmoja tu?
Hivi juzi, hukuona Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi akiteuliwa na Mwenyekiti wa CCM.

Hii Katiba na Tume Huru nani anayeipa msukumo kwa sasa na kwa manufaa ya nani? Bado unaamini Katiba itapatikana kabla ya 2024, au hata 2025? Hiyo itakuwa ni Katiba, ya nchi, au makubaliano tu kati ya CHADEMA na CCM jinsi ya kuwanyonga waTanzania vizuri huku wao wakifaidi matunda ya jasho la wananchi?

Nimalizie kwa kusema hivi. Tanzania sasa hakuna vyama vya upinzani.
 
Katiba ni ya Taifa lakini wenye nguvu ni ccm. Hilo ulijue
 
Mkuu, mambo muhimu kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi, na mustakabali mwema wa taifa, watu wanayachukulia kama mambo ya mzaha. Mchakato unaoendelea wa maridhiano haya una baraka zote za vyombo vya ulinzi na usalama.

Vyombo vya dola vinatambua kuwa CCM na CDM vinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na makundi yote muhimu ya Watanzania. Ukiruhusu chuki miongoni mwa vyama hivi vikuu viwili ni kutaka kulipasua taifa.
Comment bora kabisa kwenye uzi huu
 
Licha ya rafu za kisiasa katika chaguzi za 2015, 2019 na 2020, lakini nguvu za CDM kutwaa dola bado ni tishio kubwa kwa CCM, achilia mbali vyama ambavyo vipo kwenye balehe kama ACT Wazalendo. Ushauri mbaya ulitolewa na wahafidhina ndani ya CCM ili kukidhoofisha na hata ikiwezekana kukiua CDM, lakini haikuwezekana.
Kama cdm haijafa 2015 na 2020 basi tena haitakufa kamwe.
 
Katiba ni ya Taifa lakini wenye nguvu ni ccm. Hilo ulijue
Heshima mkuu 'Rasterman'.
"Wenye nguvu" ni wananchi, na hilo ndilo lililoanza kuwatia kiwewe CCM wakati CHADEMA ikielekea kukubaliwa na wananchi.
Huoni jinsi CCM walivyoanza kuhangaika kabla ya kubuni maridhiano?
 
😅😅😅sawa. Wanajidai wenyewe wana Dola
 
😅😅😅sawa. Wanajidai wenyewe wana Dola
Hii ya dola iliondoka na Magufuli. Hakuna tena ndani ya CCM mwenye uwezo wa kuitumia dola kipuuzi kama alivyofanya Magufuli.
Samia anatafuta asifiwe na ulimwengu kama siyo Tanzania, hawezi kutumia dola kwa njia alizotumia mtangulizi wake.
 
Kama Magufuli aliweza wengine watashindwa vipi?
 
So uchaguzi wa 2020 ni halali ama sio halali? Ruzuku inatokana na kina Mdee? So ni wabunge halali?
Kwani ruzuku itatokana vipi na akina Mdee? Kwani ndiyo walikuwa wagombea Urais?

Akina Mdee ni zao la kura za wagombea ubunge wote wa mwaka 2020.
 
So uchaguzi wa 2020 ni halali ama sio halali? Ruzuku inatokana na kina Mdee? So ni wabunge halali?
Sio hivyo..

Amelifafanua vyema sana hili. Hata Mimi nilikuwa sijui kabisa..

Kumbe mgawo wa ruzuku msingi wake huwa ni;

1. Idadi ya kura walizopata wabunge wa majimbo. Na chama Cha siasa kina qualify kupata ruzuku iwapo kura za wabunge wa majimbo ni si chini ya 5% ya idadi ya kura zote. Hapa CHADEMA kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya CCM, walikuwa na 16.7% ya kura zote..

2. Idadi ya kura ya kura za U - Rais. Hapa haijulikani Kwa sababu mpaka sasa NEC ya CCM haijstangaza rasmi kura halisi za ushindi wa u - Rais wa John P. Magufuli jimbo Kwa jimbo..
 
Back
Top Bottom