ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge unazidi kukaribia. Wapinzani wanaoonekana maeneo mengi ya kampeni ni Tundu Lissu na Prof. Ibrahim Lipumba.
Kumekuwa na mijadala katika maeneo mbalimbali nchini juu ya hatma ya wagombea hawa baada ya uchaguzi kuisha.
Kwa upande wa Lipumba, kwa vile amekuwa mgombea kwenye chaguzi za siku za nyuma, watu wengi wanategemea atarudi kukiongoza chama chake cha CUF kama alivyofanya baada ya chaguzi zilizopita.
Kwa vile Tundu Lissu anagombea kwa mara ya kwanza, watu wamekuwa na maoni mbalimbali juu ya kile wanachotarajia akifanye baada ya uchaguzi. Miongoni mwa yaliyojirudiarudia ni kama ifuatavyo;
1. Tundu Lissu atataka kuchukua nafasi ya Uenyekiti ndani ya Chadema. Hatua hii itaongeza msuguano uliopo kati yake na Mbowe. Kwa vile hakuna uchaguzi wa ndani wa Chadema hivi karibuni, uwezekano wa Tundu Lissu kufuata njia hii ni mdogo.
2. Tundu Lissu atarudi Ubelgiji kuungana na familia yake. Kwa vile Tundu Lissu ameomba kutambuliwa kama mkimbizi nchini Ubelgiji, upo uwezekano mkubwa kuwa atarudi kule mpaka maombi yake hayo kukamilika ili familia yake iendelee kutunzwa na serikali ya Ubelgiji.
3. Tundu Lissu ataungana na Zitto Kabwe kwenye ACT. Kutokana na msuguano unaoendelea kati yake na Mbowe, iwapo ataamua kubaki nchini, anaweza kujiunga na Zitto kwenye ACT.
4. Tundu Lissu ataanzisha chama chake. Baadhi ya watu wanadhani Tundu Lissu ataibuka na kusajili chama chake kipya. Uwezekano wa kuanzisha chama baada tu ya uchaguzi ni mdogo. Historia inaonyesha vyama vingi huanzishwa unapikaribia Uchaguzi Mkuu au baada ya mivutano kwenye chaguzi za ndani za vyama.
5. Tundu Lissu ataomba nafasi kwenye serikali ya Magufuli. Wapo pia wanaoamini kuwa Tundu Lissu atamkumbusha Magufuli juu ya ahadi ya kumpa kazi. Kwa vile Magufuli alitoa ahadi hiyo hadharani, itakuwa ni uungwana kuitekeleza. Hii pia itasaidia kumuwezesha Tundu Lissu kujikimu na kuirudisha familia yake nchini.
Kama mnavyoona, matarajio ni mengi, lakini cha muhimu zaidi tuendelee kumuomba Mungu atijalie uchaguzi wa amani na utulivu ili tuendelee kuijenga nchi yetu.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.