Tundu Lissu avurugwa.

Tundu Lissu avurugwa.

Hapa unacheza na maneno, na hujaja na jibu.

Tunachotaka ni majibu, jee, walikufa kweli wakiwa mikononi mwa Serikali ya Nyerere na au Karume? Jee, walifungwa kwanini kama jibu la kwanza ni ndio. Jee, kama walizikwa kisheria ya dini zao, walizikwa wapi, kwani Tundu Lissu kasema bungeni na hakuna mpaka sasa kauli iliyotoka kujibu shutuma za hawa watu.

Tundu Lissu hakusimama pale bungeni na hoja yake binafsi, Tundu Lisssu alikuwa anaongea hoja za wapinzani. Serikali kukaa kimya kwa hili inatutia mashaka sisi wananchi.

Na hapa naona wewe unakuja kucheza na maneno, inaonesha ni vipi ulivyo na kejeli katika kuonegelea masuala ya binaadam ambao wengi tumesikia juzi bungeni maafa yaliowakuta wakiwa mikononi mwa Serikali. Wala hatukusikia pale bungeni mbunge yeyote akisema Lissu athibitishe aliyoyasema la sivyo afute kauli zake kuwa ni uongo, hatujaona hayo.

Nakushauri amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfano.

Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, na hapa unaongea kama mtu aliyelewa madaraka.
kwa hii kauli kutoka kwa gamba FaizaFoxy kwenda kwa gamba mwanadiwani naanza kupata mwanga wa gamba mwanadiwani ni nani!!!
 
Hayo ni matusi na kejeli.

Sijawahi kuongea ambacho sikiamini. Sipo kumremba au kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa. Siku zote naandika humu nnachoamini kuwa hiyo ndio haki na ukweli kwa muono wangu.


Ni miaka kadhaa sasa nimekuwa nikihubiri kuhusu dhulma za Nyerere kwa nchi hii kwa ujumla na si kwa Zanzibar pekee. Nashukuru hivi sasa hata upinzani unayaona hayo, imeanzia kwa dhulma za muungano na nna uhakika itafika mpaka kwa dhulma za hapa hapa ndani ya Tanganyika, dhulma za Nyerere hazikuanzia wala kuishia kwenye muungano.

Kuna watu wengi sana walikufa wakati Nyerere anawahamisha kwa nguvu kutoka makazi yao ya asili kuwapeleka maporini kuanzisha vijiji vya ujamaa, wako waliokufa kwa magonjwa, kwa njaa, kwa kuliwa na wanyama wakali, kwa kugongwa na nyoka. Na wapo waliouliwa na mgambo na polisi waliokuwa wanawaswaga kuwapeleka kwenye hayo maeneo mapya.

Wapo waliokataa, wengine wakauliwa kwa makusudi kabisa na wengine wakapotea wasijulikane walikoishia hadi hii leo.

Hayo yote kuna siku yataibuka.
Toa data na majina.
Siyo sweeping statements za kuambiwa.
 
Hapa umesema kitu chenye akili sana.
wewe bibi siku familia yako itakapozikwa hai na wale wazee wa mabwepande ndio utaacha kutetea uovu eti ilimradi tu unalipwa buku sabau pale lumumba!!!!shame on you.
 
Wakati wa ujio wa Baraka
Obama Tanzania, Obama aliongea na Invisible kuhusu
mimi na Invisible akashindwa kumvunja Rais wa
Dunia, ikabidi nifunguliwe kutoka kifungo cha maisha cha JF.

naona bibie Faizer anamkubali Obama na kumuita Raisi wa dunia, so si vibaya America ikiendelea kuzikalia flame za kiarabu?
 
Last edited by a moderator:
HALI ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, juzi ilikuwa tete baada ya wabunge kuamua kumtolea uvivu kutokana na kauli zake za uwongo zilizodaiwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.

Huku wakionyesha mifano, wabunge wengi waliosimama walimshambulia Lissu kwa kupotosha umma kuhusu masuala mbalimbali ya Muungano huku mengi yakidaiwa kuwa hayana tija wala ushahidi wa kutosha.

Hali hiyo ilijitokeza juzi wakati wa kujadili Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), awali, Lissu, aliwasilisha taarifa ya Kambi ya Upinzani.

Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ndiye aliyekuwa mwiba kwa Lissu, ambapo alisema mbunge huyo amezoea kusema mambo ambayo hayafahamu wala kuwa na uhakika nayo.

Mwigulu, ambaye alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizohusu wizara yake, alisema fedha za misaada kwa kawaida wafadhili hutoa maelekezo ambapo katika hilo, kiasi cha usawa wa asilimia 4.5 hutengwa kabla ya kufanya mgawo husika.
“Naomba tu kwanza niweke kumbukumbu sawa. Fedha wanazopaswa kupata Zanzibar, zimekuwa zikitolewa kwa miaka yote mfululizo kama kawaida.

“Unajua kama mambo huyajui, ni vyema ukauliza. Hata ndugu zangu wa Zanzibar, ni kwa nini msiwaulize viongozi wenu. Bahati nzuri kuna kitengo kinachohusu masuala ya fedha, kuliko kufanya mambo yasiyo na ushahidi.

“Kwa kwaida, fedha za wafadhili ambazo zitatolewa ndivyo mgawo utakavyofanywa. Sasa kama hii iliyoelezwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani kwamba zilitakiwa kiasi cha sh. Bilioni 32. Tulizozipata, tumetafuta uwiano wa 4.5, kiasi kilichobaki tutapeleka Zanzibar,” alisema Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM).

Alishauri kuwepo kwa utaratibu wa kutoa takwimu zinazohusu fedha ili kuwezesha akina Lissu kuelewa kabla ya kuzungumza ndani ya bunge.
Pia, aliwahadharisha wabunge wa Zanzibar kuwa, mambo yaliyozungumzwa na Lissu katika hotuba yake, hayaonyeshi kuwa ana mapenzi ya dhati kwa wananchi wa visiwa hivyo.

“Unajua mtu huyo baada ya kuona chuki aliyoipandikiza Tanzania Bara imekosa mashiko, ameamua kuhamia Zanzibar. Mkivurugana yeye atabaki Singida.

Akinukuu maneno ya Lissu aliyoyatoa mwaka jana kuwa kero za Muungano si mali binafsi ya wabunge, alisema hata watanzania wanakerwa na ubaguzi unaofanywa na Wazanzibari, jambo ambalo ni kinyume cha anayoyasema sasa.
Katika kuonyesha Lissu ni kigeugeu, Mwigulu alisema aliwahi kusema kwamba, Wazanzibari walikuwa wakipendelewa kinyume na jinsi hotuba yake inavyoeleza kwa sasa.

“Yaani wakati mwingine napata shida kuamini kama Lissu ametokea Singida kule ninakotoka mie,” alisema.
Awali, wakichangia hoja hiyo, Mohamed Amour Chombo, alimshangaa Lissu kuwa na mapenzi na watu wa Zanzibar huku awali alikuwa akiwapinga na kuwatolea maneno ya karaha na yenye kukera.

Chiombo, alisema muungano wa sasa baina ya CHADEMA na CUF ni sawa na kuchepuka na kwamba, CUF wanapaswa kuwa macho na Lissu.
“Ndugu zangu acheni mchepuko, rudini njia kuu, hawa wanawapenda leo wana nia yao si bure wenzenu ni sisi,’’ alisema Chombo.

Chombo alisema hotuba ya Lissu ni ya uchochezi na kuwataka watanzani kutokubali kuingizwa katika uchochezi.
“Wewe unaposema muungano hauna maana ujue fedha za uwanja wa ndege zimetokana na nini, acheni michepuko rudini njia kuu.

“Kuna baadhi ya watu wakishapata wimbo Fulani, basi kila wakati atauimba huo huo wakati akienda kula, akienda wapi, sasa ni sawa na Lissu amepata wimbo wa muungano ni huo huo,’’ alisema.
Aidha, kwa upande wake Steven Masele, aliweka rekodi sawa aliposema Wizara ya Mambo ya Nje imewahi kuwa na Waziri kutoka upande wa Zanzibar.

Masele, alisema hayo baada ya kuzuka hoja kwamba Muungano uliopo una upendeleo kwa viongozi wanaotoka Tanzania Bara.
“Jamani niwakumbushe tu kwamba Ahmed Hassan Diria (Marehemu), aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alifafanua Masele.

Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge waliochangia ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri Samia Suluhu Hassan, aliahidi kushughulikia changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi wenye tija.
Hoja ni Lisu au ni maoni ya kambi rasimi ya upinzani bungeni?
Wanathibitisha tatizo alilosema Mch.Mtikira la EPIDOMEA.
 
Juma Abdallah Hanga, na Tundu Lissu alimuongelea Kassim Hanga. Wapi na wapi?

Mtoto wa Hanga ni huyu akiitwa YELENA na nilimsikia kwa masikio yangu Moscow mwaka 2008 akisema Baba yake aliuwawa na Kanali Seif Bakari

%D0%A5%D0%B0%D0%BD%D0%B3%D0%B0_%D0%95%D0%BB%D0%B5%D0%BD%D0%B0.jpg
 
Zamani wapinga muungano kama alivyo Tundu Lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais mvumilivu sana kwa sasa

ulivyo mbulura unadhani huu muungano unawahusu interahamwe tu! Umekuwa mtumwa wa fikra kwa sababu ya tumbo
 
Natamani sana nimuone huyo mtoto anaenda mahakamani, ndipo mbivu na mbichi za Zanzibar na Tanganyika zitapojitokeza.

MwanaDiwani anashindwa kuelewa kuwa maandamano ya Tunisia yalianza kwa mtu mmoja kuilalamikia Serikali kuwa haitoi majibu kwa dhulma zilizofanyika zamani na akaamuwa kujichoma moto hadharani, hilo ndilo lililopelekea utawala kuangushwa., huo kuangushwa na effect yake ikawafikia Wamisri, Walibya na kwingineko.

Hakuna kitu kibaya kama Serikali kutoa kauli za kuwafanya watu wote ni wajinga.

Nikimsoma huyu MwanaDiwani kwa masuala nyeti kama haya na niliposikiliza William Lukuvi aliyoyaongea Kanisani nnawaweka katika kundi la unafik wa hali ya juu sana. Na watu kama hawa hawakitakii mema chama changu cha cha CCM na wala hawamtakii mema Rais Jakaya Kikwete.

Umenena vyema sana Mama FaizaFoxy
Ila umemalizia vibaya.
Amini nakuambia,yeyote yule aitakae Mabaya CCM ni rafiki wa Tanganyika na Wa Zanzibar wote kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:
Faizafoxy unajisumbua kutaka uelezwe au upate majibu ya hoja za T.Lissu kuhusu A.K.Hanga majibu hutopata.Kisu cha moto kimegusa jeraha.

Swali kwako Faizafoxy. Je! CCM inang'ang'ana na mfumo wa serikali 2 kama mkakati mahususi kuizuia Zanzibar kuwa dola ya kiislam? rejea kauli za mh.Lukuvi

Kutokana na kauli za William Lukuvi alizozitoa kanisani, hilo ni wazi kabisa wala sio siri tena.
 
vita vya wenyewe kwa wenyewe hiivyoooooo vinakuja...... na bora vije tuu tuzipacheee vilivyo mwishowe tuheshimiane!
 
Back
Top Bottom