Tundu Lissu avurugwa.

Tundu Lissu avurugwa.

Bado najiuliza kama anayeandika hapa ni FaizaFoxy ninayemsomaga humu, au aliacha computer bila ku-log out sasa kuna mtu anaitumia!
Kweli huu muungano batili umewagawa CCM kwa wengine wakitetea maslahi ya nchi kama FaizaFoxy na wengine wakitetea matumbo yao kama MwanaDiwani ambaye cheo alichonacho CCM hapo kabla hakikuwepo, hivyo akitumia akili kuhusu huu muungano kwa kudai Tanganyika yetu, huenda cheo chake kikafutiliwa mbali kwenye uso wa sisiem.
So inamlazimu aendelee kutumia tumbo kufikiri kwenye masuala nyeti kama haya.
Unamsoma FaizaFoxy lakini humuelewi na sidhani kama utakuja kumuelewa!! Huyu dada/bibi alishawahi kulimwa #LifeBan na #Mods ...miaka ile (nadhani badae alisamehewa na ndo ndio unamuona tena hapa jamvini).

Linapokuja suala la Zanzibar na Muungano huyu FaizaFoxy ni moto mwingine kabisa, hatawaliwi na fikra za Kiinterahamwe! Mara nyingi anasimamia anachokiamini kuwa huenda ni sahihi,mpaka kitolewe ufafanuzi wa kina. Anajua mifumo ya kiutawala inavyoikandamiza wazenj. Ndio maana hapa unaona kuna mpambano mkani na huyo MwanaDiwani ambapo kwa fikra za FaizaFoxy anadhani huyo diwani AMELEWA MADARAKA na amepofuka na ndo mana anacheza na maneno billa majibu murua.

Tuendelee kuufuatilia huu mjadala, labda tutapata majibu ya hayo maandaki.
 
Last edited by a moderator:
Hoja ya Kassimu Hanga ilishajibiwa jana na mtoto wa Hanga. Alisema kuwa baba yake alikufa kifo cha kawaida na alizikwa kwa mujibu wa taratibu zote za dini ya kiislam. Anasema pia kaburi la baba yake lipo

Alaaa kumbee!
Kwani mnadhami hii ni hadithi njoo uongo ukoleee!
Tukubali hawa jamaa wawili hasa othman sharif na hanga waliuliwa kinyama na hakuna kaburi lake.
Na mara ya mwisho wote wawili kuonekana hadhatani ni kwenye wa hadhara ambao waliletwa na pingu na kuhukumiwa pale pale uwanjani.
Mwalimu ndie akisherehesha hukumu yao.
Baada ya hapo walipelekwa znz na kule nako wakaletwa uwanjani ma karume akawasimbulia tena na baada ya hapo hawakuonekana tena mpaka leo.
Hii ni jeraha na kovu la uovu.
Tuache propaganda hakuna kaburi lolote na jee othman sharif naye kaburi lake lipo wapi ?
 
Tatizo viongozi wa CCM hawasomi na ndio maana hata kwenye mikataba wana sign madudu.

Lissu amenukuu kitabu, kwa maana hiyo mambo aliyosema bungeni yapo mtaani siku nyingi, lakini kwa sababu ya uvivu wao wa kusoma wanahamaki kumsikia Lissu.

Taifa lolote haliwezi kutulia bila ya kuweka wazi historia yake. Badala ya CCM kumshambulia Lissu watoe majibu juu ya vifo vya hao watu.
 
Ndugu, Kama ni swala la maandiko tu, mbona kuna maandiko ya fiction mengi tu.

Hoja hapa siyo maandiko bali mantiki iliyoko ndani ya maandiko halafu cha kushangaza, anayedaiwa kutenda ndiyo tena anaulizwa kama ametenda.
Aisee napata shida kuielewa hiyo kauli yako BLUE naona unairudiarudia bila hoja. Kwani ukipelekwa mahakani au hata selo za polisi kwa kosa la kuiba kuku, kweli pale utaanza kuhukumiwa tu bila kuulizwa kama uliiba kuku au la? Hapo lazima ujibu NDIO nimeiba au SIO sijaiba jibu ambalo litamuhitaji anayekushtaki sasa aje na hiyo "proof".

So maswali ya Lissu au Upinzani yapo wazi tunahitaji majibu ya upande wa pili na si mipasho...!(Kiufupi maswali yenyewe ni haya: Je ni kweli walikuwa torchered na waliuawa? Je walishtakiwa kwa kosa gani? Je ni mahakama gani iliwashtaki? Wapi wazikwa kwenye handaki moja?)
 
Hapa unacheza na maneno, na hujaja na jibu.

Tunachotaka ni majibu, jee, walikufa kweli wakiwa mikononi mwa Serikali ya Nyerere na au Karume? Jee, walifungwa kwanini kama jibu la kwanza ni ndio. Jee, kama walizikwa kisheria ya dini zao, walizikwa wapi, kwani Tundu Lissu kasema bungeni na hakuna mpaka sasa kauli iliyotoka kujibu shutuma za hawa watu.

Tundu Lissu hakusimama pale bungeni na hoja yake binafsi, Tundu Lisssu alikuwa anaongea hoja za wapinzani. Serikali kukaa kimya kwa hili inatutia mashaka sisi wananchi.

Na hapa naona wewe unakuja kucheza na maneno, inaonesha ni vipi ulivyo na kejeli katika kuonegelea masuala ya binaadam ambao wengi tumesikia juzi bungeni maafa yaliowakuta wakiwa mikononi mwa Serikali. Wala hatukusikia pale bungeni mbunge yeyote akisema Lissu athibitishe aliyoyasema la sivyo afute kauli zake kuwa ni uongo, hatujaona hayo.

Nakushauri amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfano.

Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, na hapa unaongea kama mtu aliyelewa madaraka.

Leo FaizaFoxy kwa kweli arguements zako zimejaa hekima, busara na utu. Kama siku zote tungeweka interest zetu za kichama pembeni na kuangalia utu zaidi/ubinadam zaidi basi kero nyingi za kijamii na kiuchumi zingekuwa zimetatuliwa au kupungua kwa kiwango kikubwa na sehemu kubwa ya wananchi walio maskini sasa wangefaidika na keki ya taifa kupitia miundo mbinu mizuri, elimu bora, huduma za afya zilizoboreshwa, maji na mambo mengine kadha wa kadha.

Mtu kama MwanaDiwani yeye anawaza kwa kutumia tumbo lake na chama chake na anasahau nyuma yake kuna ndugu wengi wanaoumia kwa huu mfumo mbovu lakini angeweka utu ndani yake asingeangalia hoja imetolewa na nani bali angeangalia mantiki ya hoja. Kama kuna watu waliuwawa, its all wrong wawe wameuwawa na serikali ya CCM au serikali ya chama kingine chochote, wawe wameuwawa na Boko Haramu au serikali ya Marekani.
 
Kwa nini huyo anayesema wamezikwa kwenye handaki asiwapeleke kwenye hilo handaki.

Yaani haya maswali yako nje ya mantiki . Hiyo hiyo serikali inadaiwa iliua halafu hiyo hiyo serikali inaulizwa tena kama iliua.

Mind you. The burden of proof rested with the accuser rather than the accused.

We Jamaa sheria umesoma wapi? Mimi sijasoma sheria lakini hapa naona kama unachanganya mambo.
 
Zamani wapinga muungano kama alivyo Tundu Lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais mvumilivu sana kwa sasa
Kwa hali ilivyo sasa inabidi awe mvumilivu la sivyo na huko kutangatanga kwake na kutembeza bakuli kila mahali anaweza akapigwa stop. Hata hivyo anaweza kupata muda wa kujua matatizo ya wananchi wake akitulia inchini. Anaweza kuona watoto wanaokaa chini ,wanaoandikia kwenye magoti yao, wanaosomea chini ya mwembe nk.wasio na maji,wanaokaa kwenye tembe, hospital zisizo na dawa kama Panadol, watu ambao waliuziwa mbegu za pamba silizochakachuliwa nawasijuwe pa kupata fedha za kusaidia maisha yao bila serikali kutoa fidia yoyote.na mengine mengi sana
 
Zamani wapinga muungano kama alivyo Tundu Lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais mvumilivu sana kwa sasa

Endelea kutoa elimu kwa wenzako ambao hawataki kukubaliana na unyama walioufanya kwa watanzania.
 
Hivi muungano unaendeshwa kwa pesa za nani? kama ni wafadhili basi mjue hakuna muungano hapo ila kuna interest za wanaoufadhili. Nasema hivi kwa sababu muungano kama unaendeshwa na nchi wanachama ni lazima nchi husika wachangie, hata kama nchi moja itachangia zaidi. Sasa kama Muungano unatoa fedha tena kupeleka Zanzibar, ina maana Zanzibar wao ni wa kupakatwa tu na Tanganyika maana hakuna wanachochangia kwenye Muungano.
 
Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.

For the first time FaizaFoxy umeandika mambo ya msingi ambayo siyo ya kishabiki hata mimi nimeishqngaa sirikali kwa kutokuja na majibu badala yake wakamshambulia Tundu Lisu hii inaleta maswali mengi sana juu ya serikali inayoamini utawala wa sheria.
 
Aisee napata shida kuielewa hiyo kauli yako BLUE naona unairudiarudia bila hoja. Kwani ukipelekwa mahakani au hata selo za polisi kwa kosa la kuiba kuku, kweli pale utaanza kuhukumiwa tu bila kuulizwa kama uliiba kuku au la? Hapo lazima ujibu NDIO nimeiba au SIO sijaiba jibu ambalo litamuhitaji anayekushtaki sasa aje na hiyo "proof".

So maswali ya Lissu au Upinzani yapo wazi tunahitaji majibu ya upande wa pili na si mipasho...!(Kiufupi maswali yenyewe ni haya: Je ni kweli walikuwa torchered na waliuawa? Je walishtakiwa kwa kosa gani? Je ni mahakama gani iliwashtaki? Wapi wazikwa kwenye handaki moja?)
Ndugu, Kwanza lazima uelewe hii siyo selo achilia mbali mahakama.

Pili, utampelekea mtu sero bila kidhibiti/kielelezo ambacho ni kuku aliyeibiwa?. Lazima kwanza huyo kuku aliyeibiwa awepo.

Tukirudi kwenye hoja, kiko wapi hicho kielelezo/kidhibiti kinachofanya uniulize maswali na hasa unapodai marehemu walizikwa kwenye mahandaki.
 
We Jamaa sheria umesoma wapi? Mimi sijasoma sheria lakini hapa naona kama unachanganya mambo.
Ndugu, kama hujasoma sheria utafahamu vipi mambo ya kisheria na kuanza kuwakosoa wengine ambao hufahamu kama ni wataalam wa sheria.
 
Ndugu, swali lako ni zuri sana.

Hiyo hotuba tunafahamu imeandikwa na CUF na akapewa Tundu Lissu aisome kwa sababu yeye kwa sasa ndiyo mwenye "akili kubwa' ndani ya UKAWA.

CUF nia yao ni kupandikiza mbegu za utengano kwa kumshambulia Mwl. Nyerere wakitegemea kushusha heshima yake katika taifa ili hata hoja zao za Muungano zipate wafuasi.

Unaumwa, a, hebu jibuni kaburi la Kassim Hanga na Sheriff liko wapi Tanganyikaama Zanzibar?
Hivi ni kwanini mpaka leo Rais Jumbe yuko kizuizini Tanganyika kwa miaka yote hiyo? Ni sahihi kuendelea kumuweka kizuizini miaka yote hiyo bila kosa lolote kisa alihoji uhalali wa Muungano?
 
Kama ni uzushi basi waache kuyaongelea na waongelee kuhusu maendeleo lakini kusimama kwa kila mccm na kuanza kumponda Lisu kuonesha kuwa kuna ukweli flani.
Mbona inaonekana mnalazimisha mjibiwe mnavyotaka nyie, serikali iachane na kujibu uzushi kila siku jamaa alishazusha kuhusu hati za muungano na zikaonyeshwa watu mkabaki midomo wazi sasa mtoto wa Hanga amesema serikali ijibu nini tena.

Hakuna wananchi wanaotaka hayo majibu wengi wamezaliwa baada ya muungano na tuko poa, wanasiasa ndio wanaotaka majibu na wananchi msiwasingizie semeni mnachotaka straight.
 
Ndugu, Kwanza lazima uelewe hii siyo selo achilia mbali mahakama.

Pili, utampelekea mtu sero bila kidhibiti/kielelezo ambacho ni kuku aliyeibiwa?. Lazima kwanza huyo kuku aliyeibiwa awepo.

Tukirudi kwenye hoja, kiko wapi hicho kielelezo/kidhibiti kinachofanya uniulize maswali na hasa unapodai marehemu walizikwa kwenye mahandaki.
Kassim Hanga alikuwa waziri mkuu na baadae makamu wa Rais , hivi ni kiongozi yupi alihudhuria mazishi yake ? Kiongozi mkubwa kama huyu hata Sheha asiiwakilishe serikali kweli?
 
Hata mkitupotezea na DENGUE, bado tunataka maswali ya msingi ya mh. Lissu yajibiwe. Kuanzia yale ya BMK mpaka haya ya kwenye Bunge la Jamuhuri. Acheni kuzunguka mbuyu....
 
Ndugu, swali lako ni zuri sana.

Hiyo hotuba tunafahamu imeandikwa na CUF na akapewa Tundu Lissu aisome kwa sababu yeye kwa sasa ndiyo mwenye "akili kubwa' ndani ya UKAWA.

CUF nia yao ni kupandikiza mbegu za utengano kwa kumshambulia Mwl. Nyerere wakitegemea kushusha heshima yake katika taifa ili hata hoja zao za Muungano zipate wafuasi.

Kama mnafahamu hivyo kwamba hiyo HOTUBA iliandikwa na CUF na TL alikuwa msomaji tu, Kwanini sasa mashambulizi yote yanaelekezwa kwa TL, including hata wewe mwenyewe ulimshambulia TL personally?. The bottom line kama hotuba hiyo ya kambi rasimu ya upinzani ni ya UWONGO kwanini nyinyi CCM hamuusemi huo UKWELI ili Watanzania tufahamu chuya na mchele ni upi?!
 
Madaraka na Haki za Bunge
100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
Sasa hapa jamii ndo unamkanya ama kwanini hamkujibia bungeni zaidi mnakwepa kujibu hoja zake badala yake mnamuongelea yeye kama TL!

Hata hivyo sijawahi kuona mnamjibu zaidi ya kuja kwetu na kulialia, kwani sisi ni nani kwa TL? baba yake au mwalimu wake?

Kajibu hoja sisi tunaangalia point za mtu na sio uwongo uwongo wenu wa enzi za kula mizizi na nyama mbichi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom