Tundu Lissu avurugwa.

Tundu Lissu avurugwa.

Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,


Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.


Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.


Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.


My take,


Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.

Lissu utamshitaki kwa kosa lipi??? Hajasema serikali ndio iliyowauwa watuhumiwa amenakili tu vitabu ambavyo mpaka sasa vipo ila kwa uvivu wetu wakusoma ndo maana hatujui au tunaogopa kusema yeye alichosema anaiomba serikali ituambie ukweli kuhusu watu hawa basi lakini kinachotokea ni kumshabulia Lissu. swali kwani Mzee karume aliuawa na nani? na kwa sababu gani vile?
 
Wakuu Sikonge na nyabhingi chuki za faiza Foxy nazijua sana. Hii story inamuhusu pia Baba wa marafiki zangu wa karibu sana. Baba yao aliwahi kuwa balozi mdogo UK, mtoto wa kike wa marehemu wakati yuko Jangwani Sec aliwahi kuwazidi akili walinzi wa Mwalimu Nyerere alipomaliza kuhutubia pale Diamond Jubilee na kumuuliza alipo baba yake. Mwalimu aliwaomba wapambe zake wampangie siku ili aende Ikulu akaonane naye. Mama wa binti alivyofahamu yaliyofanywa na binti yake alikasirika sana na sikusikia tena kilichojiri baada ya hapo, inaelekea mama wa binti alimuonya binti yake kuachana kabisa na issue ile. Msiniulize jina la huyo Baba wa marafiki zangu, ila Lissu kalitaja jina hilo.
 
Bak, nisome hapo juu. Huyu Mjane yeye hasira zake ni Nyerere na Karume kuuwa Waarabu, basi.

Akipita aone Muaraabu anampiga mwanao wa miaka 8, ndiyo kwanza atatafuta fimbo aje amuongezee kipigo.

Tupigane kivyetu bila ya kumuhusisha huyu Kikongwe class mate wake Jaji Warioba.
Mkuu mbona hapo umenigeuza mawazo tena? Hilo nilikuwa sijaliona kabisa. Kumbe kwenye hili anatuzuga? Haya tuendelee na yetu
 
FaizaFoxy umefanya unachoamini, safi sana, napenda sana hata tukitofautiana kwa itikadi ila penye ukweli wote tusimame bila kujali itikadi zetu. Taifa kwanza, uhai ni tunu ya maisha tuliyopewa na Mungu.

MwanaDiwani,

Mbona hujagusia hoja za akina Kassim Hanga na wenzake aliowataja Tundu Lissu kwa majina? wako wapi?

Sijaona hizo hoja zinazowahusu akina Kassim Hanga kujibiwa, Jee, ni kweli waliuliwa na kuzikwa kwenye handaki moja na Nyerere na Karume?

Itakuwa ni kutetea maovu kama CCM na Serikali haijajibu hoja hizo na kuusema ukweli. Hazifai kupuuzwa hata kidogo.

Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.

Hapa unacheza na maneno, na hujaja na jibu.

Tunachotaka ni majibu, jee, walikufa kweli wakiwa mikononi mwa Serikali ya Nyerere na au Karume? Jee, walifungwa kwanini kama jibu la kwanza ni ndio. Jee, kama walizikwa kisheria ya dini zao, walizikwa wapi, kwani Tundu Lissu kasema bungeni na hakuna mpaka sasa kauli iliyotoka kujibu shutuma za hawa watu.

Tundu Lissu hakusimama pale bungeni na hoja yake binafsi, Tundu Lisssu alikuwa anaongea hoja za wapinzani. Serikali kukaa kimya kwa hili inatutia mashaka sisi wananchi.

Na hapa naona wewe unakuja kucheza na maneno, inaonesha ni vipi ulivyo na kejeli katika kuonegelea masuala ya binaadam ambao wengi tumesikia juzi bungeni maafa yaliowakuta wakiwa mikononi mwa Serikali. Wala hatukusikia pale bungeni mbunge yeyote akisema Lissu athibitishe aliyoyasema la sivyo afute kauli zake kuwa ni uongo, hatujaona hayo.

Nakushauri amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfano.

Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, na hapa unaongea kama mtu aliyelewa madaraka.

Hakuna siri Nyerere na Karume ndiyo waliomua Kassim Hanga.
 
Yaani leo nimelog in ili nikupe like tu,then nalog out. Nawapenda wanao simamia misimamo yao like u. Kwenye masuala yanayo gusa taifa tuunganneni kutetea maslai ya umma. Taifa kwanza chama baadae. Keep it on Madam.
 
FaizaFoxy, Una sema ukweli mtupu kuhusu Nyerere alivyo hamishia watu vijijini ( Makao Mapya). Mimi nilikuwa Arusha Kijiji cha Msitu wa mbogo na wazanzi wangu. Tulikuwa na shamba la mbunga hekari 36. Tukalazimishwa kuhamia porini, kijiji cha Maji ya Moto au Makao mapya kama tulivyo ambiwa. Kawawa ndie aliye kuja na mgambo kijijini kwetu. Tukafukuzwa jioni. Tuli hamishiwa mbugani au makao mapya.. Hatukuruhusiwa kuchukua chochote. Tulifika makao mapya usiku. Hakuna maji, chakula, nyumba. Watoto wengi wa shule za msingi especially Karangai Primary School waliuwawa na wanyamapori wakiwa wana kwenda shule. Kipindi hicho nilikuwa na miaka 8. Ninacho kumbuka ni kwamba kila siku, tulikuwa tuna zika watoto wa jika langu ambao wengi wao, walikuwa marafikizangu. Mpaka leo sijaweza kusahau sura zao, na michezo tuliyo kuwa tuna cheza pamoja kabla ya kuhamishiwa Makao Mapya. Hii ilikuwa mwaka 1977. Nashukuru Mungu nilipona lakini kisaikologia, sija pona mpaka leo nikikumbuka jinsi wenzangu walivyo kufa. Nakumbuka harufu ya maiti. Kwa sababu tulipo hamia Ardhi ilikuwa ngumu saana, wazazi wetu hawakuweza kuchimba makaburi marefu. Yanikuwa mafupi saana. Wanyama pori, especially fisi na mbwa waliyafukua. Mimi siyo mwana chama wa chama chochote bali, inafika wakati lazima tuangalie historia yetu na kukubali yaliyo tokea ili tuweze kusonga mbele.
 
Pamoja kuwa FaizaFoxy ni mdini kwa hili tupo boti moja.

Msimuvibishe KICHWA bure huyu FaizaFoxy! Yeye kila kitu huwa anakiangalia kwa JICHO LA UDINI. Ukitaka kumjua FaizaFoxy is hopeless, mwambie kwamba Kassimu Hanga (mwislamu) aliuliwa na Karume (mwislamu) na wala sio Nyerere (Mkiristu) which is an open truth anyway!
 
Sijaona hizo hoja zinazowahusu akina Kassim Hanga kujibiwa, Jee, ni kweli waliuliwa na kuzikwa kwenye handaki moja na Nyerere na Karume?

Itakuwa ni kutetea maovu kama CCM na Serikali haijajibu hoja hizo na kuusema ukweli. Hazifai kupuuzwa hata kidogo.

You are now matured.
Wahehe wanamsemo 'Ukiona nimenyamasa ujue nimekubali"
Serikali imenyamasa,huenda imekubali kuwa ilihusika kimya kimya,watuhumiwa ndio hivyo wametangulia mbele ya haki.Huko akhera kazi kwel kwel wakikutana
 
Hapa unacheza na maneno, na hujaja na jibu.

Tunachotaka ni majibu, jee, walikufa kweli wakiwa mikononi mwa Serikali ya Nyerere na au Karume? Jee, walifungwa kwanini kama jibu la kwanza ni ndio. Jee, kama walizikwa kisheria ya dini zao, walizikwa wapi, kwani Tundu Lissu kasema bungeni na hakuna mpaka sasa kauli iliyotoka kujibu shutuma za hawa watu.

Tundu Lissu hakusimama pale bungeni na hoja yake binafsi, Tundu Lisssu alikuwa anaongea hoja za wapinzani. Serikali kukaa kimya kwa hili inatutia mashaka sisi wananchi.

Na hapa naona wewe unakuja kucheza na maneno, inaonesha ni vipi ulivyo na kejeli katika kuonegelea masuala ya binaadam ambao wengi tumesikia juzi bungeni maafa yaliowakuta wakiwa mikononi mwa Serikali. Wala hatukusikia pale bungeni mbunge yeyote akisema Lissu athibitishe aliyoyasema la sivyo afute kauli zake kuwa ni uongo, hatujaona hayo.

Nakushauri amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfano.

Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, na hapa unaongea kama mtu aliyelewa madaraka.
Ndugu, unayecheza na maneno ni wewe kwa sababu unajenga hoja za kisiasa. Sheria hazina siasa na katika sheria, proof ndiyo kielelezo ambacho ndiyo mwanzo na mwisho. Nimekuambia ulete proof.

Hata maswala ya imani yanahitaji proof. Huwezi kusema serikali imeua watu na kuwazika sehemu fulani halafu ukiulizwa kutoa proof unaanza kusema hili swala halihitaji proof kwa sababu ni suala serious.

Ni afadhari angalau ungeishia tu kusema mauwaji yalifanyika kuliko kuongeza maneno na kusema nini kilifanyika baada ya mauwaji na wapi walizikwa. Kama hizi information zote unazozisema unazo, basi huna hata haja ya kuiuliza serikali ambayo kwa mtazamo wako ndiyo iliyotenda. Kinachotakiwa, nenda ukaripoti polisi ili mahakama itoe haki kwa sababu hiyo ni criminal investigation.

Hili andiko lako hapa chini ukilisoma na kulielewa utafahamu kuwa tayari umeisha hukumu serikali na kwa maana hiyo, unanitaka nisiutetee uovu wa serikali.

Sasa wewe umeishaendesha mashitaka na ukatoa hukumu, halafu tena unarudi kuiuliza serikali kama imetenda maovu. This is fun to say the least!.
Nakushaurim amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfa
 
kuna kabila nyibgi TZ hawajawahi kutoa rais wala waziri mkuu Zanzibar wamepata hiyo nafasi hii sio hoja wana siasa wanakuongopea na wewe unakurupuka tu

Mimi siangalii wanasiasa wanasema nini? Na hayo mambo ya makabila unayajuwa wewe kwa ajili ya kazi ya kutambika. Na pia zilizoungana ni nchi mbili huru Zanzibar na the then Tanganyika na sio makabila. Mwanzoni mwa muungano huu kulikuwa na usawa baina ya pande mbili lakini sasa hivi inaonekana upande wa Tanganyika uliojibadilisha na kuwa ndio Tanzania unajifanya ndio kila kitu. Ifufueni Tanganyika yenu halafu muendelee kuyaonee makabila na mikoa mnayoita ya pembezoni na sio Zanzibar. Hapa hakuna kulala mpaka kieleweke, tumechoka kugonganishwa vichwa huku mkituibia mchana kweupe.
 
Mama FaizaFoxy
MwanaDiwani ni njaa,ujinga,unafiq ndo vinamsumbua.
Huyo ni sawa na yule mtoto wa Hanga aliyekurupuka na kudai kumpeleka Lissu Mahakaman.
Ndugu, Wewe hufahamu hata unachokisema achilia mbali msimamo wako.

Hakuna mtu hatari katika dunia inayochagizwa maono kama kuwa na blind follower kama wewe.

Katika fikra na mtazamo wako, siyo siku nyingi ulituambia FaizaFoxy alikuwa Black widow wa Alshabaab, leo unataka kutueleza amekuwa enlightened.

Misimamo yako inatuasa tukupuuze!.
Mkuu FaizaFoxy ni a Black widow wa Alshabaab, kuwa Makini ni Mwana Mama Hatare sana
cc dudus

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...pindi-cha-uzalendo-itv-leo-saa-1-usiku-2.html
 
Last edited by a moderator:
Tundu Lisu ni Kichaa, mwendawazimu, Zimwi, Shetani, baladhuri, Kenge, gaidi, ibilisi, Lucifa, Jambazi la kisiasa, mzee wa gubu, mbw mwitu.
 
Ndugu, Wewe hufahamu hata unachokisema achilia mbali msimamo wako.

Hakuna mtu hatari katika dunia inayochagizwa maono kama kuwa na blind follower kama wewe.

Katika fikra na mtazamo wako, siyo siku nyingi ulituambia FaizaFoxy alikuwa Black widow wa Alshabaab, leo unataka kutueleza amekuwa enlightened.

Misimamo yako inatuasa tukupuuze!.

Wewe peleka upuuzi wako huko.
Nimempa credit FaizaFoxy kwa kuwa kwa upuuzi uliouleta amesimama katika kweli na si ki Jinga na Ki propaganda kama wewe otherwise ningemchana tu.
Wewe hujijui kabisa na --------- hata kwa vitu ambavyo viko wazi hadi unatia kinyaa.
Hizi njaa mnazoziendekeza zinawadhalilisha sana...
 
Last edited by a moderator:
Hoja za Mhe: Lissu zote huwa ni Misumari mikali kwa CCM. Yaani bila serikali 3 or 1. Huo mchakato wa katiba mpya utakwama tu. Hata mm nitatoa visenti vyangu kuhakikisha unakwama
 
MwanaDiwani kumbe nawe ni kina walewale, hujamjibu Faizafox kitu chochote ni blaablaa tu mkuu umeweka hapa. Nikisema hatuelewi tunachokiandika mtalalama siku nzima. Anyway wenyewe washindwe ni weye utaweza, sanasana utaishia kuonekana bonge ya kichwa vumbi tu
 
Mbona nyie wapumbavu mnahangaika sana na LISSU? MBONA KITENDO CHA UKAWA KUUNGANA KUNWAKOSESHA ISINGIZI? kaeni sawa dawa iwangie. endeleeni kuiba BOT ndio kazi mnayojua
 
Dahhh, Tundu Lissu utaokotesha watu makopo sasa hivi. Yaani huyu hadi kakosa busara kichwani.

Kwa umri wa Tundu Lissu unaweza kumwita Mzee? Tena Mbw mwitu sijui ndiyo kitu gani?

Hata tukisema ni Mbwa mwitu ila naona mwanzo kaitwa Kenge..... mhhhhh Mbwa mwitu na Kenge wapi na wapi?
Tundu Lisu ni Kichaa, mwendawazimu, Zimwi, Shetani, baladhuri, Kenge, gaidi, ibilisi, Lucifa, Jambazi la kisiasa, mzee wa gubu, mbw mwitu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom