Tundu Lissu avurugwa.

Tundu Lissu avurugwa.

Mambo aliyo yasema lisu japo ni ya kisiasa yana ukweli ndo maana watanzania tumechafuliwa kimataifa tunaficha ukweli kwa ajili ya siasa!

Je? ni uongo rais wa Zanziibar mwaka jana kwenye sherehe za Muungano hakukagua gwalide la JWTZ, na kupigiwa mizinga kama amiri jeshi mkuu?.
Je Kati ya Mgeni rasmi, wakati wa kuingia kwenye sherehe hizo alikuwa nani?
Kumbuka mi sio mwana siasa na sio mwanasheria ndo maana ukifuatilia comments zangu nyingi nilisumbuka sana kuuliza hili swala kwani nilizaliwa kwenye utawala wa nyerere.

SASA KUFUMBIA MAMBO YA MSINGI HAYO SI MNAJIFANYA BOKO HARAMU WALIO MTESA MSICHANA KWA KIFO CHA AIBU?
 
kwani ni maneno ya lisu au alinukuu mahali?. na ni hotuba ya lisu au kambi ya upinzani
 
Ndugu, kwani hao wabunge kama walikuwa wanamjadili Tundu Lissu tatizo lako ni nini?.

By the way, hufahamu kama Tundu Lissu alikuwa anajadili watu aliokuwa anadai waliuawa na serikali!.

mkuu TL alikuwa akijadili kero za muungano moja ya kero hizi Ni ukimya na usiri juu ya wapi walipelekwa akina Hanga na kwa nini? Hapa wewe na wabunge wengine, mnajikita kumjadili Tundu Lisu badala ya kujadili hoja yake, hapo juu unanipa maswali zaidi unaponiuliza "kama wabunge wanamjadili Lisu tatizo langu nini?" kweli upo serious?
 
Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.
Ndugu, unasema "waliosemakana". Sasa hiyo "semekama" itaiondoa vipi bila proof. Wewe ndiyo unadai kuwa walizikwa na serikali kwenye handaki moja. Halafu tena unasema hutaki proof. Kwa hiyo unataka jibu la YES or NO and then biashara ya kuuliza swali inaisha.
 
Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,

Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.

Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.

Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.

My take,

Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.

lISU musimuonee alinukuu vitabu vilivyo andikwa sio maneno yake kwanini walioandika vitabu hivyo wasiulizwe? au watanzania wote tuko wavivu wa kusoma vitabu isipokuwa Lisu?
 
Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.

kula "like" dada yangu! hizo ndo hoja tuzitakazo hapa JF. Siyo ushabiki wa kichama hata kwenye mambo sensitive km haya yanayoweza bomoa nchi...
 
mkuu TL alikuwa akijadili kero za muungano moja ya kero hizi Ni ukimya na usiri juu ya wapi walipelekwa akina Hanga na kwa nini? Hapa wewe na wabunge wengine, mnajikita kumjadili Tundu Lisu badala ya kujadili hoja yake, hapo juu unanipa maswali zaidi unaponiuliza "kama wabunge wanamjadili Lisu tatizo langu nini?" kweli upo serious?
Ndugu, haya ni majadiliano kama unadhani siko serious, kuna ignore button!.

Hizi ni hoja za kitoto. Yaani mtu ameishamwambia kuwa ni mwizi halafu unamuuliza tena kama ni mwizi. Nani hapa ambaye hayuko serious.
 
Ndugu, unasema "waliosemakana". Sasa hiyo "semekama" itaiondoa vipi bila proof. Wewe ndiyo unadai kuwa walizikwa na serikali kwenye handaki moja. Halafu tena unasema hutaki proof. Kwa hiyo unataka jibu la YES or NO and then biashara ya kuuliza swali inaisha.

Hapa unacheza na maneno, na hujaja na jibu.

Tunachotaka ni majibu, jee, walikufa kweli wakiwa mikononi mwa Serikali ya Nyerere na au Karume? Jee, walifungwa kwanini kama jibu la kwanza ni ndio. Jee, kama walizikwa kisheria ya dini zao, walizikwa wapi, kwani Tundu Lissu kasema bungeni na hakuna mpaka sasa kauli iliyotoka kujibu shutuma za hawa watu.

Tundu Lissu hakusimama pale bungeni na hoja yake binafsi, Tundu Lisssu alikuwa anaongea hoja za wapinzani. Serikali kukaa kimya kwa hili inatutia mashaka sisi wananchi.

Na hapa naona wewe unakuja kucheza na maneno, inaonesha ni vipi ulivyo na kejeli katika kuonegelea masuala ya binaadam ambao wengi tumesikia juzi bungeni maafa yaliowakuta wakiwa mikononi mwa Serikali. Wala hatukusikia pale bungeni mbunge yeyote akisema Lissu athibitishe aliyoyasema la sivyo afute kauli zake kuwa ni uongo, hatujaona hayo.

Nakushauri amma njoo na majibu ya hayo ki staha na utaarabu amma sema huna majibu, lakini kutetea uovu ni laana kubwa kuliko mfano.

Hakuna ulevi mbaya kama ulevi wa madaraka, na hapa unaongea kama mtu aliyelewa madaraka.
 
Hoja ya Kassimu Hanga ilishajibiwa jana na mtoto wa Hanga. Alisema kuwa baba yake alikufa kifo cha kawaida na alizikwa kwa mujibu wa taratibu zote za dini ya kiislam. Anasema pia kaburi la baba yake lipo

uliongea nae etieee...
 
Hoja za lissu hazijawahi kujibiwa kamwe na mainterahamwe, zaidi ya kumshambulia yeye binafsi! Lissu bado ni mwiba mkali umagambani na interahamwe kiujumla!

Mtu kigeugeu ajibiwe ili iweje? Mtu kama huyo ni kuachana naye na kumtoa maana kabisa!
 
Mkuu faizaFox narudia tena team MwanaDiwani haiwezi kujadili hoja hizi, hasa zenye kumtaja hayati mwalimu (RIP), maandiko yapo Tele, lakini kila atayejaribu kuyasema atatangazwa nchi nzima kuwa "anatukana na kudhalilisha" waasisi. Heko wanaousimamia ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,

Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.

Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.

Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.

My take,

Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.
ntafurahi sana hiyo kesi ikifunguliwa haraka na mapema zaidi ili tupate ukweli halisi. ila nijuavo miyee sidhani kama huyu bwa mdogo ataruhusiwa kufungua hayo mashtaka maana ccm wanajua kabisaa ikifunguliwa kesi haitakuwa ndogo yataibuka mengi zaidi ya kifo cha hanga.. na hapo ndio kutatokea kuumbuliwa kwa serikali ya ccm kwa umafia wake wakati wa enzi za mwalim na mpaka sasa tulipo umafia wa kuua watu muhim kwa manufaa ya wachache tu. TUNASUBIRI KWA HAMU
 
Mbona inaonekana mnalazimisha mjibiwe mnavyotaka nyie, serikali iachane na kujibu uzushi kila siku jamaa alishazusha kuhusu hati za muungano na zikaonyeshwa watu mkabaki midomo wazi sasa mtoto wa Hanga amesema serikali ijibu nini tena.

Hakuna wananchi wanaotaka hayo majibu wengi wamezaliwa baada ya muungano na tuko poa, wanasiasa ndio wanaotaka majibu na wananchi msiwasingizie semeni mnachotaka straight.

Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.
 
Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,

Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.

Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.

Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.

My take,

Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan alikataa kueleza walipo waasisi sita wa Muungano ambao kambi ya upinzani ilidai kuwa waliuawa na kuzikwa handaki moja, badala yake akatumia nafasi hiyo kumshambulia mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akidai hizo ni propaganda na upotoshaji.

Juzi wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Lissu aliitaka Serikali kutoa maelezo bungeni kuhusu sababu za kuuawa kwa waasisi sita wa Muungano wa Tangayika na Zanzibar na kuzikwa katika handaki moja visiwani Zanzibar.

Lissu aliwataja waasisi hao kuwa ni Abdalah Kassim Hanga, aliyekuwa waziri mkuu, Abdul Aziz Twalam aliyekuwa Waziri wa Fedha na Abdulaziz na Saleh Akida aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

Pia aliwataja Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa ambao alisema nao waliuawa na kuzikwa katika handaki moja eneo la Kama nje kidogo ya Zanzibar.

“Tunataka kujua ukweli kama walifanya makosa, walishtakiwa katika mahakama gani iliyowahukumu adhabu ya kifo... tunataka kuambiwa ukweli kwanini mchango wao kuhusu Muungano umefichwa,” alisema Lissu juzi.

Lakini alipoulizwa kuhusu madai hayo, Waziri Hassan alionekana kuzigeuza hoja hizo kuwa ni za Lissu pekee badala ya kambi ya upinzani na kumshambulia mbunge huyo akidai kuwa ni mpotoshaji, anayepiga propaganda na mchochezi.

Waziri huyo, ambaye ni Mzanzibari, alisema alipuuza maswali yote kuhusu waasisi hao akisema mbunge huyo wa Chadema alipotoka katika hotuba yake na ndio maana hakutaka kuzungumzia katika majumuisho ya bajeti ya ofisi yake bungeni.

“Yule Lissu sio mkweli na ndio maana sisi tulimpuuza,” alisema waziri huyo.

“Hakuna kitu kama hicho na endapo kingekuwepo sisi Serikali tungeshatoa ufafanuzi ili watu wapate kujua ukweli wake,” aliongeza Waziri Samia bila kutoa ufafanuzi wa nini kiliwatokea watu hao walioshika nafasi za juu serikalini mara baada ya Mapinduzi na Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

Pamoja na kudai kuwa aliona hoja hizo ni upotoshaji, Waziri huyo, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba, aliwasihi wabunge wa upinzani kupeleka hoja zao katika Bunge Maalumu la Katiba linalojadili uundwaji wa Katiba Mpya, ambalo pia limetawaliwa na suala la muundo wa Muungano na kero zake.
 
Kuuliza akina Hanga leo ni sawa na kuuliza kwanini watu waliuawa katika mapinduzi. Zanzibar ilikuwa kimsingi ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi. Inaonesha amani yetu imetudumaza kufikiri, hivyo watu wanajua maana ya serikali ya mapinduzi aka ya kijeshi?
 
Zamani wapinga muungano kama alivyo Tundu Lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais mvumilivu sana kwa sasa

Umeshasema Zamani ndipo Unyama ulifanyika pasipo Mahakama ya Uhalifu wa kimataifa kuchukua Hatua ! Ni kweli zamani Mengi mabaya yalifanyika na hakukuwa na Maswali ! Hata Karume alimuua Hanga kisha nae akauawa ili kuficha ushahidi, huko zamani idd Amin aliua watu lakini aliishi Saudia hadi anafariki pasipo kufikishwa mahakamani,hapo Zamani kulikuwa na Jela(kizuizini)hiyo jela watu walifungwa pasipo kupitia Mahakamani,Tambua Zamani ni Zamani maisha yalikuwa Analojia Ulimwengu haukutambua Uovu haraka, lakini Ulimwengu wa Digtal ukitenda Unyama unakuwa mgeni wa mahalanma ya Dunia na akina Rais Kenyata.
 
Mbona inaonekana mnalazimisha mjibiwe mnavyotaka nyie, serikali iachane na kujibu uzushi kila siku jamaa alishazusha kuhusu hati za muungano na zikaonyeshwa watu mkabaki midomo wazi sasa mtoto wa Hanga amesema serikali ijibu nini tena.

Hakuna wananchi wanaotaka hayo majibu wengi wamezaliwa baada ya muungano na tuko poa, wanasiasa ndio wanaotaka majibu na wananchi msiwasingizie semeni mnachotaka straight.

Mtoto wa Hanga ni Serikali? kwanza hata majina ni tofauti halafu useme ni mtoto wa Hanga, huyo anaitwa Juma Abdallah Hanga na aliyetajwa na Lissu anaitwa Kassim Hanga, vipi?
 
Kuuliza akina Hanga leo ni sawa na kuuliza kwanini watu waliuawa katika mapinduzi. Zanzibar ilikuwa kimsingi ilikuwa chini ya utawala wa kijeshi. Inaonesha amani yetu imetudumaza kufikiri, hivyo watu wanajua maana ya serikali ya mapinduzi aka ya kijeshi?

Wewe, wacha uongo.
 
Back
Top Bottom