Tundu Lissu avurugwa.

Tundu Lissu avurugwa.

HALI ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, juzi ilikuwa tete baada ya wabunge kuamua kumtolea uvivu kutokana na kauli zake za uwongo zilizodaiwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.

Huku wakionyesha mifano, wabunge wengi waliosimama walimshambulia Lissu kwa kupotosha umma kuhusu masuala mbalimbali ya Muungano huku mengi yakidaiwa kuwa hayana tija wala ushahidi wa kutosha.

Hali hiyo ilijitokeza juzi wakati wa kujadili Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), awali, Lissu, aliwasilisha taarifa ya Kambi ya Upinzani.

Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ndiye aliyekuwa mwiba kwa Lissu, ambapo alisema mbunge huyo amezoea kusema mambo ambayo hayafahamu wala kuwa na uhakika nayo.

Mwigulu, ambaye alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizohusu wizara yake, alisema fedha za misaada kwa kawaida wafadhili hutoa maelekezo ambapo katika hilo, kiasi cha usawa wa asilimia 4.5 hutengwa kabla ya kufanya mgawo husika.
“Naomba tu kwanza niweke kumbukumbu sawa. Fedha wanazopaswa kupata Zanzibar, zimekuwa zikitolewa kwa miaka yote mfululizo kama kawaida.

“Unajua kama mambo huyajui, ni vyema ukauliza. Hata ndugu zangu wa Zanzibar, ni kwa nini msiwaulize viongozi wenu. Bahati nzuri kuna kitengo kinachohusu masuala ya fedha, kuliko kufanya mambo yasiyo na ushahidi.

“Kwa kwaida, fedha za wafadhili ambazo zitatolewa ndivyo mgawo utakavyofanywa. Sasa kama hii iliyoelezwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani kwamba zilitakiwa kiasi cha sh. Bilioni 32. Tulizozipata, tumetafuta uwiano wa 4.5, kiasi kilichobaki tutapeleka Zanzibar,” alisema Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM).

Alishauri kuwepo kwa utaratibu wa kutoa takwimu zinazohusu fedha ili kuwezesha akina Lissu kuelewa kabla ya kuzungumza ndani ya bunge.
Pia, aliwahadharisha wabunge wa Zanzibar kuwa, mambo yaliyozungumzwa na Lissu katika hotuba yake, hayaonyeshi kuwa ana mapenzi ya dhati kwa wananchi wa visiwa hivyo.

“Unajua mtu huyo baada ya kuona chuki aliyoipandikiza Tanzania Bara imekosa mashiko, ameamua kuhamia Zanzibar. Mkivurugana yeye atabaki Singida.

Akinukuu maneno ya Lissu aliyoyatoa mwaka jana kuwa kero za Muungano si mali binafsi ya wabunge, alisema hata watanzania wanakerwa na ubaguzi unaofanywa na Wazanzibari, jambo ambalo ni kinyume cha anayoyasema sasa.
Katika kuonyesha Lissu ni kigeugeu, Mwigulu alisema aliwahi kusema kwamba, Wazanzibari walikuwa wakipendelewa kinyume na jinsi hotuba yake inavyoeleza kwa sasa.

“Yaani wakati mwingine napata shida kuamini kama Lissu ametokea Singida kule ninakotoka mie,” alisema.
Awali, wakichangia hoja hiyo, Mohamed Amour Chombo, alimshangaa Lissu kuwa na mapenzi na watu wa Zanzibar huku awali alikuwa akiwapinga na kuwatolea maneno ya karaha na yenye kukera.

Chiombo, alisema muungano wa sasa baina ya CHADEMA na CUF ni sawa na kuchepuka na kwamba, CUF wanapaswa kuwa macho na Lissu.
“Ndugu zangu acheni mchepuko, rudini njia kuu, hawa wanawapenda leo wana nia yao si bure wenzenu ni sisi,’’ alisema Chombo.

Chombo alisema hotuba ya Lissu ni ya uchochezi na kuwataka watanzani kutokubali kuingizwa katika uchochezi.
“Wewe unaposema muungano hauna maana ujue fedha za uwanja wa ndege zimetokana na nini, acheni michepuko rudini njia kuu.

“Kuna baadhi ya watu wakishapata wimbo Fulani, basi kila wakati atauimba huo huo wakati akienda kula, akienda wapi, sasa ni sawa na Lissu amepata wimbo wa muungano ni huo huo,’’ alisema.
Aidha, kwa upande wake Steven Masele, aliweka rekodi sawa aliposema Wizara ya Mambo ya Nje imewahi kuwa na Waziri kutoka upande wa Zanzibar.

Masele, alisema hayo baada ya kuzuka hoja kwamba Muungano uliopo una upendeleo kwa viongozi wanaotoka Tanzania Bara.
“Jamani niwakumbushe tu kwamba Ahmed Hassan Diria (Marehemu), aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alifafanua Masele.

Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge waliochangia ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri Samia Suluhu Hassan, aliahidi kushughulikia changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi wenye tija.

Intarahamwe mmevurugwa....
 
Huyu jamaa huwa yule mtu wa iramba akisema kitu, lazima akipaishe humu! Nadhani kuna tatizo sehemu!
 
Sijaona hizo hoja zinazowahusu akina Kassim Hanga kujibiwa, Jee, ni kweli waliuliwa na kuzikwa kwenye handaki moja na Nyerere na Karume?

Itakuwa ni kutetea maovu kama CCM na Serikali haijajibu hoja hizo na kuusema ukweli. Hazifai kupuuzwa hata kidogo.

Dada umenikuna mpaka basi. Unapotumia ubongo kikamilifu katika mambo serious kama haya, hata Mungu anatabasamu na kufeel proud.
 
Hakuna siri Nyerere na Karume ndiyo waliomua Kassim Hanga.

Unajua wewe Ritz na FaizaFoxy mnanikosha kweli leo, unajua vyama visitufanye kuwa watumwa wa kutetea kila kitu hata kama kina madhara kwa binadamu.
Hongera kwa kuwa huru kwa kuusema na kusimamia ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Hongereni kwa ritz na faizafoxy kwakubali ukweli nakutetea ukweli...hongereni sna
 
wewe bibi siku familia yako itakapozikwa hai na wale wazee wa mabwepande ndio utaacha kutetea uovu eti ilimradi tu unalipwa buku sabau pale lumumba!!!!shame on you.
Possibly atakuwa kabaki mwenyewe na hivyo chochote atakachofanya hakitosaidia sana..na mkandamizaji atakuwa na nguvu na uhuru usio na kifani kumuadhibu na kucheza na uhai/utu wake apendavyo.
 
MwanaDiwani,

Mbona hujagusia hoja za akina Kassim Hanga na wenzake aliowataja Tundu Lissu kwa majina? wako wapi?

Habari za kina Hanga?

Yelena Khanga - Wikipedia, the free encyclopedia

pia tafuta kitabu cha Issa bin Nasser- Zanzibar: Kinyang'anyiro na Utumwa, kinaongea vizuri kuhusu kilichowakuta kina Hanga Kassim na wenzao.

pia unaweza kusoma posti hii:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...jua-kuhusu-kassim-hanga-na-othman-sharif.html

Halafu tafuta kitabu cha Dkt. Harith Ghassany-Kwa heri ukoloni , kwa heri uhuru. Tafadhali fuata link hapo chini kudownload:

Free Downloading ya Kitabu | Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!


Hizo zote ni historia hai za Zanzibar, ingawa kizazi cha sasa ni ngumu kuijua. Na wala haiishii Zanzibar. Hata Tanganyika ina mambo mengi ambayo masikio ya wananchi wa kawaida haijawahi kuyasikia! Na kama kuna anayeamini kwenye utakatifu wa viongozi....mimi siyo mmojawao kwani mengine yalitokea nikiwa na akili zangu zote.
 
Hilo si lingeulizwa Baraza La Wawakilishi, au kule kwa Karume.
Amani si bado yupo.
Lissu hana akili sana na ukimfuata unaonekana sawa naye.
Kwanini haulizi Dedan Kimathi kaburi lake liko wapi?
Kwani Dedan Kimathi naye alikuwa Mtanzania?
 
Jaman huyu Mama FaizaFoxy leo ananipa raha sana.
Wale Nyumbu wa lumumba ambao wao kila kwao ni sawa tu so long as CCM Lumumba imesema leo Povu limewaisha kabisa na Mpaka.mtoke damu puani.
Cc MwanaDiwani, Lizaboni MWALLA ifweero, abakorakam
Kabla sijamuelewa Faiza Foxy nilikuwa namchukia sana! nilikuja kujilaumu sana kwamba sikumtendea haki mama huyu. Mama huyu husimamia ukweli daima hata kama unaumiza. Tangu hapo namheshimu sana. Kunasiku aliwahi kuwazukia hata watu wanaojidai ni watetezi wa uislam wakati wamebeba ajenda zao binafsi.
 
Kabla sijamuelewa Faiza Foxy nilikuwa namchukia sana! nilikuja kujilaumu sana kwamba sikumtendea haki mama huyu. Mama huyu husimamia ukweli daima hata kama unaumiza. Tangu hapo namheshimu sana. Kunasiku aliwahi kuwazukia hata watu wanaojidai ni watetezi wa uislam wakati wamebeba ajenda zao binafsi.

Mkuu,
Hata mimi aisee. FaizaFoxy. Tafadhali Mama ninaomba niku PM tuandae kaji date nikupige hata Beer Mbili tatu za Samahan kwa Makwaz yote niliyokukwaza hapa Jukwaan.
Natanguliza shukran
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,


Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.


Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.


Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.


My take,


Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.

HAPA NI AKILI NDOGO NDIYO INAYOSUMBUA!

Wakati anayasema haya, Tundu Lisu alinukuu kitabu ambacho kipo mitaani siku nyingi sana. Hivi ndo kusema kitabu hicho walikuwa hawajakiona hadi kumjia juu hivi? Kwa nini huyo mwandishi hakujibiwa mara tu alipotoa chapisho la kitabu hicho?
Huyu anayejiita mtoto wa Hanga kama kweli ana uchungu na mzee Hanga alikuwa wapi siku zote asitoe ufafanuzi huu baada tu ya chapisho la kitabu?
 
Siku nyingine huwa unanifurahisha sana kwa hoja zako zilizotulia dhidi ya chama chenu cha MACCM, natamani ungekuwa hivi kila siku iendayo kwa Muumba wetu ili uhoji mengi sana ambayo ni kero kubwa sana kwa Watanzania walio wengi, hongera zako.


Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.
 
Hakuna siri Nyerere na Karume ndiyo waliomua Kassim Hanga.
lazima watu kama lisu wawepo kuchokonoe mambo haya magumu ili ukweli uanikwe,children lost fathers,mothers lost sons!!!halafu wanapigiana upatu wa utakatifu,..binadamu wana mahaba ya ajabu sana kama wewe na magamba...hivi kuna binadamu mtakatifu duniani!!
 
Siku nyingine huwa unanifurahisha sana kwa hoja zako zilizotulia dhidi ya chama chenu cha MACCM, natamani ungekuwa hivi kila siku iendayo kwa Muumba wetu ili uhoji mengi sana ambayo ni kero kubwa sana kwa Watanzania walio wengi, hongera zako.
mkuu reserve your hongeraz,mimi mwenyewe nimekubaliana na hoja zake nyingi humu lakini black widow ukimsoma kwa makini utagundua she has got her revenge,ukitaka kumkata stimu chezea imani yake ndio utajua msimamo wake...apart from that ametetea utu leo lakini sijawahi kuona akitetea rasilimali za taifa(hapa huwa ana-side na ustaadh kikwete hata kwenye makosa)
 
Tatizo lake FF ni Mdini na anasujudu Waarabu. Hapa Muarabu hata awabake watoto wenu, yeye ataendelea kumtetea Muarabu na kuwakandamiza watoto wenu. Atakuja na maneno kama "watoto wenu waliomba kubakwa" au "walivaa nguo fupi" nk nk
Kwa hili tuko naye kwa sababu Nyerere na Karume waliwauwa hawa Waarabu waliouza Mababu zetu utumwani na kututawala. Ila huyu huyu kesho ataanza kumtukana Lissu kwa kuishambulia CCM.

Kabla sijamuelewa Faiza Foxy nilikuwa namchukia sana! nilikuja kujilaumu sana kwamba sikumtendea haki mama huyu. Mama huyu husimamia ukweli daima hata kama unaumiza. Tangu hapo namheshimu sana. Kunasiku aliwahi kuwazukia hata watu wanaojidai ni watetezi wa uislam wakati wamebeba ajenda zao binafsi.

Mkuu,
Hata mimi aisee. FaizaFoxy. Tafadhali Mama ninaomba niku PM tuandae kaji date nikupige hata Beer Mbili tatu za Samahan kwa Makwaz yote niliyokukwaza hapa Jukwaan.
Natanguliza shukran
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bak, nisome hapo juu. Huyu Mjane yeye hasira zake ni Nyerere na Karume kuuwa Waarabu, basi.

Akipita aone Muaraabu anampiga mwanao wa miaka 8, ndiyo kwanza atatafuta fimbo aje amuongezee kipigo.

Tupigane kivyetu bila ya kumuhusisha huyu Kikongwe class mate wake Jaji Warioba.

Siku nyingine huwa unanifurahisha sana kwa hoja zako zilizotulia dhidi ya chama chenu cha MACCM, natamani ungekuwa hivi kila siku iendayo kwa Muumba wetu ili uhoji mengi sana ambayo ni kero kubwa sana kwa Watanzania walio wengi, hongera zako.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa nini huyo anayesema wamezikwa kwenye handaki asiwapeleke kwenye hilo handaki.

Yaani haya maswali yako nje ya mantiki . Hiyo hiyo serikali inadaiwa iliua halafu hiyo hiyo serikali inaulizwa tena kama iliua.

Mind you. The burden of proof rested with the accuser rather than the accused.

kuweka rekodi sahihi, mkuu ufute msitari wa mwisho , hauna maana kisheria , iyo statement iko vague na inatofautiana kwa kila seti ya kesi...mengine mnaweza kuendelea kubishana!!
 
Back
Top Bottom