Natamani sana nimuone huyo mtoto anaenda mahakamani, ndipo mbivu na mbichi za Zanzibar na Tanganyika zitapojitokeza.
MwanaDiwani anashindwa kuelewa kuwa maandamano ya Tunisia yalianza kwa mtu mmoja kuilalamikia Serikali kuwa haitoi majibu kwa dhulma zilizofanyika zamani na akaamuwa kujichoma moto hadharani, hilo ndilo lililopelekea utawala kuangushwa., huo kuangushwa na effect yake ikawafikia Wamisri, Walibya na kwingineko.
Hakuna kitu kibaya kama Serikali kutoa kauli za kuwafanya watu wote ni wajinga.
Nikimsoma huyu
MwanaDiwani kwa masuala nyeti kama haya na niliposikiliza William Lukuvi aliyoyaongea Kanisani nnawaweka katika kundi la unafik wa hali ya juu sana. Na watu kama hawa hawakitakii mema chama changu cha cha CCM na wala hawamtakii mema Rais Jakaya Kikwete.