Tundu Lissu ashtakiwa

Kweli watanzania tunayo kazi kubwa ya kuwatoa ujinga watu kama nyie.

Umtoe nani ujinga na elimu yako ya kuungaunga pale magogoni? Kamsaidie Nape kwanza ndio uje kutusaidia great thinkers...
 
Nani ameweza kutekeleza aliyo ahidi? tupe jina kijana
Bwana Green guard, Mbunge wangu wa upinzani kafanya robo ya aliyotuahidi ikiwa na kuanza kuwasomesha watoto wasiojiweza zaidi ya 250, ahadi nyingine ni kujengewa shule ya watoto wenye maisha magumu na sasa zinapigwa mabati,.Magari manne ya ambulance aliyotuahidi yamekuja. Jifunze wingi na umoja pindi unapozungumzia jambo lolote bwana mdogo.
 
Nani ameweza kutekeleza aliyo ahidi? tupe jina kijana

Mkuu, Mbunge ni mwakilishi wa wananchi kwa serikali yenye mamlaka ya kukusanya kodi, yaani serikali ya ccm! Ambayo ndiyo iliyoahidi kutekeleza ahadi mbalimbali! Wabunge waulizwe wamefuatilia vipi kutekelezwa kwa ahadi hizo za serikali?
 
wana JF kumbukeni nilisema mimi humu humu jamvini kwamba; miongoni mwa watu ambao hawatarudi bungeni 2015, ni mh. Tundu Lissu pamoja na uwezo na umahiri mkubwa alionao katika kujenga hoja bungeni. sababu kubwa ya kutorudi kwake bungeni 2015 ni kwamba anajishughurisha zaidi na harakati za ukombozi wa nchi kwa ujumla wake kuliko kushughulikia matatizo yaliyopo jmboni kwake!

ushauri wangu kwakwe, atenge muda wa kushughulikia matatizo ya jimboni kwakwe, la sivyo hali yake itakuwa ngumu 2015!
 
Mbunge gani wa upinzani alie weza kutekeleza ahadi zake? Hawa ni domo tu, Lissu yuko busy kwenye maandamano hana muda na jimbo lake.
Ni zipi hizo ahadi alizowaahidi? Maandamano ni haki iliyotolewa kikatiba na usipofanya maandamano hasa kupinga udhalimu wa serilkali za kimafioso utakuwa huitendei wema haki yako kikatiba.
 
Kwa muda huu mfupi.amekomesha uwizi wa serikali uliobatizwa la "michango ya maendeleo" ambayo inatumika kuchangia harusi ya akina lazaro nyalandu badala ya kupelekwa ilikokusudwa.!na hapo hana dola.Magamba choka mbaya.
 
Kweli watanzania tunayo kazi kubwa ya kuwatoa ujinga watu kama nyie.

Katimiza ahadi nyingi sana si kwa wapiga kura wake tu bali ni kwa watanzania wote, kwangu mie yeye ni mbunge anayewasaidia watu wa Tanzania at a level ambayo watakuja kuyaona matunda for generations to come na ndio maana haishi kutembea na mafaili.

Wabunge wa CCM huwa wanaahidi vitu ambavyo vilitakiwa vifanywe jana. Very short sighted.
 
huyo anayejadili mambo ya Tundu Lissu kushindwa kutekeleza ahadi zake kwanza angeweka wazi ni ahadi zipi ambazo hajatekeleza.Pia naona huyu jamaa atakuwa ametumwa kuja kutumia jf kumchafua Tundu Lissu, maana hata CCM wanajua huyu jamaa ni mziki mnene.JK alipokuwa kwenye kampeni 2010 pale singida alisema"HERI DR SLAA KUWA RAIS KULIKO TUNDU LISSU KUWA MBUNGE"Hapo alikuwa anamaanisha kuwa alikuwa tayari kushindwa na Dr Slaa na akamkabidhi urais kuliko Tundu Lissu ashinde ubunge wa Singida mashariki.
Nawasilisha wakuu
 
yote tuyasemayo, ni kuwafanya viongozi hawa wawe wajibikaji kwa wananchi walio waajiri. Kama tundu lisu hajarudi hata kusema aksanteni, na kuwa mikakati ya kuwakwamua, bado hajawatendea haki na wanaweza kuamua vinginevyo kumumwaga 2015.

kinachotakiwa tuwasihi hawa wabunge wetu, wasiakae mbali na wapiga kura, wawe na ewgular vist kwao, wakague shughuli za kimaendeleo, watoe miongozo ili wananchi waendelee kuwaamini na waone tofauti ya CCM na vyama vingine hasa CDM.
Ntamaholo na wabunge wa geita wameshtakiwa? Maana nasikia nao ahadi zao hawajatekeleza
 
"Tundulisu ashtakiwa na wapigakura wa kata ya ikungi kwa aliyekuwa mlezi wa mkoa wa singida ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa pwani mh Mwatumu Mahiza.kisa tangu achaguliwe hajatimiza ahadi hata moja kazi yake kubeba mafail" Angel Akilimal mtangazaji wa redio ya magamba (uhuru)- status yake ya leo hiyo kenye fb page yake.

Naona magamba sasa wameamua kuwashambulia wabunge wa CDM ambapo ndani ya mwaka mmoja wameanza kuwanyooshea vidole wakati wao nadani ya miaka 50 ya uhuru wameifilisi nchi kwa ufisadi na utawala mbovu wenye kuwagawa watz kwa makundi ya aliyo nacho na asiye nacho.

binafsi nimewahi kukutana na huyu dada Angel na kuchat nae kidogo mambo ya inji hii na wapi tz inaelekea, huyu dada ubongo umeganda kabisaaa...naomba jf member mtafuteni muweze kuongea japo kidogo mambo ya nchi hii,mtashangaa kwa nini ni boc radio uhuru.
 
Bila kujali kwamba Lissua ameshtakiwa kwa nani. Swali la kujiuliza ni kwamba amelipa deni la ahadi zake (maana ahadi ni deni)?

Je JK amelipa madeni ya ahadi zake maana ana madeni lukuki ya ahadi.
 
Bila kujali kwamba Lissua ameshtakiwa kwa nani. Swali la kujiuliza ni kwamba amelipa deni la ahadi zake (maana ahadi ni deni)?

Mkuu wa kaya kashalipa ngapi kati ya zile ahadi za matrilioni? Acheni umasaburi. Huyo mbunge aliyekuwepo kabla ya Lissu alitimiza ahadi ngapi?
 
Bila kujali kwamba Lissua ameshtakiwa kwa nani. Swali la kujiuliza ni kwamba amelipa deni la ahadi zake (maana ahadi ni
deni)?
Kikwete ametimiza ngapi? mbona kigoma ni vichaka ,,dubai ipo wapi? jiji la viwanda tanga? mtwara? acha uzuzu!!!
 
Wakuu, nimejaribu kupitia baadhi ya comments za wana JF, kwa bahati mbaya sijaona chochote cha msingi cha kujadili.
a) Hakuna mkoa wowote hapa TZ wenye mlezi.
b) Hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na mkutano wa wanakijiji hicho na kutolewa malalamiko hayo.
c) Kushitaki ni kutoa malalamiko yako kwa chombo chenye mamlaka ya kumwajibisha mshitakiwa pindi atakapokutikana ana makosa aliyoshitakiwa nayo. Je huyo anayesemekana ati ni mlezi wa mkoa ana mamlaka gani kwa Mh. Lisu?
d) Alitoa ahadi ngapi kwa kijiji hicho? Na kila moja aliipa muda gani wa kuitekeleza kiasi cha kuonekana kwamba hajatimiza
So it's all crap.
 
binafsi nimewahi kukutana na huyu dada Angel na kuchat nae kidogo mambo ya inji hii na wapi tz inaelekea, huyu dada ubongo umeganda kabisaaa...naomba jf member mtafuteni muweze kuongea japo kidogo mambo ya nchi hii,mtashangaa kwa nini ni boc radio uhuru.
Unajua mtu akiwa mnene sana na uwezo wake wa kufikiri unapungua, sio kosa lake.
 
The only group can do this ni wana CCM ambao wanaenda kwa huyo sijui nani .Watu wa Chadema hawawezi kwenda huko zote hila hizi CCM wamebanwa kila kona .Huyu Mwantumu kafanya nini akiwa waziri ? Yaani mnachekesha kweli .Atafanya nini juu ya Lissu ? Lissu ni mwiba CCM akili zimewakimbia wana weweseka tu .
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom