Ama kweli nyani anapokaribia kufa miti yote inateleza.......... Lissu ni Mwanaharakati ambaye kwa wale tunaomfahamu ameanza harakati za kutetea wanyonge tangu akiwa sekondari, Lissu kabla hata ya kuwa Mbunge alipiga Marufuku Wananchi wa Singida Kusini kuchangishwa michango isiyokuwa na tija kwa wana Singida kabla hata ya jimbo hilo kugawanya vipande viliwili kuwa Kusini Mashariki na Kusini Magharibi ili kumlinda Mbunge ambaye alikuwa hakubaliki Mohammed Missanga ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Singida Magharibi.
Amewatetea kwa kutumia ujuzi wake wa sheria watu kutokufungwa hovyo, ametetea wachimbaji wadogo wadogo wa Sepuka na Sambaru huko Mang'onyi kutokunyanyaswa na Polisi.
Tumeona misimamo yake akiwa bungeni hasa akitetea maslahi ya Wana-Singida na watanzania kwa ujumla, lamewatetea wana Tarime kutokana na maonezi ya wawekezaji wa madini, eo hii kama ilivyojidhihirisha kwenye gazeti la Tanzania Daima, mafisadi wamejipanga kufanya propaganda za kuwachafua Watetezi wa Wanyonge lakini watanzania tuko makini na siasa hizi chafu, na kwa taarifa tu, Lissu anakubalika Singida Nzima hata jimbo la MO DJ anaweza kuingiza team na kumng'oa.
Lissu ni Mbunge wa wana Singida wote, alifanya kampeni wana Singida tukamwelewa na ndio maana hata kauli zilizotolewa " Heri Slaa awe rais kuliko Lissu awe Mbunge" ziligonga mwamba ingawa mafisadi walimwaga mapene kama pipi ili kuhakikisha huyu mwanaume wa shoka hatii maguu mjengoni.