Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,691
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imepigwa kalenda hadi Aprili 24, 2025.
Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 3 ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.
Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.
Ukiondoa kesi ya Uhaini, Lissu anashtakiwa pia kwa makosa mengine matatu:
1. Kuchapisha taarifa za uongo: Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 uliharibiwa kwa maelekezo ya Rais (YouTube)
2. Kuchapisha taarifa za uongo: Polisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi. (YouTube)
3. Kuchapisha taarifa za uongo: Majaji ni wa CCM hawawezi kutenda haki, ni wateule wa Rais wanataka uteuzi wa majaji wa rufani. (YouTube)
Soma Pia:
Mbali ya kufunguliwa kesi ya uhaini, April 10, 2025 pia Tundu Lissu alifunguliwa kesi nyingine ya jinai yenye mashtaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo.
1. Shtaka lakwanza, ilielezwa kuwa April 3, 2025 katika Mkoa na Jiji la Dar es salaam Mshtakiwa alichapisha taarifa za Uongo kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa -2024 Wagombea wa CHADEMA walienguliwa kwa maelekezo ya Rais huku akijua ni uongo.
2. Katika shtaka la pili, ilielezwa kuwa April 3, 2025 mshtakiwa alichapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa Polisi wa Nchi hii wanatumika kuiba kura huku akijua kuwa ni uongo.
3 Katika shtaka la tatu, ilielezwa kuwa Aprili 3, 2025 mshtakiwa alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Youtube zikisema kuwa Majaji wa Nchi hii ni CCM na hawawezi kutenda haki kwa kuwa wanapenda kuteuliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani.
Pia soma ~ Adhabu ya uhaini Tanzania siyo lazima kifo

- Jeshi la Polisi Ruvuma latoa tamko kuhusu kukamatwa kwa Lissu, ni sababu ya Uchochezi
- Mwanasheria wa CHADEMA: Polisi wanasema Lissu anatuhumiwa kwa Uhaini, atafikishwa Mahakamani ndani ya Saa 48
- Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
- Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
==============
Mashtaka matatu aliyosomewa Tundu Lissu kwenye Kesi ya nyingine baada ya kesi uhaini