Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Ndugu zangu,
Nimejaribu mara kadhaa jana kumpigia mdogo wangu Tundu aliyeko Ubelgiji lakini simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kama "Kaka mkubwa".Nikamwambia Lissu amemsikia au kusoma ujumbe wa Peter Geleti? Ghafla akachukua simu huku akisema "Kaka najua unataka kujeruhi nafsi yangu kwa kunukuu matamshi yangu kwenye sakata la Barrick mwaka 2017 mmeshinda,hongereni sana" akakata simu.
Kauli yake ilinikumbusha jinsi alivyowahi kusema kwa majigambo kuwa "mtashitakiwa na hamna hata haki mchanga licha ya dhahabu" kauli yake hii iliibua vijana ambao ni wafuasi wake wakaanza kunukuu kauli hiyo huku kila kukicha wakitupa wasifu wa "wazungu" waliokuja kujadili suala la makinikia.
Tuliambiwa mengi zaidi tuliambiwa sifa na wasifu wa Chief operating officer wa Barrick ambaye aliwa kuwa mwanajeshi eti huyu jamaa ni mwanamikakati balaa.Huku vijana wengine kila siku wakifuatilia na kuripoti jinsi gani wanasheria wa Barrick wanajiandaa kufungua kesi MIGA sijui ICJ nk.
Wengi wao leo wamebaki kimya,wameumbuka hakika Tundu Lissu amejeruhiwa tena.
Hii ni JF!