Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,509
- 6,862
Tunaweza kubishana tu mkuu kwa hili, nadhani hapa yanaongea mahaba na chuki kwa mtu; tukubaliane kuto kukubaliana.Ktk Nec alishinda na angeshinda, lkn huu ndo ukweli usopingika, NEC haiwakilishi watanzania wapiga kura wa ndani ya ccm na wa kitanzania wengine. Nje ya Nec jamaa alishabikiwa na Ukawa tu na ccm wachache.
Nalo hili litaleta mjadala? Kwamba ktk kipindi cha kumtafuta mgombea uraisi wa ccm,cdm walikuwa wakimshabikia Lowasa na wangempigia kura hukohuko ccm kama angesimamishwa?
Yaani unambie eti ccm wachache? Ulizisikia zile nyimbo walizoziimba wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm pale ukumbini wakati mwenyekiti anaingia ukumbini mara baada ya kukatwa majina ya wagombea likiwepo na la Lowassa? Nyimbo ambazo zilimkera hadi mwenyekiti mpya na akazizungumza siku anakabidhiwa kijiti?, hivi ile ya uzinduzi wa utia nia wa Arusha nayo unasema walikua ni UKAWA? Unaikumbuka idadi ya wabunge wa ccm waliokwenda Arusha? Unaikumbuka idadi ya wenyeviti wa ccm waliokwenda Arusha? Wakuu wa mikoa na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa ccm? Mimi naweza kua labda nampenda Lowassa (by assumption) na wewe may be unamchukia Lowassa but that does not change the meaning; Lowassa alipendwa sana na wana ccm. Mwisho nakuomba urejee hotuba ya Kikwete wakati anavunja Bunge pale Dodoma, sikiliza wakati Kikwete anawashukuru waliomsaidia, jina la Lowassa lilipofikiwa tu Kikwete ilibidi asimamishe hotuba kupisha ushangiliaji wa wabunge wale wa ccm. Hivi uliisha wahi msikia maremu captain John Komba wewe!? Well, orodha ni ndefu. Naishia hapa.