Tundu Lissu aeleza kwanini walimchagua Lowassa kugombea Urais | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu aeleza kwanini walimchagua Lowassa kugombea Urais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ndege JOHN, Jan 10, 2017.

 1. ndege JOHN

  ndege JOHN JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2017
  Joined: Aug 31, 2016
  Messages: 3,107
  Likes Received: 4,482
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu aeleza kwanini waliamua kumchagua Lowassa kugombea Urais

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini katika utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje kwamba alikuwa na uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita.


  Hayo yalizungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na Global TV Online ambapo alisema pia Lowassa aliongoza wagombea wote katika utafiti huo.


  “Wazungu wakatuambia hivi political personalities zote za Tanzania walimfanyia kila mmoja wao walimfanyia uchunguzi wake, wakatuambia hivi ‘katika wote hao ukimweka huyu na huyu, huyu bwana mkubwa Lowassa huyu yeye peke yake anatembea na asilimia 18 ya Tanzania voters,’ aliyekuwa anamfuata alikuwa na asilimia 11 tu. Kwahiyo Lowassa as Lowassa alikuwa na eighteen percent ya likeability ya kupendwa na hao Watanzania akienda huku anaenda na asilimia 18 ya ziada, akienda huku anaenda na asilimia 18 za ziada nyingine ongezeeni,” alisema Lissu.


  “Tukasema hivi, ‘tunataka kushinda uchaguzi eeh tuzungumze na Lowassa’ na Dkt Slaa akasema tuzungumze na Lowassa tukamwambia ‘Dkt una mawasiliano naye’ akasema ‘sina mawasiliano naye, ila kuna mtu ambaye anaweza akawezesha mawasiliano naye ni nani? Askofu Gwajima’ tunaelewana, so this how we got Edward Lowassa.”
   
 2. ArD67

  ArD67 JF-Expert Member

  #41
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 14, 2016
  Messages: 2,488
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Hawa ni wanafiki sana, ni wanafiki wenzao tu awezaye kumuunga mkono yeyote kati ya hawa. Ufisadi wa Lowasa wametufichulia wao kwa intelijensia zao, na wao wakazikanusha sijui kwa tafiti za nani, ni wanafiki.
   
 3. kopites

  kopites JF-Expert Member

  #42
  Jan 10, 2017
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 4,842
  Likes Received: 4,070
  Trophy Points: 280
  Kama ww unavoamini za wahindi wa twaweza kua magufuli anakubalika asilimia 200.he he hee
   
 4. ArD67

  ArD67 JF-Expert Member

  #43
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 14, 2016
  Messages: 2,488
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Ktk Nec alishinda na angeshinda, lkn huu ndo ukweli usopingika, NEC haiwakilishi watanzania wapiga kura wa ndani ya ccm na wa kitanzania wengine. Nje ya Nec jamaa alishabikiwa na Ukawa tu na ccm wachache.

  Nalo hili litaleta mjadala? Kwamba ktk kipindi cha kumtafuta mgombea uraisi wa ccm,cdm walikuwa wakimshabikia Lowasa na wangempigia kura hukohuko ccm kama angesimamishwa?
   
 5. M

  Maua kilasa JF-Expert Member

  #44
  Jan 10, 2017
  Joined: Aug 6, 2016
  Messages: 1,040
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Stop bluffing. You exactly what took place in the election vote counting.
   
 6. M

  Maua kilasa JF-Expert Member

  #45
  Jan 10, 2017
  Joined: Aug 6, 2016
  Messages: 1,040
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Wangapi waliiMba " Tuna imani na Lowassa........" kama unasema ni wachache wa ccm. Mbona floo nzima ilijaza sauti ikiimba hivyo. Hata jk akabutwaa. Wacha woga.
   
 7. IROKOS

  IROKOS JF-Expert Member

  #46
  Jan 10, 2017
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,190
  Likes Received: 2,623
  Trophy Points: 280
  ... Narudia tena na tena numbers don't lie... Unakumbuka Slaa alipata kura ngapi? Mnyongeni Lowassa mpendavyo but kama alivyosema Lissu mtaji wake kisiasa hata CCM wenyewe hawamsahau. Na kama siyo kumkata Jina kitemi nadhani unajua nini kitengetokea.
   
 8. s

  stesheni JF-Expert Member

  #47
  Jan 10, 2017
  Joined: Mar 25, 2013
  Messages: 414
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 60
  Hao wazungu hata wakiwaambia kula mavi mtakula,wakisema inama chini nifanye mambo,mtainama. Idiotic
   
 9. s

  stesheni JF-Expert Member

  #48
  Jan 10, 2017
  Joined: Mar 25, 2013
  Messages: 414
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 60
  Tundu Lisu wrote it,tena anajisifu kabisa
   
 10. G'taxi

  G'taxi JF-Expert Member

  #49
  Jan 10, 2017
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 3,018
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Anaewaamini CDM na abaki hvyo hvyo
   
 11. Harnandez

  Harnandez JF-Expert Member

  #50
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 29, 2015
  Messages: 410
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Wazungu wakawambia ndo maana Africa tutaendelea kutawaliwa cant we see mpaka wazungu wafanye utafiti ndo wakwambie?????

  Tena msomi mzima unajinadi wazungu wakatuambia shame on you!?
   
 12. bridalmask

  bridalmask JF-Expert Member

  #51
  Jan 10, 2017
  Joined: Jan 14, 2015
  Messages: 2,164
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  ccm bao la mkono ndiyo lililowasaidia na wote wanajua na dunia inajua....ENL alishinda kwa 62%
   
 13. Titicomb

  Titicomb JF-Expert Member

  #52
  Jan 10, 2017
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 3,195
  Likes Received: 2,880
  Trophy Points: 280
  Wanafuata ule msemo the end justifies the means...
   
 14. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #53
  Jan 10, 2017
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  ◇Chadema mabingwa wa kubadili gia angani??
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #54
  Jan 10, 2017
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  >>>Makamanda ni mabingwa wa kubadili gia angani
   
 16. PMsechu

  PMsechu Member

  #55
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 12, 2016
  Messages: 73
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Bro hujajua vile watu wanaumia kuongozwa na chama kimoja chenye fikra zile zile zisizo na tija kwa miaka. Watu walitaka kuonja utamu wa demokrasia ya vyama vingi tena kuamisha madaraka kwenda upinzani. Hivyo Lowassa alitumika kama chambo kuwezesha mabadiliko hayo.
   
 17. sostenes mbwelwa

  sostenes mbwelwa JF-Expert Member

  #56
  Jan 10, 2017
  Joined: Jul 25, 2016
  Messages: 283
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  sasa mlipo shindwa mliwa uliza wanzungu wapi mlikosea
   
 18. b

  baadae sana Member

  #57
  Jan 10, 2017
  Joined: Mar 31, 2013
  Messages: 27
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 5
  Tunachotaka ni kushika dola mengine baadae
   
 19. m

  mmmkme JF-Expert Member

  #58
  Jan 10, 2017
  Joined: Jan 18, 2015
  Messages: 244
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Twaweza wanafahamika...findings zao ukiingia kwny net unazipata..hata kama hukubaliani nazo but they are there to stay! !!!
  SWALI NI KWAMBA...NI KAMPUNI GANI YA WAZUNGUNGU IKIYOWAAMINISHA CHAGADEMA KUWA HUYO FISADI ANA 18% ZAIDI? ??? FINDINGS ZAO ZIKOJE BA TUNAZIPATA WAPI?????
  Kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui Mzungu anayezungumziwa hapo ni KINGUNGE NGOMBALE MWILU....NA YULE TISS MSTAAFU MWANG'ONDA...HAO NDIO WAZUNGU WAKO WALIOWAHAKIKISHIA FISADI LOWA..HASA ATASHINDA
  NAWASHAURI:-- DHARAUNI AIBU TU MUMUOMBE RADHI DR SLAA CHAMA KIENDE...PIA OMBENI RADHI WATANZANIA KUWA FOR 8 CLEAR YEARS MLIKOSEA KUMCHAFUA LOWASSA KUWA NI FISADI NA USHAHID MLIODAI KUWA NAO ILIKUWA KICK YA KISIASA...MTAELEWEKA TI
  MTU MZIMA AKIVULIWA NGUO HUCHUTAMA!!!!! ACHENI UTOTO
   
 20. ArD67

  ArD67 JF-Expert Member

  #59
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 14, 2016
  Messages: 2,488
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Sa we endelea kuamini ndoto za alinacha, na utaendelea kuota hivyo milele. Amekatwa? Na nani sasa? Sa unaingiaje kwenye uchaguzi wa gharama zote zile huku ukiamini kuna posibilite za kukatana? Huu ni wehu ulopitiliza, na kama si wehu coz hakuna kukatana ni ujinga uliofikia kiwango cha upumbavu.

  Hamtakuja myaone makosa mnayoyatenda hadi mfe, watu wataongea kuhusu ukanda nanyi hamtaliona hilo, wehu utawaziba fikra, wataongea udini, hamtaliona, mtapofuka na ujinga, wataongea na ufamilia pia hamtayaona hayo, mtapofushwa na umimi. Kushinei. Mnadhani kwa hali ilipofikia Tz now,,, yenu ni ya msingi??!!??!!???

  Ukanda, ukabila, udini wenyewe unajifia. Ni kipi mkijengacho xaxa???

  Lidumu taifa hili.

  Sijawahi na sitakuja kuwaza kuona cdm kuwa chama cha upinzani cha kisiasa tz,na hakitafanikiwa.

  Wajinga wanakufa, welevu wanazaliwa daily. Badilini mbinu.
   
 21. ArD67

  ArD67 JF-Expert Member

  #60
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 14, 2016
  Messages: 2,488
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  Hayupo. Labda wajinga wachache tu. Mrudisheni Dr. Slaa labda mtashika dafu kidogo. Cdm nje ya ufisadi utasimamaje sasa?
   
Loading...