Tundu Lissu: Acheni kutunga uongo, mshaurini Rais Samia awataje na kuwakamata walionishambulia

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mwanasheria nguli amekuwa mbogo na kutaka watu kutozua uongo kuwa hamkosoi mama Samia kuwa anakubaliana nae. Bali ametaka watu wamshauri ili waliompiga risasi wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baada ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.

====

TL 1.PNG


TL 2.PNG
 
Mwanasheria nguli amekuwa mbogo na kutaka watu kutozua uongo kuwa hamkosoi mama Samia kuwa anakubaliana nae. Bali ametaka watu wamshauri ili waliompiga risasi wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Pia ndugu Lissu amedai kuwa kuliko kuzua uongo bora wamshauri mama Samia ili yeye alipwe haki zake alizoporwa na utawala CCM chini ya hayati JPM.

Lissu amekuwa mbogo baada ya watu wasio wema kuzua kuwa anamsifia mama Samia kwa ukarimu alionyesha baadz ya kumtembelea hospitalini huko Nairobi Kenya.
Huyu pungu kweli! Mdomo wake huo unaobwabwaja na kutusi kila mtu hautoshi kutoa ushauri kwa mama eeh🤔!? Dereva waliomficha na Mbowe wake ndio awashauri wajitokeze na kutajana na walipane wenyewe kwa wenyewe! Na kama nchi kwa yote ya hovyo aliyoipakazia nchi yetu na JPM wetu pia tutahitaji 'compensation'!
Kama ni kweli JPM alitaka kumdhuru mbona harudi nchini baada ya Mh. Dr JPM (Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amen) kuitwa na Muumba wake!?
 
Shukuran ya punda ni mateke, Lisu siku zote anachoangalia yeye ni tumbo lake na sio wema wa mtu yoyote. Kuhusu waliomshambulia aruhusu dereva wake aje ahojiwe na polisi ili waliomshambulia waweze kukamatwa kama anavyotaka. Angalie njia nyingine ya kutafuta pesa za kumlipa Amsterdam.
 
Mama yupo busy na mambo ya msingi... Kiki za risasi zishapitwa na wakati tafuteni mpya.

..wewe unaweza usione kuwa ni jambo la msingi, lakini wapo wengine kwao ni jambo la msingi.

..kinachotakiwa ni HAKI itendeke na waliofanya unyama dhidi ya Lissu na waliowatuma wakamatwe na kujibu mashtaka mahakamani.

..fikiria kama wewe ungekuwa ndio Lissu, mwanafamilia, rafiki, wote tunastahili kulindwa na kutendewa haki tunapopatwa na tatizo kama lililomtokea.
 
Back
Top Bottom