Tundu Lissu, unaweza kuthibitisha tuhuma za wizi dhidi ya Samia Suluhu Hassan?

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Naandika Mimi Rashda Zunde

Huyu mama unayemuita na kumtuhumu kama mwizi ukifikishwa mbele ya vyombo vya sheria utaweza kuweka wazi amekuibia nini? Huyu Rais nchi hii unayemuita mwizi mbele ya wananchi wake na dunia imesikia, ukipelekwa mahakamani utaweza kusema ameiibia nini nchi na ushahidi?

Huyu Rais unayemuita mwizi ndiye kiongozi wa juu PEKEE aliyekuja kukupa pole na kukujulia hali pindi ukiwa na hali mbaya nusu kufa, huyu Rais unayemuita mwizi ndiye aliyekufata nje ya nchi na kuongea nawewe, huyu Rais unayemuita mwizi ndiye aliyehakikisha kesi zako na haki zako unazipata. Haya tuonyeshe kitu gani amekuibia au ameiibia nchi yetu Tanzania.

Kwako Tundu, sote tunajua kwamba unaongea hivyo jukwaani tena kwa jazba sababu wewe na wenzako hamuamini kwamba kweli #mamaanafanikisha Tanzania kuzidi kusonga mbelee maana mlidhani hatoweza kuiongoza hii nchi sababu yeye ni MWANAMKE lakini mwanamke huyu ameweza kuliongoza gurudumu la maendeleo na TANZANIA tupo salama.

Lissu tunajua maslahi yenu ndio maana hamuwezi hata kutoa hoja za maana mpka mtukane watu au kusingiza mambo ya uongo, na hii ni kwa sababu tu Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imeamua kuwa ya ukweli, uwazi na inaruhusu maoni. Lakini kumbuka kutumia uhuru wako vizuri usitukane wala kusingizia watu mambo ya uongo.

Rais Samia Suluhu hawezi kutokea kuanza kujibizana nawewe na kukudhihaki kama ambavyo wewe unafanya sababu mama amejaliwa hekima na ana malezi ya pande mbili lakini wewe mjalaani uliyokosa malezi unayaweza yote hayo sababu ndio upo hivyo.

Kuwa makini na unachoongea na kama hakuna cha kusema kaa kimya sio lazima uongee, yakikukuta yakukuta uje uanze kusema unaonewa kumbe ni mdomo wako mchafu.

Unaruhusiwa kukosoa kwa hoja lakini si kwa matusi au kutoa maneno na taarifa za uongo.

LISSU OMBA MSAMAHA KWA MANENO YAKO MACHAU, KAMA MMEISHIWA HOJA ZA KUONGEA KAENI KIMYA.
1690624599704.png
 
Niliwahi kuandika hapa wakati wa kipindi cha nyuma, pale Mh Rais SSH alipoanza kutafuta maridhiano ya kitaifa. Kwamba hamna kitu mtu atafanya kuwaridhisha viongozi wa CDM hawa wa sasa. Nilisema hivyo kwa kuzingatia jinsi walivyokuwa wanamwita fisadi EL hapo kabla ya kubadilisha gea angani na kuzunguka naye nchi nzima kumuuza kama mgombea wa Urais wa Ukawa.

Hili la bandari ni maamuzi yaliyo ndani ya uwezo wa Mh Rais SSH. Mapungufu ya kimkataba au hayo yanayo itwa makubaliano ya awali yako na kila mwenye uelewa na anayetaka kuelewa anayaona wazi kabisa.

Sasa ni Ibilisi gani anaye mfanya Mh Rais aseme hadharani nimeziba maskio hatujui. Kuna ugumu gani kwa Mh Rais kusema hadharani haya mapungufu yanafanyiwa kazi na ikishindikana kwa upande wa pili kutuelewa tutauvunja haya makubaliano ya awali ambayo yanaleta sintofahamu katika Taifa. Na tutakuwa tayari kwenda huko kwenye mahakama tulizoafikiana kutafuta suluhisho la kufuta makubaliano haya ya awali. Mh hata kuwa wa kwanza kukutana na changamoto za aina hii watangulizi wake wamekutana nazo walizoweza kuzitatua walifanya hivyo na walizo acha viporo amekutana navyo na yeye obvious ataacha viporo hiyo ndio reality ya uongozi.

Itakuwa ni afadhali kwake kuona namna nzuri ya kuachana na vipengele vyenye ukakasi kwenye mkataba huu kuliko kuendelea kungangana navyo. Na Serikali ya Dubai wakikataa kurekebisha na kama wanajifanya hawaoni mambo yanayoendelea hapa nchini kuyapinga makubaliano yao basi watakua hata wao hawaitakii Tanzania na Kiongozi wake Mkuu mema.
 
Hizi id mpya mpya hizi zipo kimkakati sana.

Hakuna mwanasiasa asiye tukana au asiye toa lugha inayo kera.
Rejea kauli za hiyo bi mkubwa "ukinipara nakuparua'
"Ukinizingua nakuzingua"

Lugha kama hizi zisingepaswa kutoka kwa mtu kama yule ila tu ndio hivyo.
 
zunde zunde zunde, kuwa mfalme sio ndo huwezi kukosolewa, na kuwa kiongozi wa nchi jua kabisa ktk watu 60mil.wote ni wako wenye tabia njema na mbaya , ukilijua hiko basi huna sababu ya kutaka kuziba midomo yao kwa vitisho au vinginevyo, sisi wafugaji tuliowahi kuchunga makundi makubwa ya mbuzi , tulikuwa tunawapenda mbuzi wote , japo ktk Hilo kundi bwana weee Kuna wale mbuzi wehu , yaani yeye hatuliii kuchunga ni kuhaha huku na kule ini mladi tu akutie hasira mchungaji , lkn Wala unawavumilia kwa kuwa wote ni Mali yako. So hata wewe zunde jitafakari kwa huo mfano wangu wa mfugaji mbuzi .

Rais ni Mali ya watanganyika wote akiwemo lisu , hivyo lisu Kama anaona Kuna mahali , mambo si shwari ni haki yake kikatiba , kumkosoa , iwe kwa kuonya, au kukaripia . kiongozi Bora ni Yule anayeyapokea yote (ya kufariji au ya kunyongesha, yaani ya kufurahisha au yakukasirisha).

Acha kumtisha lisu hii nchi ni Mali ya watanganyika wote , sio ya familia au watu fulanifulani , watanganyika wote tuko sawa , hakuna aliye special ktk ardhi hii ya Tanganyika.
 
Back
Top Bottom