Tundu Lissu: Ufukuaji wa Machifu unavunja Katiba na Sheria. Samia akemewe

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,095
103,346
DAEAB8D5-E895-441D-ABF3-C09C20E85E66.jpeg

Kupitia mtandao wa ClubHouse Mzalendo wa Kweli Tundu Lissu anahutubia na anaeleza kwa kina historia ya machif. Ameeleza chimbuko la machif wakati wa ukoloni na kufutwa kwake 1965. Anasema katika utawala wa Mwalimu Nyerere bunge la Tz chini ya Katibu Pius Msekwa lilitunga sheria kupiga marufuku machif na shughuli zao na kuondoa kabisa masalia ya machif.

Jamaa anaongea mambo mazito hatua kwa hatua ngazi kwa ngazi. Anaeleza historia kama vile katunga yeye.

Anaendelea. Anasema Katiba ya sasa imepiga marufuku vyeo vya kurithi au jadi ikiwemo uchifu. (Nawaza: Mama Samia hajui Katiba?).

Anasema kurejesha machif ni kitendo cha kijinai. Anamuuliza Rais Samia au Chief Hangaya kama ameamua kupuuza sheria na matakwa ya nchi?

Anasema kama malengo ni mazuri kwa nini Samia hajaanzisha michakato ya kufufua mfumo wa Usultani huko Zanzibar 🤣🤣🤣🤣🤣

"Rais Samia amekuwa na mwenendo wa kudhalilisha na kuipuuza katiba ya JMT. Dawa ya makosa ya kupuuza katiba ni kwa bunge kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani" anasema ☹☹☹

Nasema pamoja na misingi ya Jamhuri na maono ya Mwalimu na mwenyekiti wa CCM kuvunjwa,lakini CCM imekuwa kimya na haijasema chochote. Anashangaa wazee wa nchi ikiwemo Pius Msekwa, NGO na taasisi za kisheria wamekuwa kimya huku vyama vingine vikipigana vikumbo kumpongeza Rais.

Anaeleza kuna malengo ya kisiasa ndani yake na kuvuruga kabisa mfumo huru wa Serikali za Mitaa.

Rais Samia anasema machief watakuwa wanatatua migogoro ya kijamii. Anahoji wenyeviti wa mitaa na mahakama zitakuwa na kazi gani? Samia anasema serikali imetenga fedha za kuanzia. Lissu anaahoji vyanzo ya mapato ya kugharamia shughuli za machief.

Tundu Lissu anahoji mfumo huu utaendeshwa kwa sheria ipi?

Anahitimisha kuwa Katiba Mpya ni muhimu sana kwa sababu nchi inaendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja au kikundi cha watu bila kuhofia chochote
Anasema Rais ana ajenda hatari sana.

Hatua za kuchukua
1. Bunge kutoa azimio la kumuondoa Rais kwa kukiuka Katiba na sheria
2. TLS wanashauriwa kufungua kesi mahakamani. Raia yeyote au taasisi zingine ziungane kwenda mahakamani.
3. Mapambano ya Katiba Mpya yaendelee

Anaongeza kwamba hajaalikwa kwenye ujio wa Rais,ila ikitokea amealikwa ataenda kumwambia Rais mlolongo wa vitu ambavyo anakosea na kumshauri.

Naendelea kumsikiliza kwa makini. Naomba na Rais Samia apewe link amsikilize


 
BABA MORGAN NIMEMUONA MAENEO YA FIRE KWENYE MATAA NA NDINGA LAKE KALIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Wazanzibari wanatunyonya sana.Mashekhe wa uamusho licha ya kuwa na makosa walisamehewa kwa kuwa Ni wanzanzibar huku Mbowe hana hata kosa anasota lumande.Wazanzibar wanaserikali mseto bala huwez ona kitu kama hicho.Wazanzibar wana usultani ulishafutwa huku bara Rais mzanzibar anaturudishia uchifu.Nilitegemea kabisa rais SH aende Zanzibar akasimikwe usultan.
 
Uchifu uachwe uendelee kuwa kama alama ya utamaduni tu.

Lakini Ku institutionalize uchiefu ni sawa na kuutumia kama ulivyotumjwa na wakoloni kutawala na kunyanyasa watu.
 
Ni shughuli za mila na utamaduni, huyo mwamba asitoke povu. Ata ukitunga sheria kuzui ma-chief wapo tu, na watu wao wanawajua
 
Back
Top Bottom