Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aahidi neema kwa Madaktari, Walimu na Vyombo vya Dola

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Mgombea wa Urais wa JMT kwa tiketi cha CHADEMA, Tundu Lissu aahidi neema kwa watu Watumishi wa Umma ikiwemo Madaktari, Malimu na Vyombo vya Dola kwa kulipwa mara mbili ya mshahara wa sasa.

Katika mazungumzo yake na viongozi wake wa ngazi za juu ameeleza kipaumbele chake kikubwa ni kuongeza mishahara kwa Watumishi wa Umma kulingana na maisha ya sasa yalivyo.

Jengine alilotugusia ni kufuata mfumo wa nchi za Ulaya ambazo hulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wiki badala ya kulipwa kwa mwezi.
 
Hata kama hakuna ajira Serikali iwape mikopo yenye riba ndogo wale ambao watakuwa tayari kuungana ili kujiajiri kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo.

Siyo tu kuwaambia graduates kutoka familia za kimaskini wajiajiri wakati hawana mtaji wa kujiajiri.

Asisahau na swala la wahitimu kusotea nyumbani huyu jamaa wa chato alianza kwa mbwembwe sana kuwaondoa wa vyeti feki lakini mpaka sasa vijana Hawaoni tumaini
 
Back
Top Bottom