Tundu Lissu: Unasajili vikundi vya kufa na kuzikana ili iweje? Huu ni Ufashisti na Udikteta

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,150
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lissu amesema Ufashisti na Udikteta una sura hii Serikali kutaka kujua na kudhibiti kila kitu wafanyacho wananchi

Unasajili Vikundi vya Kufa na Kuzikana au vya Ujirani Mwema ili iweje? Amelalamikia Lisu ukurasani X

Mungu wa Mbinguni awabariki Sana.

Pia soma > Msajili wa Jumuiya za Kiraia: Makundi ya WhatsApp kusajiliwa Kisheria kwa TZS 200,000/-

----

Ufashisti na udikteta huwa una sura hii. Serikali kutaka kujua na kudhibiti kila kitu wafanyacho wananchi. Lengo ni kudhibiti uhuru wa wananchi kujiamulia mambo yanayohusu maisha yao. Unasajili vikundi vya kufa na kuzikana, au vya kusaidiana, au vya ujirani mwema ili iweje?

lissu - Ufashisti.png
 
Kabla ya yote huo muda na resources wangewekeza kwenye kutatua changamoto na sio vinginevyo..... Bila TCRA hata bei ya bundle ingekuwa nafuu kuliko otherwise.....

 
Huyu mama badala ya kurekebisha hilo bwawa la Nyerere linalomwaga maji hovyo na kuwakamata waliotajwa kufuja hela kwenye ripoti ya CAG, yeye yuko bize na petty issues. Anasajili kufa na kizikana ili nini?
 
Back
Top Bottom