Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,811
6,504
Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum

Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya haramu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, ?Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'

Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana

Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).

Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.

Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.

Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadhalilisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.

Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.

Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uhalali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.

Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
[video=youtube_share;bB7BxxMepR8]http://youtu.be/bB7BxxMepR8[/video]
[video=youtube_share;jE7oTPXtpas]http://youtu.be/jE7oTPXtpas[/video]

 
acha kupotosha ukweli wewe aliposema kuwa kuna uwongo na udanganyifu alikuwa anamaanisha wana ccm wa hivi leo kama akina HARRISON MWAKYEMBE alipotamka wazi huko nyuma mwaka 1995 katika kitabu chake cha kupatia hiyo Phd aliyonayo huko ujerumani kuwa muungano pekee ambao utaleta usawa zanzibar na bara ni wa serikali tatu tu leo kapewa cheo kageuka
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost
Mimi huwa nadhani wanasheria ni watu wazuri sana katika uwanja wa siasa hasa ukiangalia kwa kutumia darubini katika siasa za nchi za magharibi utakuta kuwa, viongozi wengi wa nchi hizo ni wanasheria na wamefanikiwa/wanafanikiwa katika siasa zao.

Kama hoja yako ni kweli, kwa nini inakuwa tofauti kwa Mh. Tundu Lissu?.
 
Wakuu, hotuba ya Kamanda Lissu Bungeni jana nina uthubutu wa kusema, tena kwa ujasiri kwamba tangu Tanganyika huru iwepo hatujawahi kushuhudia hotuba kali kama ile. Ni hotuba ya kisomi iliyojaa kila aina ya vielelezo na ushahidi, zaidi ya vielelezo 70 (footnotes), sio mchezo.

Ili kukata mzizi wa fitna nawaomba advocates wa Serikali 2 waje na ushahidi na vielelezo visivyo na shaka kukanusha paper ya Kamanda Lissu na sio kupayukapayuka bila mpango wala hoja za maana. I can see kwanini jamaa wanang'ang'ania Serikali 2 kwa udi na uvumba lakini bahati mbaya kwao kadiri wanavyozidi uking'ang'anizi wao ndivyo wanavyozidi kuharibu na kuachwa uchi wa nyama.

Poleni watetezi wa Serikali 2 ambao mnadhani mna akili na uzalendo kuliko Jaji Joseph Warioba, the former Attorney General of the Republic, Prime Minister and VP; kuliko Dr. Salim A. Salim, the former Minister for Defence, Primer Minister, and OAU Chief; kuliko Judge Brig. Gen. Augustine Ramadhan, the former high ranking member of the People's Armed Forces, NEC Chair, and the Chief Justice of the Supreme Court of the People of Tanzania; kuliko magwiji wengine lukuki waliokuwa wamejazana kwenye Tume ya Warioba. Jengeni hoja mueleweke kama Kamanda Lissu alivyofanya na sio kupayuka kama wendawazimu.

Nilistuka sana kusikia eti Nape Nnauye, W. J. Malecela, na Madabida eti wanazunguka huko na huko "kumjibu" Warioba na timu yake iliyojaa vichwa! Are we serious? Kafulila aliuliza Bungeni, hivi Warioba ni binadamu wa kutukanwa nchi hii? Hata kama alifanya makosa anapaswa kukosolewa kwa staha sio kwa matusi ya dhahiri au ya kificho. Kama kweli ni waungwana, CCM wanapaswa kumwomba msamaha Mzee Warioba na watanzania kwa ujumla.

Nakala: Pasco, Chris Lukosi, et. al.
 
acha kupotosha ukweli wewe aliposema kuwa kuna uwongo na udanganyifu alikuwa anamaanisha wana ccm wa hivi leo kama akina HARRISON MWAKYEMBE alipotamka wazi huko nyuma mwaka 1995 katika kitabu chake cha kupatia hiyo Phd aliyonayo huko ujerumani kuwa muungano pekee ambao utaleta usawa zanzibar na bara ni wa serikali tatu tu leo kapewa cheo kageuka
Mimi nipotoshe ili inisaidie nini?.

Mh. Tundu Lissu alianisha mambo manne katika muktadha wa makundi ndani ya CCM na kila jambo lilikuwa na kundi lake. Jambo la nne lilikuwa linamhusu Mwl. Nyerere na siasa za Zanzibar kama nilivyobainisha hapo juu.

Jaribu kuangalia video yake ili upate ukweli na kubainisha vizuri ninachokisema.
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

hapo nyerere anatukanwa au anaambuwa ukwel....na yeye ni nan hasa mpaka akikosea asiambiwe? ni vitu vingap vya kipuuz kafanya nyerere mpaka leo watu wanalumbana na kaishakufa..ni viongoz wangap wabov nyerere kaiandalia tanzania hii...hana uspecial wiwote ni mtu kama wewe kama tundu lisu..akizingua anapewa black and white
 
Kwani Nyerere hakuwa binadamu? By the way, Lissu alikuwa anazungumzia mfumo sio watu. Mwl. Nyerere aliwakilisha watawala, Shivji na Mwakyembe waliwakilisha "wasomi", n.k.
Mkuu, nani amesema hapa kuwa Mwl. Nyerere hakuwa mwanadamu?.

Tukubaliane tu kuwa, Mh. Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi waliogopa na wanaendelea kuogopa kulipasua. Kwa lugha inayoeleweka na wengi, amemchana chana Mwl. Nyerere na pamoja na kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania.
 
Mimi nipotoshe ili inisaidie nini?.

Mh. Tundu Lissu aliamisha mambo manne katika muktadha ya makundi ndani ya CCM na kila jambo lilikuwa na kundi lake. Jambo la nne lilikuwa linamhusu Mwl. Nyerere na siasa za Zanzibar kama nilivyobainisha hapo juu.

Jaribu kuangalia video yake ili upate ukweli na kubainisha vizuri ninachokisema.

Ndiyo unapotosha tena unajaribu kumingo akili za watu wamuone lisu mtukutu,

-hukusikiliza wala kuisoma hotuba ya Lisu peke yako,


Jitafakali kwa kutumia hekima sisi sio wapuuzi wakukubaliana na propaganda zako kupindisha maneno nakuchomekea neno Nyerere pasipostahili ilikukidhi malengo yako.
 
hapo nyerere anatukanwa au anaambuwa ukwel....na yeye ni nan hasa mpaka akikosea asiambiwe? ni vitu vingap vya kipuuz kafanya nyerere mpaka leo watu wanalumbana na kaishakufa..ni viongoz wangap wabov nyerere kaiandalia tanzania hii...hana uspecial wiwote ni mtu kama wewe kama tundu lisu..akizingua anapewa black and white
Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.
 
Back
Top Bottom