Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Kama waliweza kufanya penetration kama hii, usalama wa nchi uko mashakani
kuna shida kuhusu security system yetu ya nchi.

najaribu ku imagine vp kama jamaa angekuwa ni gaidi aingie pale kwa intention ya kufanya tukio kubwa la kigaidi. nahisi ndg zetu wengi wangekufa. maiti zingetapakaa kila kona.
 
kuna shida kuhusu security system yetu ya nchi.

najaribu ku imagine vp kama jamaa angekuwa ni gaidi aingie pale kwa intention ya kufanya tukio kubwa la kigaidi. nahisi ndg zetu wengi wangekufa. maiti zingetapakaa kila kona.
God forbid... I just cant imagine....!!!
 
MATAGA WALIDANGANYA KUMBE HAPA
20210322_180301.jpg
20210322_180258.jpg
 
Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
Acha mambo yako ya uganga wa kienyeji.. sasa mwili unataabika vipi?

Wewe kama inakuuma mwili kuagwa kausha, zima TV zima redio kapae na Ungo mpaka msiba uishe eboohh..
 
Sina hakika kama ni kwa mujibu wa sheria au la. Lakini inaweza kuja tokea siku Mkuu wa nchi akafa halafu ipangwe ratiba ya kumzungusha nchi nzima. Tena kunakoweza kutumika kujinufaisha kwa viongozi na mamlaka kwa mamilioni ya pesa za umma.

Kama Marais walivyokataa kuzikwa eneo maalum la pamoja huko Dodoma, naamini wanaweza pia kukataa utaratibu huu.

Itatosha Mkuu wa nchi akiagwa eneo la makao makuu ya nchi na kisha nyumbani kwake kwa maziko.

Mizunguko mirefu ni kuongeza gharama, maafa ya watu na hata [kuuchosha mwili wa marehemu] bila sababu.

Ule ni mwili tu (corpse) yeye hayupo wala hasikii. Ya duniani hayajui wala hayamhusu tena.
 
Sina hakika kama ni kwa mujibu wa sheria au la. Lakini inaweza kuja tokea siku Mkuu wa nchi akafa halafu ipangwe ratiba ya kumzungusha nchi nzima. Tena kunakoweza kutumika kujinufaisha kwa viongozi na mamlaka kwa mamilioni ya pesa za uma.
Itatosha Mkuu wa nchi akiagwa eneo la makao makuu ya nchi na kisha nyumbani kwake kwa maziko.[emoji1545][emoji1545][emoji1752][emoji1752][emoji1534][emoji1534][emoji1534]
 
Mzee alikuwa ni mchumi sana na alijali sana wanyonge, Msiba kutumia gharama kubwa na kumzungusha maeneo mbali si vizuri na marehemu ili swala hajalipenda kabisa. Kumuaga eneo moja ilitosha sana.

Tumuenzi marehemu kwa kupunguza matumizi mabaya ya pesa kama haya yakumzungusha zungusha kila mahara.

There is nothing to prove , sababu upendo uko moyoni. Hii mizunguko haisaidii kitu katika huu ulimwengu wa digitali.

Mastermind wa hii mizunguko [emoji2960][emoji2960]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia siamini Kama angeamka akakuta avyozungushwa hivi angefurahi kwa jinsi ninavyofahamu Ni uharibifu wa pesa hivi vitu ndio alikuwa hataki ndio maana hata habari za sherehe za Uhuru alistopisha.
 
Back
Top Bottom