Tunatoa wapi Elimu yetu?

Philo_Sofia

Member
Oct 4, 2023
60
94
Tunatoa wapi elimu yetu au msingi wa elimu na mafundisho yetu ni nini? Hili ni swali muhimu katika kuelewa: moja elimu yenyewe, na pili mafundisho yanayotolewa na hiyo elimu.

Katika kuelewa elimu yetu, utafiti unapaswa kuwa katika kuelewa mafundisho gani inatoa kwa wanaojifunza au tunaowafundisha. Tunataka wanaojifunza au tunaowafundisha wawe kitu gani au wajifunze nini kwa elimu hii?

Lengo la elimu kama ilivyo maana yake ni, "kukua na kuendelea". Kwa hiyo tunatarajia kwamba anayepata elimu anakua na anaendelea.

Neno "kukua" katika muktadha wa elimu maana yake ni, 'kubadilika' na neno "kuendelea" ni, 'kuwa bora zaidi'. Maneno 'kukua' na 'kuendelea' katika mantiki ya elimu yana maana ya "mageuzo yenye maendeleo.

Ukizingatia maana ya elimu na uwepo wa vitu ni wazi kwamba elimu ni lazima kama mtu anataka kukua na kuendelea. Kwa kujua ukweli huu, mamlaka imefanya elimu haki ya msingi ya kila mtu popote.

Kwa msingi kwamba elimu ni ya lazima kama mtu au jamii inataka kukua na kuendelea, tunaelewa kwamba elimu sio tatizo bali tatizo ni mafundisho yake.

Elimu yetu inatufundisha nini? Tunajifunza au tunafundishwa nini kwa elimu hii? Na kwa ajili ya kuwa nini? Hapa ndipo ulipo msingi wa swali: elimu yetu inatoka wapi?

Watu waliopewa mamlaka ya kufundisha elimu (wazazi/walezi, walimu na wakufunzi) wanashughulikia nini? Wanakazia kitu gani katika elimu? Ufaulu? Kutafsiri, kuelewa na kujifunza kutokana elimu? Ni nini hasa tunashughulikia katika hayo mawili hapo juu?

Elimu kama ilivyo; iwe rasmi au isiyo rasmi lazima imbadilishe mtu kuelekea chanya kiakili na kimwili. Elimu yoyote: rasmi na isiyo rasmi inakufanya ujifunze, uelewe na kutafsiri vema mambo bila kusababisha uharibifu.

Aidha, kwa sababu ya sifa yake ya kukua na kuendelea elimu inaona kila kitu au jambo kama mambo ya utafiti mwingi na unaoendelea.

Shule na vyuo vyetu au elimu isiyo rasmi, mafundisho yake hayaaksi maana ya elimu. Wanaosoma katika shule na vyuo au walio katika elimu isiyo rasmi hawaonekani kukua na kuendelea. Hakuna mageuzo au hata mageuzo yanye maendeleo.

Elimu inamtoa mtu au jamii kutoka katika upotofu wa mambo na vitu na kumpeleka katika uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu. Hii ndio sifa ya elimu kwamba anayepata elimu anajifunza na kuelewa mambo na pia elimu ya vitu.

Lakini vipi kwenye jamii au familia zetu, mambo yakoje? Kuna mabadiliko yanayotokana na kujifunza? Je, Kuna kukua na kuendelea kwa familia au jamii kutoka hali duni kwenda bora zaidi kiakili na kimwili, kiuchumi na kijamii?

Vipi kuhusu changamoto za kifamilia na kijamii au kitaifa. Je! Zinapatiwa suluhisho au zimebaki vivyohivyo kwa zaidi ya miongo kadhaa?

Kuhusu mabadiliko yanayotokea duniani, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi na teknolojia, elimu yetu inatuandaa kukabiliana nayo?

Muhimu kabis. Je! Elimu yetu inatuwezesha kujifunza na kubadilika tabia kwa ajili ya kuwa watu bora zaidi kiakili na kimwili?

Fikiri kuhusu tamaduni mbalimbali za jamii zetu, ndivyo zinavyotakiwa kuwa kadiri ya akili? Fikiri pia kuhusu ustawi wa watu. Je! Mambo yako sawa?

Tunatoa wapi elimu yetu?
 
Elimu yetu hasa Tanzania hapa, kweli Ina msaada, faida nyingi sana, sema tujifunze kutazama vitu positively na sio kuona negatives tu
 
Back
Top Bottom