Tunataka barabara ya 'Kanisa Road' ifunguliwe! - Lema

Tunataka barabara ya 'Kanisa Road' ifunguliwe! - Lema

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Posts
899
Reaction score
1,108
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


Jana tarehe 28/2/2013 nilifanya ziara ya kutembelea bara bara baadhi katika Jiji la Arusha Mjini , niliambatana na Waandishi wa Habari wa Radio za Arusha Mjini . Baada ya mizunguko yangu nilitoa taarifa kupitia vyombo vya habari hivyo kuhusu utata wa Barabara ya Kanisa Road .

Arusha Mjini kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la msongamano wa Magari na tunauitaji mkubwa wa bara bara na hivyo sio jambo la busara hata kidogo Mtu mmoja kutumia nafasi yake au Cheo chake kufunga barabara .

Barabara ya Kanisa ilifungwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Isidori Shirima miaka michache iliyopita na tulivyohoji sababu tuliambiwa kuwa Mke wake asingependa kuona bababara hiyo inatumika kwani ilikuwa inaleta kero ya vumbi nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa na familia yake.

Tulipoendelea kutaka barabara hiyo ifunguliwe Kaimu Mkurugenzi wa Jiji wakati huo Bwana Estomih Chan'ga alikiri kuwa hawezi kufungua barabara hiyo kwani hawezi kugombana na Mkuu wa Mkoa.

Sasa Watu wa Arusha hawewezi kuendelea kutokutumia barabara hiyo ambayo ingepunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa kwa sababu kama hiyo , na ni Imani yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa Ndg Magesa Mulongo hawezi kuendelea kuwa na ubinafsi wa kumkinga Mke wake na vumbi na familia yake huku Wananchi tulio wengi tukiendelea kuteseka na msongamano wa magari.

Baada ya taarifa hii kwenda kwenye Radio mbali mbali jana kama vile Radio 5 , Mj Radio na nyinginezo , Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha Radio 5 na kuwatisha kwa nini wamerusha hewani matangazo kuhusu ufunguzi wa hiyo barabara na kudai kuwa lugha iliyotumika kwamba hatuwezi kuendelea kuwakinga wake wa Wakuu wa Mikoa Arusha wasipate vumbi wakati Wananchi wengi wanahitaji huduma ya Bara bara hiyo , ilikuwa ni lugha ya uchochezi .

Nirudie kusema kama nilivyoongea jana na Radio , kwamba barabara hiyo haina sababu ya msingi kuendelea kufungwa , ni matumaini yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa atakuwa na Uungwana wa kutosha wa kuona Wananchi wa Arusha wanatumia barabara hiyo.

Pia nalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumika kutishia usalama wa vyombo vya habari na Demokrasia katika Nchi yetu kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana tarehe 28/02/2013 ni muendelezo wa matendo yao kila mara kwenye vyombo vya habari . Hii ni hatari kubwa na hatuwezi kukubali matisho ya aina hii kwani ni njama na jitihada za kuondoa Uhuru wa Habari katika Taifa letu.


Mwisho " Dhambi kubwa kuliko zote Duniani ni uoga " Tunataka bara bara hiyo ifunguliwe na Wananchi waendelea kutumia barabara hiyo.

Godbless J Lema (MB
 
Makubwa tena ya mke wa mkuu wa Arusha zamani, Mh mambo ya kidelila zaidi haya!
 
Je, imefunguliwa? Maana msongamano wa wa magari ni moja ya kero za Jiji la Arusha.
 
Masisiemu yamelewa madaraka bila maguvu hayawezi ifungua ng'o.
 
loh!
hata kuandika jina CCM naona ntapata laana.
 
siku tukiandamana tuhakikishe tunapita njia hiyo.na bila maandamano hii nchi haitasonga itasimama.Nchi yangu Tanzania bila mashinikizo kutoka kila pembe hawajishughulishi.Lema wewe lianzishe sisi tunamalizia.
 
Kaka Lema Endelea na Mapambano mkuu tunakuaminia sana haswa kwenye suala la mbolea ulivyotusaidia Terrat na ,Moshono , hongera kwa kuwabana mafisadi na sasa nasikia wanahojiwa na polisi na takukuru , je hao takukuru wataweza kufanya kazi kweli ?
 
hata mke wa RC analeta usumbufu kwa wananchi,? kweli hii inchi ya kifalme.!
 
Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani. GODBLESS LEMA

 
Hao policcm wamekosa kabisa kazi ya kufanya siku hizi. Kuna haja ya kuanzisha vita na nchi jirani ili waende huko wakapigane na watakaporudi akili zitakuwa zimewarudia vichwani mwao.
 
Lema itisha maandamano tukaifungue.na muda umepita sasa tunataka uchaguzi wa kata maana hatuna wawakilishi wa kata.itisha maandamano tunahamu nayo kwani maji arusha nishida kata zote na machinga tunahamu na wagambo kwani kwa sasa hawavai sare za kigambo wanapiga raia huku wamevaa nguo za homu na baadhi ya wagambo wamerudi makwao kwa madai ya kutolipwa.
 
Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani. GODBLESS LEMA


Nini tena hii jamani? Hapa ni suala la Road jombaa. Hawataki vumbi waweke ki2 cha lami, hawawezi wawe wanamwaga maji asubuhi na jioni vumbi litakoma.
 
Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;
- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)
- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.
- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.
- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.

Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.
 

Attachments

  • Mt Meru Hotel.JPG
    Mt Meru Hotel.JPG
    1.6 MB · Views: 218
  • Mt Meru Hotel.JPG
    Mt Meru Hotel.JPG
    1.6 MB · Views: 188
Back
Top Bottom