Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;
- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)
- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.
- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.
- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.
Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.