Tunataka barabara ya 'Kanisa Road' ifunguliwe! - Lema

Tunataka barabara ya 'Kanisa Road' ifunguliwe! - Lema

Mbona mnatuchanganya? Tumwamini nani sasa?

Kwa hali ilivyo sasa ni kipande cha kama mita 500 hivi ndio kimefungwa kwani barabara inatumika(kwa magari) mpaka kwa mkuu wa mkoa au chinise restaurant.kipande kifupi kilichobaki ndio kimefungwa (barrier ya chuma) ingwa kinatumiwa na watembea kwa miguu na toyo.

Lema amesimama upande wa wananchi wa kawaida na sio wahindi na RC wanaofaidika na barabara hii.

Huu ndiyo ukweli. Mkanganyiko unatokana na unakolezwa kwa viongozi kutokuwa wa wazi na maamuzi yao. Kwa sasa issue ni kuwa barabara ikifunguliwa italeta tija ya kupunguza msongamano ipi au itaathiri nini?
 
Acha jazba mkuu, kukulia Arusha sio kujua kila kitu, kwanza umeona hiyo ramani? Pili kwa kukulia kwako Arusha uliwahi kuona magari yakipita hiyo barabara au yalikuwa yanaishia gymkhana club? Kama una majibu ya hayo maswali jiulize mipaka ya Mt Meru Hotel ni ipi? kiukweli kama sio Idara ya maji pasingetokea kuwepo barabara pale kamwe. Kama ni upotoshaji utakuwa wako mwenyewe maana mimi nina record na nilihusika kufuatilia mipaka ya Mt Meru Hotel wakati inauzwa na hiyo ramani niliyoambatanisha hapo (achana na hizo rangi) ni nakala toka wizarani au bado una jazba?

Nilikuwa nafanya kazi Philips 1977 hadi 1981. Nilikuwa napita hiyo barabara na tuliamini itatengenezwa vizuri zaidi kwa jinsi ilivyokuwa ina manufaa. Kumbuka pia kulikuwa na barabara/daraja ya kupitia mtoni kwenda moja kwa moja AICC uliweza kwenda Mt Meru Hospital kwa urahisi sana. Mpaka sasa hakuna maelezo kwa nini zote hizi hazifunguliwi wakati zilikuwa na manufaa.

Utetezi ninaousoma humu hauzungumzii manufaa ya kufunguliwa barabara bali utetezi usio wa kina. Nakiri mbunge amekoleza siasa kwenye hoja yake lakini hoja ina mshiko labda tatizo details za kisiasa hazikuhutajika.
 
Hivi waliompa Mh Lema majibu ya mke wa RC kutaka ifungue kwa sababu ya vumbi walikua hawana haya maelezo au ni ule uzoefu wa kutoa majibu mepesi mepesi bila kujali matokeo yake!
 
Mbona mnatuchanganya? Tumwamini nani sasa?

haipo kwasababu ni mbunge wa CDM anataka ifunguliwe. Angekuwa mbunge au diwani wa CCM hiyo barabara 'ingekuwepo. Watu wanaingiza siasa kila sehemu. Mbona makinda naye alizuia barabara sinza na diwani aliipigania mpaka ikafunguliwa? Siasa zina mipaka
 
magari yanayoelekea clocktower kutokea maeneo ya sekei yangeweza kuitumia barabara hii badala ya kuleta msongamano pale sanawari.hata wanaokuja mt meru hotel wangepata urahisi badala ya kuzungukia philips au sanawari.niko pamoja na lema kuwa barabara hii ifunguliwe! fredmlay
hatuna muda wa michakato na upembuzi yakinifu!
Kama hamna muda wa michakato mnasubiri nini msiifungue hiyo barabara? Siasa sio kukurupuka kila kitu ni swala la facts, ndio maana wengine hutuita wanaharakati badala ya wanamageuzi...!
 
Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani. GODBLESS LEMA

unachotakiwa kufahamu ni kwamba, hakuna mkristo anayelazimishwa kula nyama iliyochinjwa na muislam,ulichotakiwa kusema hapo ni kwamba kila dini iwe na machinchio yao na mabucha yao, kama ilivyo kila watu wana nyumba zao za ibada
 
Kanisa Roard inaanzia kanisa la Christ Church toka Sokoine Rd na kuishia mahakamani/gymkhana club..
Kama unatoa ufafanuzi toa kwa kuhakikisha ni wa ukweli usipotoshe wana bodi"hiyo barabara inaanzia kanisani old moshi road(sio sokoine road)na kupita gate la mkuu wa mkoa na lami inaishia mwisho wa uzio wa nyumba ya mkuu wa mkoa(sio mahakamani/gymkhana club)kipande cha vumbi kutoka hapo hadi ms/arusha road hakizidi 50mts.NA BARABARA HII KAMA ITAFUNGULIWA KIUKWELI ITAKUWA UKOMBOZI KWA WAKAZI WA ARS NA NI UKWELI PIA KWAMBA TULISHAITUMIA NILISHAPITA HAPO NA GARI MIAKA YA TISINI NA SIO MARA MOJA.
 
Kama unatoa ufafanuzi toa kwa kuhakikisha ni wa ukweli usipotoshe wana bodi"hiyo barabara inaanzia kanisani old moshi road(sio sokoine road)na kupita gate la mkuu wa mkoa na lami inaishia mwisho wa uzio wa nyumba ya mkuu wa mkoa(sio mahakamani/gymkhana club)kipande cha vumbi kutoka hapo hadi ms/arusha road hakizidi 50mts.NA BARABARA HII KAMA ITAFUNGULIWA KIUKWELI ITAKUWA UKOMBOZI KWA WAKAZI WA ARS NA NI UKWELI PIA KWAMBA TULISHAITUMIA NILISHAPITA HAPO NA GARI MIAKA YA TISINI NA SIO MARA MOJA.
Pamoja na kwamba nilikosea kutaja old moshi rd lakini bado si kweli kwamba miaka ya 90 barabara ilipitika kwa gari, huo ni uongo wa wazi na ni aibu kwa mtu mzima kusema uongo.. kanisa rd inakutana na haile selasie rd mahakamani wala si zaidi ya hapo huko kwingine ni siasa ndio zinaleta tabu
 
siku zote maslahi ya wananchi yaheshimiwe. kitendo cha Shirima kufunga barabara kinaonesha uhujumu wa miundombinu ya nchi kwa madhumuni binafsi. Barabara hiyo ilijengwa kwa pesa za walipa kodi ili itumiwe na raia, sasa isipotumiwa si sawa na ufujaji wa fedha za umma???
 
Pamoja na kwamba nilikosea kutaja old moshi rd lakini bado si kweli kwamba miaka ya 90 barabara ilipitika kwa gari, huo ni uongo wa wazi na ni aibu kwa mtu mzima kusema uongo.. kanisa rd inakutana na haile selasie rd mahakamani wala si zaidi ya hapo huko kwingine ni siasa ndio zinaleta tabu

Mimi miaka ya tisin nikiwa najifunza gar tulikua tunatoka hme maeneo ya Sanawari na kwenda uwanja wa mgambo tunapita hiyo barabara. Nilikua napokea gar mara baada ya kuvuka lami na kuanza kile kipande cha vumbi. Wewe ndio unatudanganya hapa. Na sasa ifunguliwe coz mtu unatoka Mt Meru mf kwenda mahakama kuu/yamkoa unalazimika kupita AICC au philips matokeo yake mnaenda kurundikana old ms-arusha road na mzunguko unakua mkubwa(nakadiria 4...km kwa philips au 3....kms kwa AICC/Mt Meru) wakat ukikatisha ni kipande cha mt kama sabini toka barabara ya moshi mpaka geti la mahakama.
 
Pamoja na kwamba nilikosea kutaja old moshi rd lakini bado si kweli kwamba miaka ya 90 barabara ilipitika kwa gari, huo ni uongo wa wazi na ni aibu kwa mtu mzima kusema uongo.. kanisa rd inakutana na haile selasie rd mahakamani wala si zaidi ya hapo huko kwingine ni siasa ndio zinaleta tabu
Wewe ndiye muongo mtu mzima,unatoa mapovu kisa chuki kwa M-bunge wa upinzani,Kama ulikuwa mporipori mie simo,Enzi hizo ndio ilikuwa mitaa yangu Babu yangu alikuwa anakaa hapo uzunguni na hiyo ilikuwa shortcut yetu kwa gari tukielekea hapo Mt Meru hotel ku-swim,pamoja na kuwa hizo 50mts za vumbi zilikuwa kero kwa madimbwi ya maji na lile jabali la kati.KAMA ILIKUWA HATUPITI KWA MAGARI HILO GATE LA BOMBA LILIKUJA WEKWA KUZUIA NINI???Hilo bomba lenyewe ni la kutoa kwani limeshajeruhi watu kadhaa na wengine kuzirai wanapopita wakiwa na pikipiki haswa abiria.,kuna kituo cha bodaboda hapo mwisho wa barabara siku hizi waulize wakulishe habari wengi ni wazaliwa wa sekei sio unarukaruka tu hapa.
 
Wewe ndiye muongo mtu mzima,unatoa mapovu kisa chuki kwa M-bunge wa upinzani,Kama ulikuwa mporipori mie simo.

Enzi hizo ndio ilikuwa mitaa yangu Babu yangu alikuwa anakaa hapo uzunguni na hiyo ilikuwa shortcut yetu kwa gari tukielekea hapo Mt Meru hotel ku-swim,pamoja na kuwa hizo 50mts za vumbi zilikuwa kero kwa madimbwi ya maji na lile jabali la kati.

KAMA ILIKUWA HATUPITI KWA MAGARI HILO GATE LA BOMBA LILIKUJA WEKWA KUZUIA NINI???Hilo bomba lenyewe ni la kutoa kwani limeshajeruhi watu kadhaa na wengine kuzirai wanapopita wakiwa na pikipiki haswa abiria.

kuna kituo cha bodaboda hapo mwisho wa barabara siku hizi waulize wakulishe habari wengi ni wazaliwa wa sekei sio unarukaruka tu hapa.


......

Acha hasira, hoja hujibiwa kwa hoja na penye hoja si chuki.. sina chuki na mbunge na sitawahi kuwa na chuki na mbunge hata iweje, mimi napenda kusimamia hoja, kwanza ungejua itikadi yangu wala usingekurupuka na kusema uliyoyasema ila nikutakie kila la kheri katika mkakati wa kuifungua hiyo barabara iliyofungwa (maana ilikuwepo)
 
Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;

- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)

- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.

- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.

- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.

Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.


......

Ni wakati barabara hiyo ikafunguliwa kwani Arusha ni masikini wa barabara ina barabara kuu chache sana za kuingia na kutoka mjini! Pia Keepleft cha Impala na Clock tower zinasababisha foleni zisizokuwa za lazima ni bora zikaondolewa na zikawekwa taa za kuongoza magari!
 
Acha hasira, hoja hujibiwa kwa hoja na penye hoja si chuki.. sina chuki na mbunge na sitawahi kuwa na chuki na mbunge hata iweje, mimi napenda kusimamia hoja, kwanza ungejua itikadi yangu wala usingekurupuka na kusema uliyoyasema ila nikutakie kila la kheri katika mkakati wa kuifungua hiyo barabara iliyofungwa (maana ilikuwepo)
Am sorry,kilichonipain ni kuniita muongo huku mimi nilikuwa ninapita hapo nikiwa akili zangu timamu.
 
Back
Top Bottom