Tunataka barabara ya 'Kanisa Road' ifunguliwe! - Lema

Fredmlay!

Acha kupotosha watu hapa JF.Ramani uliyoweka ni ya kiwanja cha Mount Meru. Barabara ya " Church road " inaunganisha barabara ya Nairobi -Moshi na ile Old Moshi road. Kama kweli imefungwa I have not been in Arusha recently but nimekulia Arusha hiyo barabara is the only through road before the Golf course na inayofuata kupitia moja kwa moja ni Moshi road kuanzia keep left ya pale Njiro. If they have blocked it that means hata kuzunguka kupitia barabara ya Haile Selasie ina maana lazima warudi Old Moshi Road. Mabadiliko haya yanahitaji baraka za Mipango miji. These RC's are sometimes becoming semi Gods with ukada wa CCM. Tuwaachie Mbunge na Mkuu wa Mkoa wachemke of course na wakazi wa Arusha kupotosha na kusema ulikuwa ni uchochoro is very myopic and creating confusion. Somebody suggested that it should be tarmacked ili kuondoa vumbi or else wamwage maji kama mitigation mpaka wapate pesa.

Acha jazba mkuu, kukulia Arusha sio kujua kila kitu, kwanza umeona hiyo ramani? Pili kwa kukulia kwako Arusha uliwahi kuona magari yakipita hiyo barabara au yalikuwa yanaishia gymkhana club? Kama una majibu ya hayo maswali jiulize mipaka ya Mt Meru Hotel ni ipi? kiukweli kama sio Idara ya maji pasingetokea kuwepo barabara pale kamwe. Kama ni upotoshaji utakuwa wako mwenyewe maana mimi nina record na nilihusika kufuatilia mipaka ya Mt Meru Hotel wakati inauzwa na hiyo ramani niliyoambatanisha hapo (achana na hizo rangi) ni nakala toka wizarani au bado una jazba?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Jana tarehe 28/2/2013 nilifanya ziara ya kutembelea bara bara baadhi katika Jiji la Arusha Mjini , niliambatana na Waandishi wa Habari wa Radio za Arusha Mjini . Baada ya mizunguko yangu nilitoa taarifa kupitia vyombo vya habari hivyo kuhusu utata wa Barabara ya Kanisa Road .

Arusha Mjini kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la msongamano wa Magari na tunauitaji mkubwa wa bara bara na hivyo sio jambo la busara hata kidogo Mtu mmoja kutumia nafasi yake au Cheo chake kufunga barabara .

Barabara ya Kanisa ilifungwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Isidori Shirima miaka michache iliyopita na tulivyohoji sababu tuliambiwa kuwa Mke wake asingependa kuona bababara hiyo inatumika kwani ilikuwa inaleta kero ya vumbi nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa na familia yake.

Tulipoendelea kutaka barabara hiyo ifunguliwe Kaimu Mkurugenzi wa Jiji wakati huo Bwana Estomih Chan’ga alikiri kuwa hawezi kufungua barabara hiyo kwani hawezi kugombana na Mkuu wa Mkoa.

Sasa Watu wa Arusha hawewezi kuendelea kutokutumia barabara hiyo ambayo ingepunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa kwa sababu kama hiyo , na ni Imani yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa Ndg Magesa Mulongo hawezi kuendelea kuwa na ubinafsi wa kumkinga Mke wake na vumbi na familia yake huku Wananchi tulio wengi tukiendelea kuteseka na msongamano wa magari.

Baada ya taarifa hii kwenda kwenye Radio mbali mbali jana kama vile Radio 5 , Mj Radio na nyinginezo , Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha Radio 5 na kuwatisha kwa nini wamerusha hewani matangazo kuhusu ufunguzi wa hiyo barabara na kudai kuwa lugha iliyotumika kwamba hatuwezi kuendelea kuwakinga wake wa Wakuu wa Mikoa Arusha wasipate vumbi wakati Wananchi wengi wanahitaji huduma ya Bara bara hiyo , ilikuwa ni lugha ya uchochezi .

Nirudie kusema kama nilivyoongea jana na Radio , kwamba barabara hiyo haina sababu ya msingi kuendelea kufungwa , ni matumaini yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa atakuwa na Uungwana wa kutosha wa kuona Wananchi wa Arusha wanatumia barabara hiyo.

Pia nalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumika kutishia usalama wa vyombo vya habari na Demokrasia katika Nchi yetu kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana tarehe 28/02/2013 ni muendelezo wa matendo yao kila mara kwenye vyombo vya habari . Hii ni hatari kubwa na hatuwezi kukubali matisho ya aina hii kwani ni njama na jitihada za kuondoa Uhuru wa Habari katika Taifa letu.

Mwisho “ Dhambi kubwa kuliko zote Duniani ni uoga “ Tunataka bara bara hiyo ifunguliwe na Wananchi waendelea kutumia barabara hiyo.

Godbless J Lema (MB

Tanzania inayo maajabu ya ajabu sana, tena maajabu ya hovyo na ya kijinga...!!

Kwakweli, ufala wetu ndio unawafanya hao wajinga (watawala) watutendee kwa hisani zao.
 
Ukitoa tuhuma yoyote lazima kwanza uifanyie uchunguzi wa kina kabla ya kuropoka.Mheshimiwa Godbless Lema kwa mara nyingine tena ameonyesha si mtu makini.
Umeonaee!
Ndio kawaida yao hawa
Unamkumbuka yule mbunge taa ya kandili a.k,a Machemli ya huko Ukerewe akakurupuka na song la nchi kuvamiwa na majeshi ya Uganda na Kenya, na yeye bila uchunguzi........!
Hawa ndio kawaida yao, pengine kaingizwa mkenge na wapambe wake, wala gomba, tayari kashaita MEDIA.

hivyo vyeo vya wakuu wa mikoa vitolewe kwenye katiba mpya!
Who are they???

Kwani unafikiri shida ni Ukuu wa Mikoa, hivyo vyeo vilikuwepo tangu enzi za Ukoloni na mambo yalienda sasa kwa nini kwetu yasiende? Hapo hata ukivitoa hivyo vyeo utaleta vingine, utakachokifanya ni kuhamisha tatizo tu maadamu watu wanabaki kuwa walewale, tatizo sio vyeo au sijui Ukuu wa Mkoa, tatizo ni jamii yetu na Utamaduni wetu, na ukitaka kuthibisha hilo nenda Mikoani kwa Wabunge ambao wamechaguliwa na Wananchi nako hivyo hivyo, 3/4 nzima wanaishi Dar pamoja na Wapinzani ingawaje Ofisi ziko Wilayani! Nina uhakika ukiangalia siku ambazo
Bw.Mbowe anakuwa ofisini kwake huko Hai sidhani kama zitafikia hata miezi 3 kwa mwaka!

Wewe keli kilaza wa head!
Umeonaee!
Ndio kawaida yao hawa
Unamkumbuka yule mbunge taa ya kandili a.k,a Machemli ya huko Ukerewe akakurupuka na song la nchi kuvamiwa na majeshi ya Uganda na Kenya, na yeye bila uchunguzi........!
Hawa ndio kawaida yao, pengine kaingizwa mkenge na wapambe wake, wala gomba, tayari kashaita MEDIA.

Mpaka miaka mitano ya Lema iishe utakuwa umejitia uwendawazimu sana...

I mean utakuwa unaokota makopo Mkuu!
Heshima kwenu wakuu,

Barabara inayozungumziwa haijawahi kutumika kabisa.Mimi ni mkaazi wa Arusha,nimekulia Arusha na ninaishi Arusha ninajua ninachosema.Kimsingi barabara inayozungumziwa ni njia ya miguu nimeitumia sana kipindi nasoma sasa anapotokea mtu na kuzusha barabara imefungwa kwasababu ya mke wa mkuu wa mkoa namweka katika kundi la watu wa hovyo.

Ukitoa tuhuma yoyote lazima kwanza uifanyie uchunguzi wa kina kabla ya kuropoka.Mheshimiwa Godbless Lema kwa mara nyingine tena ameonyesha si mtu makini.
 
Mkuu wangu Bukanga Mwl Nyerere aliwahi kusema hakuna ugonjwa mbaya kama ule wa mtu kufikiri kwaniaba yako.Sasa mimi na wewe nani mgonjwa !.

Mpaka miaka mitano ya Lema iishe utakuwa umejitia uwendawazimu sana...

I mean utakuwa unaokota makopo Mkuu!
 
Last edited by a moderator:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Jana tarehe 28/2/2013 nilifanya ziara ya kutembelea bara bara baadhi katika Jiji la Arusha Mjini , niliambatana na Waandishi wa Habari wa Radio za Arusha Mjini . Baada ya mizunguko yangu nilitoa taarifa kupitia vyombo vya habari hivyo kuhusu utata wa Barabara ya Kanisa Road .

Arusha Mjini kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la msongamano wa Magari na tunauitaji mkubwa wa bara bara na hivyo sio jambo la busara hata kidogo Mtu mmoja kutumia nafasi yake au Cheo chake kufunga barabara .

Barabara ya Kanisa ilifungwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Isidori Shirima miaka michache iliyopita na tulivyohoji sababu tuliambiwa kuwa Mke wake asingependa kuona bababara hiyo inatumika kwani ilikuwa inaleta kero ya vumbi nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa na familia yake.

Tulipoendelea kutaka barabara hiyo ifunguliwe Kaimu Mkurugenzi wa Jiji wakati huo Bwana Estomih Chan’ga alikiri kuwa hawezi kufungua barabara hiyo kwani hawezi kugombana na Mkuu wa Mkoa.

Sasa Watu wa Arusha hawewezi kuendelea kutokutumia barabara hiyo ambayo ingepunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa kwa sababu kama hiyo , na ni Imani yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa Ndg Magesa Mulongo hawezi kuendelea kuwa na ubinafsi wa kumkinga Mke wake na vumbi na familia yake huku Wananchi tulio wengi tukiendelea kuteseka na msongamano wa magari.

Baada ya taarifa hii kwenda kwenye Radio mbali mbali jana kama vile Radio 5 , Mj Radio na nyinginezo , Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha Radio 5 na kuwatisha kwa nini wamerusha hewani matangazo kuhusu ufunguzi wa hiyo barabara na kudai kuwa lugha iliyotumika kwamba hatuwezi kuendelea kuwakinga wake wa Wakuu wa Mikoa Arusha wasipate vumbi wakati Wananchi wengi wanahitaji huduma ya Bara bara hiyo , ilikuwa ni lugha ya uchochezi .

Nirudie kusema kama nilivyoongea jana na Radio , kwamba barabara hiyo haina sababu ya msingi kuendelea kufungwa , ni matumaini yangu kuwa Mkuu wa Mkoa wa sasa atakuwa na Uungwana wa kutosha wa kuona Wananchi wa Arusha wanatumia barabara hiyo.

Pia nalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumika kutishia usalama wa vyombo vya habari na Demokrasia katika Nchi yetu kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana tarehe 28/02/2013 ni muendelezo wa matendo yao kila mara kwenye vyombo vya habari . Hii ni hatari kubwa na hatuwezi kukubali matisho ya aina hii kwani ni njama na jitihada za kuondoa Uhuru wa Habari katika Taifa letu.

Mwisho “ Dhambi kubwa kuliko zote Duniani ni uoga “ Tunataka bara bara hiyo ifunguliwe na Wananchi waendelea kutumia barabara hiyo.

Godbless J Lema (MB

Barabara ya kanisa ikifunguliwa ni lazima na Barabara ya Msikiti nao ufunguliwa hii ndio haki! kinyume chake huo ni Udini!
 
Haya makubwa tena? wake za wakubwa si wakake Ikulu ndogo jamani!
 
Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;
- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)
- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.
- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.
- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.

Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.

Lema haya yote anayajua vizuri sana, ila anatafuta sababu ya kuitisha maandamano tukwa sababu anajua wafuasi wake wengi ni bendera fuata upepo...
 
magari yanayoelekea clocktower kutokea maeneo ya sekei yangeweza kuitumia barabara hii badala ya kuleta msongamano pale sanawari.hata wanaokuja mt meru hotel wangepata urahisi badala ya kuzungukia philips au sanawari.niko pamoja na lema kuwa barabara hii ifunguliwe! fredmlay
hatuna muda wa michakato na upembuzi yakinifu!
 
Last edited by a moderator:
Tuache ubishi Arusha tunaijua kama mzee wetu Mohamed Said anavyoijua Gerezani.

Kwa hiyo barabara ilikuwepo ndiyo maana unaikuta lami chakavu. Lakini suala lililopo je ifunguliwe isifunguliwe ndilo sisi wana wa Arusha tunahitajika kuwa na msimamo.
 
Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;
- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)
- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.
- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.
- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.

Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.

Unaposema baada ya muda mrefu kupita una maana gani? Miaka 10, 15, au zaidi ya 20?
 
Mimi binafsi nimepita na gari njia hiyo kwenye miaka ya 1978. Nilidhani imefungwa kwa sababu ya mahakama.

Hapo hapajawahi kuwa na barabara gari tuacheni ushabiki palikuwa na njia ya miguu na kulikuwa na jiwe kubwa la asili,mbele yake kulikuwa na mfereji na kalavati ambalo ilikuwa watu wawili hawapishani.bora angesema barabara iliyokuwa inatoka AICC Kwenda kuungana na barabara ya kanisa hadi uwanja wa gofu ambayo daraja lake lilivunjika miaka ya 70 hii barabara ilikuwa inafika hadi sabasaba hotel pembeni ya KK securty.

Mbona mnatuchanganya? Tumwamini nani sasa?
 
kwa hali ilivyo sasa ni kipande cha kama mita 500 hivi ndio kimefungwa kwani barabara inatumika(kwa magari) mpaka kwa mkuu wa mkoa au chinise restaurant.kipande kifupi kilichobaki ndio kimefungwa(barrier ya chuma) ingwa kinatumiwa na watembea kwa miguu na toyo.
Lema amesimama upande wa wananchi wa kawaida na sio wahindi na RC wanaofaidika na barabara hii.
 
Ki msingi barabara inayozungumziwa haipo kwenye ramani ya mji, si kwamba iliwahi kutumika ikafungwa, mpango mzima uko hivi;
- Eneo ambalo sasa barabara hiyo inapopitia ni eneo la Mt Meru Hotel (mzunguko wa rangi nyeupe), lakini eneo hilo lilimegwa na serikali ili kuweka visima vya maji vinavyopsimamiwa na Idara ya maji (tazama ramani ya eneo kiwanja chenye mzunguko wa zambarau)
- Idara ya maji walikuwa hawana access ya kufikia visima vyao hivyo wakawa wanatumia eneo la hoteli kutokea barabara ya Moshi/Arusha, na hoteli waliridhia hilo kwa muda mrefu na hiyo ikasababisha kuwepo kwa njia ya miguu (sio magari) kwa raia waishio maeneo ya jirani. Tazama ramani barabara/njia ya mguu ina rangi ya njano.
- baada ya muda mrefu kupita njia hiyo ikaanza kupita toyo/pikipiki na baadhi ya watu wasiojali magari yao wakaanza kuipita lakini kwa tabu maana kulikuwa na jiwe kubwa la asili katikati ya njia.
- Katika ramani hiyo hapo kiwanja chenye nyumba ya mkuu wa mkoa kina mzunguko wa rangi nyekundu, barabara ya asili inaishia hapo kwenye hicho kiwanja, lakini kwakuwa idara ya maji hawakuwa na njia maalum ilibidi wapewe access kutokea upande mwingine ambao ukiangalia utaona hata ramani inaonyesha.

Mimi nafikiri si vema kukurupuka kwa kila kitu, barabara hiyo ni muhimu na Mt Meru hotel wameridhika na mabadiliko ndio maana hata uzio wao wameuimarisha kulingana na uhitaji wa wananchi, ni vyema mbunge wetu akatumia njia ya majadiliano ili mipango miji waingize hii barabara katika mipango ya mji ikiwezekana hata kwa kuwafidia wawekezaji kwa kutoa eneo lao.

Just wondering - Kama haikuwepo ilipataje Jina la Kanisa Road?
 
hata mke wa RC analeta usumbufu kwa wananchi,? kweli hii inchi ya kifalme.!

Enyi watanzania, hivi hamjui ya kuwa mke wa RC naye ni RC!? someni vizurii katiba ya gambaz sura ya 6 kifungu (a) (iV) para ya pili, inaeleza wazi wajibu wa mke wa RC kama mama kada wa maccm wa mkoa. Hiyo imewekwa ili RC asinyimwe unyumba hali itakayomsababishia kutowajibika vyema kwenye majukumu yake ya kichama mkoani. Kwahiyo sishangai hao ma Mama rc kuwa na nguvu kubwa kimaamuzi mikoani
 
Back
Top Bottom