Tunapenda mara moja tu!

Tunapenda mara moja tu!

stable woman

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
3,884
Reaction score
4,484
Habarini!!

Huu msemo sio mgeni kwako na kwangu hata mimi nilikua nikikua huku nausikia na Sasa nimeamini kuwa kupenda ni Mara moja tu

Nimekuwa kwenye mahusiano hapo nyuma lakini sijawahi kupenda, sijawahi kumlilia mwanaume kwa lolote wala sijawahi kuomba msamaha nadhani mfumo jike ulinitawala sikuwa na hisia na yeyote nilie wahi kuwa nae

Maisha yamebadilika Sasa ndipo nikagundua kuwa kwasasa nimependa kweli nimekuwa mdogo Kama piriton mwenye machozi yasiyoisha nikikosea na napenda kwa dhati haijalishi nini

Je ni kweli nawewe kwa upande wako imekutokea hii kwamba umewahi kupenda mara1 tofauti na Mara nyingine zote? Hata kwa wenye wapenzi wengi yupo mmoja ambae ndie unique unaemuhusudu??
Nipeni uzoefu

Nawasilisha
 
Wazee walisema kila shetani na mbuyu wake...sasa wewe umepata mbuyu wako... For some it happens once Wengine twice..Wengine it never happen
 
Kwa upande wangu ni kweli, yaani nampenda huyo mwanaume mpaka nahisi niyeye tu dunia nzima ndio mwanaume peke yake. Ila ............................!!!!!!!! Kupenda huku basi sawa.
 
Wazee walisema kila shetani na mbuyu wake...sasa wewe umepata mbuyu wako... For some it happens once Wengine twice..Wengine it never happen



Naomba ufafamuzi wako ama ujuzi kidogo juu ya hawa kina mama walio olewa zaidi ya mara tatu. Yaani utasikia fulani hii ni ndoa yake ya nne ama tano, yaani ana bahati kweli ya kuolewa. Sasa hawa wana mapenzi kweli kwa wanaume au inakuwa nini?
 
Inategemea ntu na ntu...
Wapo wengine daily wanapenda tena kwa kiwango kile kile.... Eg: Diva wa Klauds
 
Naomba ufafamuzi wako ama ujuzi kidogo juu ya hawa kina mama walio olewa zaidi ya mara tatu. Yaani utasikia fulani hii ni ndoa yake ya nne ama tano, yaani ana bahati kweli ya kuolewa. Sasa hawa wana mapenzi kweli kwa wanaume au inakuwa nini?

We Unaweza kuacha kazi au kufukuzwa kampuni nne tofauti...Lazima moja uliipenda zaidi au hakuna hata moja ulioipenda...unahangaika tu...ndo kama hivyo
 
Niaminivyo mimi,waweza kupenda mara nyingi,lakini maumivu makali ya mapenzi ni mara moja tu...yafuatayo baadaye ni marudio tu.
 
Naomba ufafamuzi wako ama ujuzi kidogo juu ya hawa kina mama walio olewa zaidi ya mara tatu. Yaani utasikia fulani hii ni ndoa yake ya nne ama tano, yaani ana bahati kweli ya kuolewa. Sasa hawa wana mapenzi kweli kwa wanaume au inakuwa nini?

Kwa mtazamo wangu hakuna mapenzi ya dhati ni kutimiza wajibu tu tena mara nyingi ht kwa wanaume inakuwa unamiss mambo fulani kwa mke aliepita na unalinganisha na wasasa unaona kama bd hujapata mapenzi ni mtihani mkubwa
 
Ilitokea Mara moja na haijawah kutokea na sidhan kama itatokea tna
 
Mie sijawahi penda hata mara moja, nina very short lasting infatuation na ikiisha wapigwa chini kiinterejensia. I wish ningependa hata kwa siku moja tu nione how it works in ones heart. Mie naamini nitaoa kwa ajili ya kutimiza tu wajibu na si kupendj aisee
 
inategemea unaangalia kutoka kona gani, unaweza penda tena.
 
Back
Top Bottom