DOKEZO Tunaomba Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) itukamilishie malipo yetu ya ‘refund’

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
photo_2023-10-17_14-27-16.jpg
Sisi ni Wanafunzi tuliohitimu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Campus ya Dar es Salaam tuna madai ya kutorejeshewa malipo tuliyolipa kabla ya kuingiziwa fedha za Bodi ya Mikopo (HESLB).

Ipo hivi, tukiwa Mwaka wa tatu zaidi ya Wanafunzi 1,000 tulilazimika kulipa fedha zetu binafsi kwa kuwa Bodi ya Mikopo haikuwa imetuingizia malipo yetu ya ada, hivyo chuo kikatuambia kuwa tufanye mchakato wa kulipa kisha tutarejeshewa fedha hizo pindi.

Chuo kiliahidi kuwa kitaturejeshea fedha hizo lakini imepita miezi kadhaa wamelipwa wachache.

Mara ya mwisho Walituahidi kuwa hadi kufikia Oktoba 15, 2023 itakuwa ndio mwisho wakutulipa sote, lakini taasisi imeshindwa kufanya hivyo, wamelipwa Wanafunzi zaidi ya 308 kati ya 1,266 ambao tunadai, na waliolipwa ni wale ambao malipo yao ni kiasi kidogo cha fedha.

Wanaodai zaidi shilingi laki tano HAWAJALIPWA.
d43f3703-17b9-4a99-9057-8643fc8790d3.jpeg
 
Back
Top Bottom