Tunakosea kumchukulia "serious" RC Makonda

Tunakosea kumchukulia "serious" RC Makonda

Mbona alikuwa anakwepa kwepa maswali aliyolengwa nayo?.
 
Hii ni moja ya aibu ktk taifa letu. Nakumbuka wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere matukio kama hayo tungeweza yasikia nje ya nchi yetu na tungeshangaa au kucheka,sasa upuuzi wa kina Bashite hupo ndani ya nchi yetu na mtawala aliyepo anachekelea uoza wake badala ya kuchukua hatua. Aibu ni kwetu wote. Tunaipenda Tanzania?
Akili ya kanda ya ziwa wanazijua wenyewe
 
Wale waliokuwa wakimhoji Bashite Star TV wamesomea uandishi wa habari? Au waliokotwa tu vichochoroni? Mbona hawawezi hata kudadisi au kuhoji? Ni kama kuna nguvu fulani isiyoonekana inawaogopesha vile. Wanatetemeka tu mbele ya mtoto wa mfalme. Walilazimishwa? Kwangu mimi waliotia aibu ni wale makanjanja waliokuwa wakimhoji. Naomba Paskali utupatie majina yao tuwafahamu ili siku nyingine tukitangaziwa kwamba ndio wataendesha mahojiano tuendelee na shughuli zetu badala ya kukaa saa tatu nzima tusikiliza hotuba ya mhojiwa badala ya majibu ya hojaji. Ovyo kabisa hawa makanjanja.
 
Tena nikuambie mkuu wale madogo wamejitahidi sana hasa Nyanda.ujio wa Makonda ulipangwa na kuratibiwa na bosi wao Diallo.Kama ulimsikia Makonda akiwaambia kile ni kipindi chake,hata baadae TV ilivyokuwa off record kule redioni Makonda akaropoka kumkomesha Ruge.Kwa hivyo watangazaji ni bangusiro tu!

Cha msingi Makonda ni mwajiriwa wako na mimi,kama hatumtaki basi ni sisi kuchukua hatua ya kumng'oa kwa lazima hata kwa maandamano.tuache lawama
 
CCM bwana! Yaani kampeni zote za 2015 wimbo ulikuwa kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Sisi tukajua kwamba ni viwanda kweli tuvijuavyo na tunavyovisoma kwenye historia na kuviona kwenye nchi nyingine. Kumbe wenzetu CCM kwao viwanda ni kuwa na vyerahani vinne! Ooh! God save us from this vampire, namely CCM.
 
Kumkana mama ndio swala si baba. Kama mama alichanganya madawa anajua mwenyewe. Mara ngapi tumeshuhudia humu mitaani kwetu watu wanalea watoto wa watu wengine? Hata pamoja na igizo la Siri za Familia kufundisha bado kuna watu hawaelewi tu? Mtoto kajua baba yake ni nani kaamua kuungana na ukoo wake tatizo liko wapi?
Ukisha jua kuna mkoroganyo huo hupaswi kuingia ndani sana. Kihistoria kabla ya kuzaliwa Makonda mama yake alikosana na baadhi ya ndugu wa mwanaume kwa kuwa hazai. Baada ya miaka kadhaa alizaliwa Makonda. Katika mtanziko huu lolote laweza kutokea lenye kudhihirisha hili. Siri za familia ni kuacha kuzichimbua kuibua migogoro isiyo sababu.
 
Back
Top Bottom