Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,058
- 134,393
- Thread starter
- #221
Wewe umeona hilo tu?!Kumkana mama ndio swala si baba. Kama mama alichanganya madawa anajua mwenyewe. Mara ngapi tumeshuhudia humu mitaani kwetu watu wanalea watoto wa watu wengine? Hata pamoja na igizo la Siri za Familia kufundisha bado kuna watu hawaelewi tu? Mtoto kajua baba yake ni nani kaamua kuungana na ukoo wake tatizo liko wapi?
Ukisha jua kuna mkoroganyo huo hupaswi kuingia ndani sana. Kihistoria kabla ya kuzaliwa Makonda mama yake alikosana na baadhi ya ndugu wa mwanaume kwa kuwa hazai. Baada ya miaka kadhaa alizaliwa Makonda. Katika mtanziko huu lolote laweza kutokea lenye kudhihirisha hili. Siri za familia ni kuacha kuzichimbua kuibua migogoro isiyo sababu.