ipogolo
JF-Expert Member
- Aug 15, 2011
- 6,275
- 5,962
Wadau,
Baada ya CCM kushindwa na nguvu ya mageuzi ya kudai uwepo wa KATIBA MPYA ya wananchi(tofauti na ile ya 1977 ambayo ilitengenezwa na wachache kwa niaba ya Watanzania) hatimaye mchakato wa kupata KATIBA mpya ukaanza.
Baada ya patashika nguo kuchanika hatimaye rasimu zikaanza kutengenezwa na mabaraza kupatikana. Mwisho wa yote wajumbe wakapatikana(kundi la 201 na wale wabunge wa bunge la JMT na BWZ).
Bunge Maalumu la Katiba likazinduliwa na Mh rais wa JMT na tukayasikia tuliyoyasikia na mijadala mizito yenye mashiko ikaanza Ndani ya Bunge na NJE ya Bunge.
suala la Muundo wa serikali likabeba kwa kiasi kikubwa hisia za watanzania wengi.Ikatokea hata wajuzi wa mambo kuhoji uhalali wa muungano ulioisshi miaka Hamsini.
Baada ya mvutano mkubwa yakatokea makundi mawili UKAWA na "INTARAHAMWE". Kundi la UKAWA likaona lina buruzwa na kuja kwa wananchi kutoa kilio chao na hao wengine wakabaki na kuendelea na vikao.
Katika vikao vya UKAWA hoja ya ujio wa TANGANYIKA ukaonekana kushika kasi.
Mie mleta hoja nawauliza wanabodi:
1: Tanganyika ikirudi je na chama chetu cha TANU ambacho kiliipigania Tanganyika huru na chenyewe KITARUDI?
2: Kama hakitarudi je, misingi yake itabebwa na chama gani kati ya hivi vilivyopo;CCM,CHADEMA, CUF,UMD,NCCR,ACT
TLP nk?
3: Kama kitarudi kipo tayari kuongoza nchi nje ya malengo na itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea?
Naomba kufungua mjadala.
cc Mchambuzi Nguruvi3, Tumaini Makene, Ritz, Mwigulu Nchemba MSALANI, @Dr Kitila Mkumbo, kababu