Masatu, tabia hiyo hata mimi sipendi lakini kupachika viongozi majina ya utani au kebehi as long as siyo ya matusi ni sehemu moja ya gharama ya kuwa kiongozi. Mwalimu alijua hilo.. na kuna wakati alikiri kwa kusema "Mara ya Kwanza waliniita Musa, Halafu wakaniita Mchonga, siku hizi wananiita Haambiliki"... Hivyo majina kama "Muungwana" au "Msanii" n.k ni sehemu ya gharama ambayo viongozi wanalipa.
That said, binafsi situmii majina yoyote zaidi ya majina yao na siungi mkono kuwatungia majina ya matusi kwani that is counterproductive na kama tunataka kuwa mahali pa kuchukuliwa kwa umakini basi kuna vitu kila mmoja kwa makusudi kuviachialia. Uzuri mmoja wa JF ni kuwa standard yetu ya ushiriki siyo sawa na TV au magazeti.
Kwa upande wangu kwenye eneo langu la "Comments" kule KLH News.. naruhusu ukosoaji wa aina yoyote wa viongozi bila kutumia matusi na hata kama mtu ana point nzuri kiasi gani akianza kutumia matusi ninafuta posting hizo!