Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,026
- 12,338
Awali ya yote wacha niweke wazi kuwa mimi sio muumini wa Presidential system ila ni mfuasi mkubwa wa Parliamentary system.
Kwa kweli kwa namna yoyote ile kama taifa tulikosea pakubwa wakati Nyerere anakabidhiwa nchi kwa kuhamisha mfumo wa Taifa kutoka mamlaka kwa bunge kwenda mamlaka yote kuhodhiwa na taasisi ya Urais.
Hilo kwangu lilikuwa kosa kubwa, kwa hakika kwa sasa kama taifa tunaumizwa na huu mfumo wa Presidential system ambao rais kwa kiasi kikubwa ndie muamuzi wa kila kitu hapa nchini bunge ni jumba la makumbusho tu halina maana wala nguvu yoyote kiasi hicho dhidi ya Rais.
Huu mfumo wa Presidential system kwa kiasi kikubwa hapa nchini unaondoa uwajibikaji unaohitaji kwa Rais ni kwa namna gani mtaweza kumfuta Rais na kuchagua mwingine kwa kipindi kifupi kutokana na upuuzi wowote atakao fanya( hapana hii itakuwa ngumu sana).
Ila Parliamentary system kwa kiasi kikubwa unaongeza uwajibikaji kwa mawaziri na waziri mkuu muda wowote anaweza wajibishwa kwa namna yoyote na kuchaguliwa mwengine atakaye sogeza gurudumu la taifa mbele bila shida yoyote.
Kwenye Parliamentary democracy waziri mkuu hawezi kusema nimeamua kukaa kimya katika ajenda kubwa inayo endelea kulitikisa taifa lazima alazimishwe na bunge mara moja atoe maelekezo akishindwa moja kwa moja anawajibishwa na bunge.
TURUDI PARLIAMENTARY DEMOCRACY TULIO ACHIWA NA MKOLONI NA KUACHANA NA HUU UPUUZI WA PRESIDENTIAL DEMOCRACY MARA MOJA