Tunahitaji akili ya kisasa Ili kuendesha nchi kisasa.

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kuna msemo wa kiingereza usemao " familiarity breeds contempt". Ukiwa na maana mazoea huleta dharau.

Ninasikitishwa sana na watu tunaowaamini na tuliowaweka mbele kama as a drive katika uendeshaji wa nchi.

Hivi Leo ukienda serikalini, mahakama na hata bungeni, hivi kweli waliopewa dhamana ya uongozi kwa ngazi yoyote Wana clue ya kile kinachoendelea katika ulimwengu wa Leo? Je Wana ufahamu wa kileo?

Wabunge wetu, mawaziri, wenyeviti wa vyama vya siasa, wachungaji, masheikh, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, majaji, nk. Je tunawaona kweli Wana ufahamu wa mambo unaotakiwa muda huu au ni kufanya kazi kwa mazoea tu kwa kuwa wameshatuzoea?

Nataka kushawishika kwa hakika kabisa kwamba hatuendelei haraka kwa sababu pia wale tuliowaweka mbele ( role models) katika aspects nyingi za maisha yetu siyo watu wa wakati huu. Wana uzamani katika fikra zao na wanafanya mambo tu kwa mazoea. No wonder wanatudharau!

It is very hard to teach an old dog, new tricks. Naiona nchi yetu inakwamia hapa.

Tunategemea mabadiliko na mindset itakayotuvusha kama nchi, lakini kwa mgongo wa watu ambao ni wa kale, Wana mawazo ya kale, akili za zamani na hawajui kabisa juu ya mambo ya Leo ( current affairs).

Tunategemea watu ambao hawajui , siasa za kisasa zinafanywaje, hukumu za mahakama zitakazodumisha umoja, amani na mshikamano zinatakiwa ziweje? Hukumu zitazofanya viongozi wawajibike zinatakiwe ziweje nk.

Ebu nambie, hukumu ya mahakama, inayopendekeza wakurugenzi waendelee kuwa wasimamizi wa uchaguzi, wakati huyu jaji anaelewa fika kwamba wakurugenzi ni presidential appointment ambaye pia huyo ni mgombea , Wana ufahamu wa kisasa kweli? Wanajua thamani ya amani kweli? Hivi Hawa wanamsaidiaje huyu Rais kuwa a law abiding citizen kwa hukumu ambayo hata yeye mwenyewe anacheka akiisikia?

Nambie wabunge wanaoenda kujadili mabadiliko ya sheria za uchaguzi zinazopendekezwa na tume huru ya uchaguzi.

Hivi kweli wanauelewa wa kisasa na kujua nchi zinazoendelea zinaendeshwaje? Au tu wanaenda kulinda status quo na kudumisha fikra za vyama kama siyo chama chao.

Hivi Hawa wabunge ni currently knowledgeable kiasi Cha kurekebisha mambo yaliyopendekezwa na vyama vyao ambayo sio akili kwa maana ya tangibility wakati wao wenyewe wanachojua tu ni kidumu chama chetu?

Hata bila kudharau mtu ( maana Sina hiyo hulka). Watu likes za kina wassira, ambaye CCM wanamuona kama think tank wao ana input ya uelewa wa kileo unaoweza kusaidia nchi kuishi kisasa au atakuwa anaongelea status quo?

Wazee wetu ambao kwa heshima kabisa, walifanya mambo makubwa wakati wao, tuwachuje Sasa. Siyo wote bado Wana akili ya kisasa itayoifanya nchi iende kisasa.

Hivi vijana kwa mfano wa chama Cha mapinduzi, waliolewa madaraka na kuzoea umaarufu rahisi ( cheap popularity) unawategemea watakuwa na akili mpya ya kisasa itayotaka kuwe na tume huru ya uchaguzi ambayo inasimamia haki kwa Kila mtanzania na kwamba Kila mtanzania ana haki ya kuongoza na siyo CCM pekee? Thubutu!

Nasubiri bunge kwa hamu niwasikie likes za akina Joseph msukuma, Lusinde, Job Ndugai, yule mama wa musoma,cjui Agness Marwa or what kama utawasikia wanaongea mawazo profound ya kuwa na tume. Naiona bunge limejaa akili ya zamani ambayo inajua uccm tu na madaraka basi. Habari ya ustaarabu, kutoa haki kwa wote, na nchi kuwa na amani endelevu na siasa hayo ni yenu wao hawayajui. ( Akili ya kale).

Nimalizie kwa kumpongeza Rais kwa attempt ya kutaka kuongoza nchi kileo na kisasa. Namuona mama mwenye akili ya kileo na anayejua nchi za kisasa zinaendeshwaje. But tell me, amekutana na Nini? Watu wa akili ya kale, wanaojua nchi ni CCM kushinda viti vyote vya uenyekiti wa serikali za mitaa, viti vyote vya udiwani, viti vya ubunge na urais Tena kwa gharama yoyote.

Amekutana na akili ya zamani, watu ambao hawana exposure na kujua kuongoza kistaarabu, watu ambao wanajua madaraka utadhani walizaliwa nayo. Amekutana na watu ambao hawana hata aibu kwenye mishipa yao ya damu kudhulumu wenzao. Watu hao kweli watayakubali mapendezo initially alivyokuwa Rais?

Kwa kuwa tayari hao tunaowatanguliza mbele wameshatuzoea, wanaongoza kwa mazoea, reasoning yao ni ya kimazoea, na Wana akili ya kizamani na mazoea, tutegemee dharau na siyo maendeleo au mabadiliko tunayoyataka .

Familiarity breeds contempt.
 
Back
Top Bottom