Tunahitaji elimu ya aina gani kwa karne hii tuliyopo?

Feb 18, 2017
63
62
Ni kwa muda mrefu sasa tumekuwa katika aina na mfumo ule ule wa elimu na mrejesho katika matokeo yake umekuwa mdogo sana.je tunahitaji kubadili nini na tunahitaji aina gani ya mifumo ya elimu itakayotuletea mabadiliko ya kweli? Tupo katika karne nyingine kabisa na kizazi tofauti kabisa, je elimu na mifumo yetu ya elimu inakidhi?
 
Elimu ipi unamaanisha elimu ya malezi, elimu ya ndoa, elimu ya fedha, elimu ya uzazi, elimu ya maisha ama:
 
Elimu nzuri ni ile itakayofanya RAIA waanze kudadisi jui ya mambo yanayowazunguka ya kijamii,kiuchumi na zaidi kitekinolojia.Ili waweze kuanzisha gunduzi mbalimbali zikazosaidia katika kuzalisha na kutengeneza vitu.

Ukoloni imeua vipaji vya watu wetu na mbaya zaidi viongozi wetu waliendeleza model za kikoloni kwenye nyanja nyingi-kitu ambacho kinatuumiza hadi leo.

Huwezi ukawa mbunifu kwa kuwaza na kutumia lugha ya mwenzio-hili ndio jambo linalokwamisha sana maendeleo ya Africa (cultural).

Angalia tuna engineer s wengi but kuanzia Barbara zetu,machine mbalimbali,dawa za binadamu na mifugo na chanjo,bidhaa mbalimbali zote tunaagiza hatutengenezi.why?
 
Back
Top Bottom