Tunaelekea msimu wa baridi; homa za mafua na kikohozi ni Jambo linalotarajiwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,403
52,034
Kwema Wakuu!

Poleni na Misiba na Kwa wale wanaofurahia niwape pongezi. Ndio Maisha hayo. Sio lazima Msiba wako uwe Msiba WA Watu wote, wengine kwao inaweza kuwa ni sherehe.

Msimu tunaoelekea ni msimu wa baridi, masika ndio imemalizika hivyoo! Kikawaida baridi ni mwezi wa sita na wasaba lakini kuna Wakati inaanzia mwezi wa tano na kuna Wakati inachelewa kuisha mpaka mwezi wa nane.

Wakazi wa maeneo ya joto hasa Pwani kama vile Lindi, Mtwara, DSM, Tanga, Pwani, Zanzibar ni rahisi kukabiliwa na homa ya mafua na kikohozi Kutokana na kuwa hawaioni baridi hasa majira ya Usiku lakini kimsingi Ipo.
Ni vizuri Wakati wa kulala Usiku mtu avae angalau nguo yoyote ya kuzuia kifua au afunike shuka.
Hii itumike zaidi Kwa wale wenye shida ya mfumo wa kupumua au wenye allergy ya baridi.

Wasalamu
 
Back
Top Bottom