Tunachukulia tahadhari kauli ya mawakala wa CCM kuhusu; Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu Dkt. Slaa

mohamed mtoi nimesoma naye a evel ni mtu mpenda mafanikio. mie kama white nampongeza kwa kijituma na muelekeo wake wakuwa high profile leader wthn cdm.
 
Mimi hushindwa kabisa kuelewa sisi wadanganyika tuna tatizo gani. Mleta mada kasema tena kwa tahadhari juu ya viongozi wa chama kuwa ktk hali ya hatari na mhusika ametajwa. Japo mtu huyu sii wa kuaminika lakini inabidi mtu huyu ahojiwe zaidi na pengine hata kumuomba mkutane naye ili apawe ukweli ambao mtaufanyia uchunguzi badala yake ni matusi na vijembe dhidi ya mjumbe.

Mohamed Mtoi mtu safi lakini kwa nini iwe yeye tu kati ya viongozi na wanachama wote? Kuna kipi special ambacho mwandishi amekitumia dhidi yake. Kama huyu mleta mada ni mzushi na muongo inatakiwa kwanza kufanya uchunguzi na ikafahamika anatumiwa na kina nani halafu ndio habari nzima mnaishusha. Kushambuliana hakuna tija hata kidogo maana hata ya Zitto yalianza hivi hivi na leo sisi wengine yametufika kooni.
Mzee mzima , naona na wewe unataka kuingia kwenye mchezo wa Mbugi ! !!!!! Hii waache watoto wajifurahishe ....eti kwaniniMtoi unataka kuaminishwa kuwa alichoandika huyu salia wa ACT ni ukweli au ?
 
Mkandara.
Swali lako kwenye maandishi ya kijani kikavu.
Sijui dhamira ya Ludovick ni nini lakini kwa mtu unayufuatilia kidogo unaweza kuhisi kwa nini akawa ni Mtoi badala ya wengine. Naweza sema yafuatayo.
mohamed Mtoi ni mwanachama na mtumishi wa Chadema mwaminifu, ni msambaa wa Tanga,ni muumini wa imani ya Kiislamu.
Kama unakumbuka ungegundua kwenye UDINI,UKABILA na Umkoa/UKANDA ndio CCM na wengine wamekua wakitumia kama agenda yao dhidi ya CHADEMA.
Ni rahisi kujenga dhana potofu juu ya Mtoi kwa kutumia dini yake na kabila lake zaidi ya mwingine.
Mkandara , kama unakumbuka Ludovick alikuja na uzi kujaribu kuzima uzi ulokua umeandikwa hapa kua alikua akihusishwa na kukamatwa kwa vijana wa Lwakatare, yeye akaja kusema oh mara palikua na uizi wa magari Arusha mara bar-maid etc etc habari ambazo hazina vidole wala kucha ili mradi ajaribu kubadili au kujitetea akijinaga kuwa yeye ni CHADEMA mwaminifu, wakati huo huo anapata ajali na magari ya ACT ???

Huo ni Mtazamo wangu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Last edited by a moderator:
Mzee mzima , naona na wewe unataka kuingia kwenye mchezo wa Mbugi ! !!!!! Hii waache watoto wajifurahishe ....eti kwaniniMtoi unataka kuaminishwa kuwa alichoandika huyu salia wa ACT ni ukweli au ?
Ahahha! hapana mkuu niko concerned tu na jinsi watu wanvyoshambuliana badala ya kujadili. Mjamaa awe ACT,CDM au CCM inapofikia swala la usalama wa mtu haijalishi nani kasema. Kwa maandishi yake, Mohamed anaweza mshtaki huyu jamaa na pia sii swala la kudharau. JF sii uwanja wa mipasho..
 
Ndugu,
Jana ulitoa comment kwenye hiyo thread, leo umeamua kuandika thread kama counter argument.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anayeangalia masuala ya kisiasa kwa kutumia mboni za 3D atagundua kuna ukweli ndani ya thread na kwa maana hiyo, ndiyo maana inakusumbua kisaikologia mpaka unatumia nguvu nyingi kutaka kuifunika kihoja.

Inajulikana upuuzi hupuuzwa, lakini unaodaiwa ni upuuzi wakati inatumika nguvu kubwa kupambana nao, lazima utakuwa siyo upuuzi tena.

Tatizo la CHADEMA ni kusimama katika msingi wa kilaghai. Kwa sasa mnajaribu kupambana na ulaghai wenu.

Haya ndiyo mavuno ya sera za
kilaghai na usaliti.

Kwa sasa mnakimbia vivuli vyenu

Unamwongelea huyu Ludovick aliyecheza Filamu fake ya ugaidi na Mwigulu? Kwa hiyo wanataka kucheza part 2 yake? Anyway tunaisubiri kwa hamu.
 
Ahahha! hapana mkuu niko concerned tu na jinsi watu wanvyoshambuliana badala ya kujadili...

Kwa nini Mtoi? ni ili propaganda ya udini ikolezwe na ccm sababu ya dini ya mhusika aliyechaguliwa na 'idara' anayoisema Ludovick

Athari: baada ya kumdhuru Mbowe au Dr Slaa uchaguzi usimamishwe maharamia wajipange

iwaathiri UKAWA na kuwatoa pamoja na wananchi kwenye Katiba Mpya

ionekane ndani ya Chadema Bado Kuna kusalitiana na kutoamini kutokee ili kuvunja mshikamano
 
"Ihakikishe Mtoi hakutani na dokta Slaa na Mbowe akiwa pekee yake"
maandiko hayo kwenye funga semi ndio yamebeba zima nzima ya Ludo na watu wake,hapa kuna mambo 2 yanaweza kuwa sawa ama si sawa,Mosi,inawezekana Mtoi anataarifa zao nyeti ambazo pengine wasingependa ziwafikie viongozi hao wakuu wa CDM hivyo wakaona umuhimu wa kumbana Mtoi na kuzuia kila fursa ya Mtoi kubaki pekee na watajwa,ama kuna jambo baya limeandaliwa juu ya watu hao 3,Dr Slaa,Mbowe na Mtoi,hivyo Ludo amejitokeza kujaribu kuset ajenda na kuwaandaa watu kisaikolojia,bt any way kila mlio wa risasi vitani una maana yake,chama kiendelee kuwa makini,imara na timamu zaidi,
 
Ni mimi niliye post ushauri ule. tatizo la siasa zetu ni kupenda uongo na upotoshaji. hizo tafsiri za makene bila shaka zina lengo la kupiga siasa. lakini angalau kwa sasa anakiri ni muhimu kufuatilia yaliyosemwa kwenye ushauri.
haya mengine cheza siasa tu.

Absalom Kibanda anasema mtu aliyemvamia na kumjeruhi anafanana na wewe na wewe ndo mtu wa kwanza kutoa taarifa kuwa Absalom Kinda amevamiwa. Tunaomba ufafanuzi wako mkuu
 
Ni mimi niliye post ushauri ule. tatizo la siasa zetu ni kupenda uongo na upotoshaji. hizo tafsiri za makene bila shaka zina lengo la kupiga siasa. lakini angalau kwa sasa anakiri ni muhimu kufuatilia yaliyosemwa kwenye ushauri.
haya mengine cheza siasa tu.

Cha muhimu tueleze ilikuwaje ukamteka Kibanda? na ni nani alikutuma?na hadi hivi sasa umenufaika vipi na tukio lile?
 
Ndugu,
Jana ulitoa comment kwenye hiyo thread, leo umeamua kuandika thread kama counter argument.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anayeangalia masuala ya kisiasa kwa kutumia mboni za 3D atagundua kuna ukweli ndani ya thread na kwa maana hiyo, ndiyo maana inakusumbua kisaikologia mpaka unatumia nguvu nyingi kutaka kuifunika kihoja.

Inajulikana upuuzi hupuuzwa, lakini unaodaiwa ni upuuzi wakati inatumika nguvu kubwa kupambana nao, lazima utakuwa siyo upuuzi tena.

Tatizo la CHADEMA ni kusimama katika msingi wa kilaghai. Kwa sasa mnajaribu kupambana na ulaghai wenu.

Haya ndiyo mavuno ya sera za
kilaghai na usaliti.

Kwa sasa mnakimbia vivuli vyenu

Hiyo mnayoita misingi ya kilaghai, CCM wanaitumia kimya kimya kuendesha nchi, japo si kwa muono wa waasisi wa misingi hiyo... Mwaka 2010 wakati wa kampeni, dk. Slaa alisema angeanzisha mchakato wa katiba mpya, mkapiga vijembe kuwa haiwezi kuwa, nchi hii haihitaji katiba mpya... Mwaka haukwisha, mwenyekiti wenu akatangaza kuanzisha mchakato wa katiba mpya... Ulaghai wa Chadema huo!

Lingine ilikuwa kuhusu elimu. Mwaka huo huo 2010, wakati wa kampeni, dk. Slaa tena alisema Chadema ikiingia serikalini, itatoa elimu bure toka msingi hadi sekondari! Unakumbuka mlesemaje?! Chadema ni waongo, suala la elimu bure haliwezekani. Leo Rais Kikwete kasemaje Morogoro kama masikio yako hayana matege? Serikali inaangalia uwezekano wa kutoa elimu bure toka msingi hadi sekondari... Ulaghai mwingine wa Chadema.

Hakika ni bora ulaghai wa Chadema kuliko ukweli wa CCM!
 
Mkuu Tumaini Makeni, hii ni jana
CHADEMA au viongozi wake, hawapangiwi wala kupokea ushauri wa namna ya kusimamia, kuendesha chama au utendaji kazi wa kila siku kutoka kwa CCM na washirika wao (its cronies as I normally write).
Baada ya hii nilisema hivi
Mkuu Tumaini Makene, asante kwa taarifa hii kuhusu Chadema na viongozi wake katika suala zima la kupokea ushauri, ushauri siku zote huwa ni ushauri tuu, mshauriwa ana hiyari aupokee au kuupuuza.

Kwa vile sote tuko humu jf, sisi wengine hatuna vyama, mazuri tutapongeza, madudu tutakemea, na kwenye ushauri tutatao, its up to Chadema to take it or leave it, ila kuna sisi wengine hatupendagi makelele ya watu kuja kutulilia humu kila baada ya miaka mitano!, ndio maana sisi wengine tunashauri, na tukiisha puuzwa, wakati wa kuleta vilio humu vya November, 2015, sio tuu tutawakumbusha tuliwashauri nini, bali badala ya kuwapa pole kwa vilio, tutawazomea tukiamini hayo ndio mliyoyataka!.

Asante.

Pasco.

Kama haitoshi nikaongezea hivi
Mkuu Kilaza, asante tena, kama in reality shetani amewahi kumshauri Mungu, what is Chadema kukataa ushauri wa shetani as if ni chama malaika!.

Ila pia shetani mara nyingi sana anapenda kujidisguise kama Mungu au malaika, ili kuwachota kwa urahisi, hivyo anayewajua zaidi mashetani ni shetani mwenyewe!, mnaweza kuwa na malaika ndani yenu mkijijua kuwa ni malaika!, kumbe ni shetani!, sasa shetani anapowatahadharisha na malaika wenu kuwa ni shetani, issue sio kumpuuza, bali kumchunguza huyo malaika wenu kama kweli ni malaika au ni shetani!.

Asante,

Pasco.

Ni jana tuu, umepuuza, lakini leo Mkuu Tumaini umekuja ki hivi

Kuna upuuzi wa kupuuzwa na mwingine unastahili kupuuzwa kwa tahadhari. Jana katika thread moja hapa; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/712800-chadema-imchunguze-mohamed-mtoi.html, yameandikwa maneno mengi ya kipuuzi ambayo yanaweza kupuuzwa, lakini bandiko hilo ukilisoma katikati ya mistari linaonekana kuzungumzia ujumbe usiopuuzwa.

Bila kulazimika kurudia maneno yote, haya yanaweza kuwasilisha concept inayopatikana katika ujumbe wote "Nashauri haraka na lazima,idara yetu ya ulinzi na usalama,na inteligensia, ihakikishe Mtoi hakutani na dokta Slaa na Mbowe akiwa peke yake.
Makene

Asante kwa hili, kupuuza kwa tahadhari, na kuichukulia tahadhari ushauri huo, ndiko kuzingatia kwenyewe, ina maana ushauri umepokelewa!.

Even the devil, sometimes does good deeds, msipuuze tena ushauri wowote!.

Asante

Pasco
 
Bila kumsahau kanjanja aliyekatika mishipa yote ya aibu anayejiita Pasco . Huyu jamaa tumbo lake linapelekesha akili yake....
Mkuu Macho Mdiliko, kwanza asante kunisemea ukweli wangu, ila sio kweli kuwa tumbo langu linapelekesha akili zangu, bali akili zangu zote nimezihamishia tumboni, kichwa ni empty case totally!.

Asante.

Pasco.
 
Makene ni mmoja wa maafisa habari wasio makini na wakurupukaji ambao wamepata kutokea kwenye vyama vya siasa!

Kama kichwa chako kingekuwa kinatumika sawasawa haya yote ulipaswa kuyaandika kwenye uzi wa Ludo.

Ulikurupuka kuropoka kabla ya kifikiri na mtu aliyekusoma hapa atashangaa maana ulionekana kupuuza ulichoshauriwa....! Salsa hivi unakurupuka tena na kusema unachukua tahadhari.....

Wewe ni afisa habari wa hovyo kabisa unazidiwa hata na Yericko Nyerere...
 
Last edited by a moderator:
Ni mimi niliye post ushauri ule. tatizo la siasa zetu ni kupenda uongo na upotoshaji. hizo tafsiri za makene bila shaka zina lengo la kupiga siasa. lakini angalau kwa sasa anakiri ni muhimu kufuatilia yaliyosemwa kwenye ushauri.
haya mengine cheza siasa tu.

Mkuu,
Joseph Ludovick Rwezaura, iwapo ni wewe uliye post huo ushauri bila shaka unatatizo kubwa zaidi ya lile tunalolifahamu.
Kwa maelezo yako unathibitisha kuwa wewe ni Member wa hiyo idara yenu ya Usalama, sasa kwani usiwafahamishe hao wakuu wenu katika hiyo idara kwa kutumia njia zenu mnazo tumia kila siku kupeana taarifa badala ya kuja hapa JF?
 
stupidity kabisa hii kushughulika na Ludovick alie ingia kwenye kundi la wasaliti sasa anaitaje kurugenzi yetu? muacheni aendelee kuharisha
 
stupidity kabisa hii kushughulika na Ludovick alie ingia kwenye kundi la wasaliti sasa anaitaje kurugenzi yetu? muacheni aendelee kuharisha

Huyu Ludovick si ndiye yule aliyepata ajali Morogoro akiwa na ACT na akatuma uzi wa kashfa humu? Amerudi lini Chadema mpaka kufikia kuishauri?
Huyu jamaa ana akili za kuku. Anasahau kirahisi sana!
 
Mkandara.
Swali lako kwenye maandishi ya kijani kikavu.
Sijui dhamira ya Ludovick ni nini lakini kwa mtu unayufuatilia kidogo unaweza kuhisi kwa nini akawa ni Mtoi badala ya wengine. Naweza sema yafuatayo.
mohamed Mtoi ni mwanachama na mtumishi wa Chadema mwaminifu, ni msambaa wa Tanga,ni muumini wa imani ya Kiislamu.
Kama unakumbuka ungegundua kwenye UDINI,UKABILA na Umkoa/UKANDA ndio CCM na wengine wamekua wakitumia kama agenda yao dhidi ya CHADEMA.
Ni rahisi kujenga dhana potofu juu ya Mtoi kwa kutumia dini yake na kabila lake zaidi ya mwingine.
Mkandara , kama unakumbuka Ludovick alikuja na uzi kujaribu kuzima uzi ulokua umeandikwa hapa kua alikua akihusishwa na kukamatwa kwa vijana wa Lwakatare, yeye akaja kusema oh mara palikua na uizi wa magari Arusha mara bar-maid etc etc habari ambazo hazina vidole wala kucha ili mradi ajaribu kubadili au kujitetea akijinaga kuwa yeye ni CHADEMA mwaminifu, wakati huo huo anapata ajali na magari ya ACT ???

Huo ni Mtazamo wangu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Hembu niambie wewe kupata ajali ktk gari la chama kisichokuwa chako kunahalalisha uanachama wako ndani ya hicho chama?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom