Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Mkuu utanisamehe kama nimekosea
Hapo kwenye survey ya Maji natofautiana na utaratibu wenu ..... surveyor anatakiwa awe ni kampuni au MTU ambaye ni independent kabisa ambaye hafungamani wala hana maslahi na kampuni ya uchimbaji wa Maji.... mara nyingi wachimbaji Wa mMaji hushirikiana na surveyors ku- exaggerate ukubwa Wa kazi ..... surveyor anaweza skuta Maji ni let say 70 meters lakini kwa vile anafahamiana na wachimbaji na report itapikwa na kuandikwa 95 meters .... hapo umeliwa 25 meters

mashauri mteja atafute surveyor wake mwenyewe na siyo kuletewa na mchimbaji Wa maji
Tungekuwa tunataka kumpiga mteja ningesema hapa kuwa kazi zote tunafanya sisi lakini nimekuwa mkweli kuwa sisi ni driller tu, na tumejalibu kuwa partner na surveyor mmoja ili kuepuka down time ,maana unaweza kukuta wanakazi nyingi halafu mteja anahalaka sasa kwa sisi lazima afanye kazi yetu ndo aendelee na zingine kwa sababu tunamkataba nae, ila kama mteja anasurveyor wake pia ni sawa. mwisho wa siku si tunataka tufanye kazi kwa haraka zaidi.
 
Vipi je nikitaka mpime kwanza kama kuna maji chini kabla ya kuchimba???
Inawezekana yupo surveyor unaweza kupima kisha ukaja kuchimba hata mwakani na si lazima tuchimbe sisi ukishapata report yako unaweza kutafuta wachimbaji utakaovutiwa nao.
 
Inawezekana yupo surveyor unaweza kupima kisha ukaja kuchimba hata mwakani na si lazima tuchimbe sisi ukishapata report yako unaweza kutafuta wachimbaji utakaovutiwa nao.

Leo nilikupigia sim, kesho pita uangalie eneo hilo
 
Tunachimba mita zote mwisho mita 150 kulingana na mashine zetu, mita 60 ni tshs 3600000(3.6M)

Kwa uzoefu wenu kwa hapa Dar maji baridi(yasiyo na nchi naweza kuyapata kuanzia mita ngapi,na je mnatumia vipimo kujua kama sehemu husika hasa kwa hapa Dar kama ina maji yasiyo na chumvi au la ,na gharama zake zikoje,je hizo gharama ni kila kitu mimi kazi yangu itakuwa kufungua tu bomba?na mwisho je solar pump kwa ajili ya kusukuma majinazo mnakuwa nazo na kama mnazo mnauza kiasi gani?
 
Upatikanaji wa maji upo mita tofauti tofauti kulingana na sehemu mfano baashi ya sehemu unaweza kupata maji mita 50 na sehemu nyingine mpaka mita 150 ndani ya dar hii, sasa ili kujua maji yalipo ndo unashauriwa kufanya kwanza survey ambayo itatoa report yalipo maji, kuhusu maji chumvi au baridi ni matokeo tu muda mwingine ni bahati, report inaweza kusema maji mazuri lakini ukapata ya chumvi
Solar depends na hp ya pump utakayofungiwa ila kwa experiance pump ya 1 hp inaweza kukugharimu 6 million kwa solar tu na 2hp inaenda hadi 10 million,
Bei za kuchimba kisima ni 60 elfu kwa mita hii inahusisha kila kitu hadi pump na bei ya survey ni laki 2.
 
Mkuu kifupi nimekuelewa sana, tena sana na nikiwa vizuri nitakutafuteni, utata uko kwenye maji chumvi na huu upimaji (survey)!

Kwa uzoefu wako ni mara ngapi inatokea survey inasema maji siyo chumvi hafu inakuja kuwa ni chumvi? Na je makosa haya ni kwa kila surveyor au accuracy inatofautiana kati ya surveyor na surveyor?

Maana ni vizuri nitoe hela nyingi kwenye survey nipate report ambayo iko sahihi, kuliko kuja kuingia gharama za kuchimba huku mnafuatisha report mbovu.
 
Imeshindikana kuupload labda video formart haipo compartible na web,

Upload kwenye youtube, kisha copy link, kwenye jf sehemu ya kureply bonyeza insert video, paste hiyo link, bonyeza OK
 
Mkuu kifupi nimekuelewa sana, tena sana na nikiwa vizuri nitakutafuteni, utata uko kwenye maji chumvi na huu upimaji (survey)!

Kwa uzoefu wako ni mara ngapi inatokea survey inasema maji siyo chumvi hafu inakuja kuwa ni chumvi? Na je makosa haya ni kwa kila surveyor au accuracy inatofautiana kati ya surveyor na surveyor?

Maana ni vizuri nitoe hela nyingi kwenye survey nipate report ambayo iko sahihi, kuliko kuja kuingia gharama za kuchimba huku mnafuatisha report mbovu.
Hawa wapimaji wanakua sahihi mara kwa mara ni mara chache nimeona matokeo tofauti na report yao, na kuna baadhi ya maeneo ambayo chumvi haikwepeki tushamchimbia mtu akapata chumvi akamwita tena surveyor akachimba kingine akapata tena chumvi ndani ya kiwanja kimoja,
 
Mkuu evigt Dsm nyumba nyingi walizochimba visima ambazo nazifahamu mimi maji yake ni ya chumvi, Je, kunauwezekano wa kupata maji yasiyonachumvi ukichimba kisima Dar es Salaam ?. Na kwa uzoefu wako eneo la Makongo Juu karibu na Mto Mbezi ili upate hayo maji inabidi uchimbe mita ngapi ?
 
Kupata maji yasio na chumvi inawezekana, ila siwezi kujicommit nikakwambia ni lazima kupata. Kwa makongo juu maji yapo mita 120.
 
Kupata maji yasio na chumvi inawezekana, ila siwezi kujicommit nikakwambia ni lazima kupata. Kwa makongo juu maji yapo mita 120.

Okay shukran bei ya mita 120 inakuwa ngapi vile ?
 
7.5 million . Kuchimba na pump installation, kifupi kila kitu juu yetu.

sio kweli,,...ni 7.2m.

anyway kuhusu maji kuwa na chumvi waambie wananchi kuwa maji yote duniani yanatakiwa kuwa na chumvi ila chumvi isizidi uwezo wa mwanadamu kuyatumia kwa kunywa na kupikia pia.
Lakini wakumbushe pia zipo mashine au mitambo ya kupunguza chumvi zisizotakiwa kwenye maji na wataalamu wapo watawashauri baada ya hayo maji kuwa yamepimwa maabara kuona ph scale yake inasoma either acidic au alkalinity kiasi gani.

pia waambie maswali na uelewa mwingine ni juu yao kufanya research kidogo kwenye mitandao na hasa ule maarufu wa guguu... waambie wa-gugu kitu kinaitwa reverse osmosis na water desalination plants na mambo nyingine kama hizo.

USISAHAU PIA KUWAKUMBUSHA YALE MANENO YA MH. RAIS MSTAAFU KUWA WATANZANIA NI WAVIVU WA KUFIKIRI na sasahivi tumekuwa wavivu wa kujisomea ila mabingwa wa kuchati kwenye smart phones hasa mambo yasiyokuwa na tija sanaa.

waambie pia sijasema mimi....sema uliyasikia sehemu yanaongewa ndio ukayaleta hapa kutimiza wajibu na jadi yetu ya umbeya umbeya tuu.

2015....for this...for sure i dont n never will care.
 
je mna matawi mikoani, au mtu akitaka kuchimba kisima mkoa kama Dodoma mjini inakuwaje?
 
Back
Top Bottom