Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Mkuu ikizidi 130m gharama zinakuwaje?
je kwa Dodoma bei ikoje?
Mashine zetu zinafika mwisho mita 150 kama kisima chako kinazidi mita hizo tunashauri utafute wachimbaji wengine.
Kwa swala la dodoma ni laziima uwe specific dodoma sehem gani? Kisha tuandae quattn kwa ajili yako.
 
mkuu ungeliweka bei kulingana na urefu mkuu niko serious nitakutafuta je survey ya kucheki kama maji yako au hayako ni bei gani mkuu
Sawa wastani ni 60000 kwa mita, sisi hatufanyi survey ila tunakampuni tunaitumiaga kufanya survey kwa wateja wetu.wanacharge 200000 .
 
tafafhali naomba majibu kwa maswali yangu machache yafuatayo....
I
1-kwa hiyo unamaanisha munachimba mita 1 kwa tshs 60,000/=?...

2-vip kuhusu survey ya uwepo wa maji kwenye site munafanye wenyewe na kwa gharama zipi kama zipo nje ya hiyo elfu 60?

3-vipi kuhusu gharama za ku-mobilize nikimaanisha kupeleka ghari mitambo na wafanyakazi ni juu yenu pia na kama sio ni kiasi gani?

4-vipi kuhusu test za laboratory za maji muliyochimba munafanya nyinyi pia kama sio ni kiasi gani?

5-vipi kuhusu pump ya maji nayo ipo katika gharama zenu za uchimbaji? Kama sio nini uzoefu wako kwa pump ya kuweza kusukuma maji urefu wa mita 100?

Naomba kujulishwa juu ya hizo gharama-ukakasi ambazo hujitokeza kwa wachimba visima mulio wengi wenu. Hizo gharama-ukakasi hukwaza sana hasa kwa sie pangu pakavu tia mchuzi....nisingependa kuwaongelea wenye viroba vyao vya escrow maana wao huingia ndani na kujichotea tuu.

Naomba majibu juu ya hayo kabla sijafanya maamuzi magumu kwenye maisha yangu....kumbuka maji ni uhai.

Sawa mkuu sisi ni wachimbaji kwenye swala la survey tunakampuni hua tunaitumia utawalipa laki 2 kisha watatukabidhi sisi report ambayo itaonyesha urefu wa water table na diameter ya kuchimba,kwa ufupi tunaifuatisha report ya surveyor.
Bei zetu ni wastani 60 elfu kwa mita hii inajumuisha mobilization,usafiri,water treatment,test na pump zote juu yetu,
Nafikiri nimekujibu vyema. Na hii bei ni kwa maeneo ya dsm tu. Hivyo kwa mita zako mia utalipa tshs 6000000(6M).
 
Ndugu ; Unapouza jitahidi kumfanya mteja aelewe zaidi na sio wewe kuwahi kuuza maana lengo ni kumpa maelezo yatakayomuwezesha kufanya "Informed Decision" kwa mfano wewe unajua fika ni mchimba visima ila kuna procedure muhimu ili mteja aweze kuridhika na kuenjoy kisima chake kama water tests, survey analysis , pump selection, etc basi do your homework ujue a bit kuhusu hivi na uweke bayana kuwa ili uchimbiwe kuna kadha wa kadha na sisi kampuni yetu imejikita kwenye uchimbaji per se. na weka all anticipated costs . kwa mtindo huu kunufaika na ujasiriamali tutakwama sana mkuu . Put your self in the shoes of the buyer kabla hujapost ; remember hata uwe na product nzuri kiasi gani kama huna communication and selling skills ni bure . Ni hayo tu Mkuu.
 
evigt haya maswali yote yanayoulizwa hapa ungekuwa umetoa tangazo lako bila kukurupuka na ukaja na taarifa ilitokamilika wala usingepoteza mda wako kijibu maswali yote hayo???

Next time jitahidi kuandaa tangazo lako vizuri
 
Last edited by a moderator:

Asante nitajitahidi.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu ; Unapouza jitahidi kumfanya mteja aelewe zaidi na sio wewe kuwahi kuuza maana lengo ni kumpa maelezo yatakayomuwezesha kufanya "Informed Decision" kwa mfano wewe unajua fika ni mchimba visima ila kuna procedure muhimu ili mteja aweze kuridhika na kuenjoy kisima chake kama water tests, survey analysis , pump selection, etc basi do your homework ujue a bit kuhusu hivi na uweke bayana kuwa ili uchimbiwe kuna kadha wa kadha na sisi kampuni yetu imejikita kwenye uchimbaji per se. na weka all anticipated costs . kwa mtindo huu kunufaika na ujasiriamali tutakwama sana mkuu . Put your self in the shoes of the buyer kabla hujapost ; remember hata uwe na product nzuri kiasi gani kama huna communication and selling skills ni bure . Ni hayo tu Mkuu.
Asante nitachukua moja ya changamoto
 
Asante nitajitahidi.

Asante nitachukua moja ya changamoto

Safi sana mkuu evigt umeonesha ukomavu kupokea hizo changamoto. Kwa hiyo nahitaji kuwa na 200,000 kupewa water survey report na hiyo kampuni nyingine?maana nataka nipate survey report kwanza kisha nijipange na uchimbaji wenyewe (inaweza kuchukua muda kidogo si unajua hali zetu?).
 
Ukiwa na hiyo laki 2 yao,utanistua nikuunganishe kisha utaanza kujipanga.
 
Last edited by a moderator:
ukiwa na hiyo laki 2 yao,utanistua nikuunganishe kisha utaanza kujipanga.

mimi ninayo hiyo laki mbili...nakustuaje ili uniunganishe waje kufanya survey kwenye eneo langu hapa dar mitaa ya goba?

Lakini waambie mie ni mtanzania hakuna biashara inayofanyika bila negotiations na hasa kupunguziwa bei...kama bei yao haipungui ni bora wasije tutachimba tutapoyapata maji hapohapo tunalipana kwa mita mulizochimba kisha nasepa.
 
Ukiniletea surveyor akapima na kudeclare maji yanapatikana katika urefu kadhaa, ukaja ukachimba na maji yasipatikane. Je unabeba hiyo liability?
 
Hizi bei za survey ni fixed bora za kuchimba hua kuna maelewano,kama upo tayari unatupigia simu unatupa appointment sisi tunakuja na surveyor anapiga kazi akimaliza unamlipa then sisi tunafuatilia report ikitoka tunakuletea wewe, kisha utangalia gharama za uchimbaji kama utazimudu tunaleta mashine za kudrill tunaanza kazi.
 
Ukiniletea surveyor akapima na kudeclare maji yanapatikana katika urefu kadhaa, ukaja ukachimba na maji yasipatikane. Je unabeba hiyo liability?

Kiukweli kama ikitokea nitabeba ila surveyor kukosea ni ngumu kwa sababu nae huwa anawajibika kwa upande wetu na anapima zaidi ya mara moja kuprove water table.
 
Sawa mkuu sisi ni wachimbaji kwenye swala la survey tunakampuni hua tunaitumia utawalipa laki 2 kisha watatukabidhi sisi report ambayo itaonyesha urefu wa water table na diameter ya kuchimba,kwa ufupi tunaifuatisha report ya surveyor.
Bei zetu ni wastani 60 elfu kwa mita hii inajumuisha mobilization,usafiri,water treatment,test na pump zote juu yetu,
Nafikiri nimekujibu vyema. Na hii bei ni kwa maeneo ya dsm tu. Hivyo kwa mita zako mia utalipa tshs 6000000(6M).

Mkuu utanisamehe kama nimekosea
Hapo kwenye survey ya Maji natofautiana na utaratibu wenu ..... surveyor anatakiwa awe ni kampuni au MTU ambaye ni independent kabisa ambaye hafungamani wala hana maslahi na kampuni ya uchimbaji wa Maji.... mara nyingi wachimbaji Wa mMaji hushirikiana na surveyors ku- exaggerate ukubwa Wa kazi ..... surveyor anaweza skuta Maji ni let say 70 meters lakini kwa vile anafahamiana na wachimbaji na report itapikwa na kuandikwa 95 meters .... hapo umeliwa 25 meters

mashauri mteja atafute surveyor wake mwenyewe na siyo kuletewa na mchimbaji Wa maji
 
Back
Top Bottom