Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Mh. Stephen Maselle (Naibu Waziri) amesikia akieleza waziwazi kuwakamata na kuwakabidhi kwa RPC viongozi wakuu (wageni) walioshiriki mkakati wa kutorosha dhahabu yetu bila kulipa kodi husika. Huu ni mwanzo mzuri wa uajibikaji bila kuoneana haya wala kuogopa eti sijui huyu ni nani au ana nini au anatoka taifa gani lililoendelea. Tumeanza kuona mwanga. Kazeni buti hivyo hivyo hata kuwashukia wale wa ndani waliotutabiria mgao mkubwa wa umeme mara tu baada ya Bunge kumbe ni wahanga wa hatua mlizoanza kuzichukuwa. Nawashauri muelekeze nguvu zenu pia kukarabati miundombinu ya umeme maana TANESCO itaendelea kupoteza Units kibao kutokana na uchakavu na wananchi tunazihitaji hizo Units kwa ajili ya maendeleo yetu na kwa ajili ya kupunguza gharama za uendeshaji wa Shirika.