Tunaanza kuona mwanga wizara ya nishati na madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaanza kuona mwanga wizara ya nishati na madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Sep 12, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mh. Stephen Maselle (Naibu Waziri) amesikia akieleza waziwazi kuwakamata na kuwakabidhi kwa RPC viongozi wakuu (wageni) walioshiriki mkakati wa kutorosha dhahabu yetu bila kulipa kodi husika. Huu ni mwanzo mzuri wa uajibikaji bila kuoneana haya wala kuogopa eti sijui huyu ni nani au ana nini au anatoka taifa gani lililoendelea. Tumeanza kuona mwanga. Kazeni buti hivyo hivyo hata kuwashukia wale wa ndani waliotutabiria mgao mkubwa wa umeme mara tu baada ya Bunge kumbe ni wahanga wa hatua mlizoanza kuzichukuwa. Nawashauri muelekeze nguvu zenu pia kukarabati miundombinu ya umeme maana TANESCO itaendelea kupoteza Units kibao kutokana na uchakavu na wananchi tunazihitaji hizo Units kwa ajili ya maendeleo yetu na kwa ajili ya kupunguza gharama za uendeshaji wa Shirika.
   
 2. a

  afwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  We ngoja uone Magamba watakavyomgeuka Mh. Maselle na kumtosa!
   
 3. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Hongera zao na tunaomba msikate tamaa.
   
 4. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,239
  Trophy Points: 280
  Kwani kabla ya uwaziri, aliingia bungeni lini??
  Zisije kua alama za nyakati.!
   
 5. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo letu ni maneno mengi. Nini kimemshinda kuchukua hatua mara moja katika hilo na tuone kweli wezi hao wakishughulikiwa? Mtu wa vitendo haongei sana, vitendo ndivyo huongea.

  Ni kwa muda gani tumekuwa tukiibiwa haya madini huku maliasiri zetu zikibakwa kwa kasi ya kutisha? Si hawahawa sasa wameanza kuingia mikataba ya utafutaji na hata uchimbaji mafuta na gesi yetu bila kuwepo kwa sera wala sheria ya mambo hayo? Tunaelezwa tayari kuna watu wameshamega 10 percent zao na wameficha fedha ughaibuni.

  Maselle hana ubavu wowote wa kuyakaba makampuni ya madini, amewekwa kwenye Wizara hiyo strategically kulinda maslahi ya JK na wabakaji wengine wa rasilimali kama ilivyokuwa kwa Ngeleja. Massele ni zao la ufisadi tu (Rejea ukaribu wake na Riz One na uchakachuaji wa kura za Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini). Kwa ujumla chini ya Serikali hii lisitegemewe jipya sana kwenye sekta ya madini.
   
 6. J

  JIS Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Katika vipofu nawewe ni no.1. Hizo naona ni chuki zako binafsi. Kijana Masele ni mfano wa kuigwa katika utendaji kazi wake. Wewe fuatilia tu ziara zake zilivyo na impact, hata wachimbaji wadogo wanamkubali. Hayo uliyoyasema ni majungu na ukipofu wa kutopenda kupongeza mtu anayefanya vyema. Pole sana.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  sanaa tu
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mmeona mwanga wakati kuna mgao wa kisirisiri! Makubwa haya, this is living and other stories by Agoro Anduru!
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  "diplomatic fool"
  huwezi kumsifia mkimbiaji eti amependeza bukta ya mashindano aliyovaa, Mwanariadha husifiwa akimaliza mbio, walisha sifiwa wengi including jk na bado tunaenda mwenda wa kinyonga. Masele hajafanya lolote la kusifiwa. Ndugu zangu epukeni kumsifia mtu kwa kutimiza wajibu wake, ama la sivyo mtamlingana werema kichwa kufugia nywele.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wako ndani hivi sasa unavyoandika.
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Taratibu zinafuata mameneja hao wawili wazungu wafikishwe mahakamani saizi tunapoongea wazugu wamo ndani, sasa sijui wewe ulikuwa unatakaje.
   
 12. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Neutral mind!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi Ngeleja anajisikiaje anapoona kuna watu wanaonyesha uzalendo kwa nchi yao na uadilifu katika utendaji wake wa kazi? Aibu kubwa sana!
   
 14. K

  KENET JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 259
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hapa bado simwungi mkono Mh Stephen Maselle(Naibu waziri).Yeye kaanza na visamaki vidogo badala angeanzia na yale mapapa kama Kampuni ya Barrick Bulyanhulu Gold Mine. Kampuni ya Barrick Bulyanhulu Mine inasafirisha mchanga wenye dhahabu nje ya nchi mankonteina kwa makonteina Je Serikali inajua ni kiasi gani cha dhahabu kilichopo kwenye huo mchanga.Ningemsifu kama angeanza na wizi wa wazi wazi unaofanywa na Kampuni ya Barrick Bulyanhulu Gold Mine kwa kutuambia ni kiasi gani cha madini kilichopo kwenye huo mchanga unaosafirishwa. Maana Wazungu wa Barrick Bulyanhulu ni wajanja na wezi wa madini yetu wanazalisha kiasi kidogo hapa nchini kukwepa kodi na kile kikubwa wanakiacha kwenye huo mchanga na kusafirisha nje ya nchi kwenda kusafisha dhahabu huko bila ya wazawa kujua ni kiasi gani wanakwenda kupata.
   
 15. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145

  Yaani mazee na wale wanaotorosha kwa ndege? waache hizo.... sitaki kuwakatisha tamaa yumkini wana nia ya kweli!! tuanze kufuatilia records za wanaochimba madini wote tukin'gamua tu.. tunawachukulia hatua!! isije ikawa wanakula chobis kdgo kupisha upepo halafu haooooo shambani kwa BIBI kalembwana!!
   
 16. +255

  +255 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Labda sehemu uliopo wewe...
   
 17. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina imani na mawaziri hawa ebu tuwape muda wanaweza kutoa kiu ya watanzania katika hii wizara.
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Huko masaki wewe unakoishi hakuna mgao wa kisirisiri? Au unachukulia ni maisha ya kawaida umeme once in a while kukatika kwa masaa 10 hivi bila maelezo? Kuzoea shida nayo ni shida unajua?
   
 19. papason

  papason JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mbona wanakamata dagaa tuu wakati mapapa yanapeta kila siku kwa taarifa huyu mzungu alikuwa kota/ broker tuu tena miaka ya zaidi ya 15 aki process marudio ya wachimbaji wadogo wadogo!

  Awakamate wale wanaotorosha matofali ya dhahabu usiku wa manane kwa mindege yao inayoruka direct toka migodin mpaka RZA!
   
 20. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unaposema mimi ni kipofu nakushangaa. Hizi mbwembwe hazikuanza leo. Ziko wapi kaulimbiu kama Za Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya? , Maisha Bora kwa Kila Mtanzania Je? Vipi kuhusu Ari Zaidi, Kasi Zaidi na Nguvu Zaidi? Kilimo Kwanza Je?

  Lakini kwenye sekta ya Madini yenyewe mapendekezo ya Tume ya Bomani na akina Zitto yako wapi? Yamefanyiwa kazi? Si yako kabatini? Kila mtu alitegemea matokeo ya tume ya Bomani yangeleta mageuzi kwenye sekta ya Madini lakini wapi?

  Siwezi kuwa na chuki binafsi na Maselle wala mtu yeyote, suala hapa ni maigizo ambayo tumekuwa tukiletewa.Unasema Masselle anasifiwa na wachimbaji wadogo. Real? Si huyuhuyu juzi alikuwa Mererani akatoa lukuki kwa wachimbaji wadogo lakini baada ya siku kadhaa tukasikia wamepigwa risasi na Makaburu wa Tanzanite One? Wanamsifia vipi? Kilio cha kupewa maeneo ya kuchimba madini kimeisha? Mbona juzi tu Nyamongo watu wamefyatuliwa risasi? Sasa tusianze kusifiana wakati uozo umejaa kibao. Hata kama kweli ndiyo anaanza kazi bado kazi iliyoko mbele ni ngumu zaidi.
   
Loading...