Tunaambiwa tule nyama na maziwa tupate protein; Je, ng’ombe hutoa wapi hizo protein na hali nyama wala kunywa maziwa?

Jaribu kula Majani kama ng'ombe uone kama utaishi (simaanishi vegetables) namaanisha majani grass..., au mpe ng'ombe nyama uone atafikia wapi...

Ngombe ni ruminants na tumbo lao lina microbacteria ambao wanasaidia kwenye digesion kufanya hayo majani ambayo ukila wewe ni uchafu ila kwa ngombe ni tofauti...,

Hii yote ni kufacilitate ecosystem ndio maana kuna herbivores, carnivores na omnivores.., wanyawa wote wangekuwa wanakula nyama mwisho wa siku animals kama species wangetoweka..., nature has got to balance Its Nature
Sawa, na vipi kuhusu Vegetarians? Na kwanini watu wanaokula nyama sana huzeeka haraka?
 
Ulisoma science mkuu? End product ya protein unayoipata kutoka kwenye nyama ni amino acid,hili liko wazi kabisa kama ambavyo end product ya wanga (carbohydrates) ni glucose, this is very obvious fact, tumesoma shuleni... Nikuulize unajua end product ya maziwa? Hebu jibu hayo kwanza ili tuingie kwenye dhana ya herbivores kula nyasi na kuweza kujenga miili yao ambayo mostly ni proteins....
Kwani tuna ugomvi? Soma thread zangu za nyuma kama unataka kujua elimu yangu. Rudi kwenye swali langu.
 
Moderator futen na huu uzi pia ni utopolo mtupu maswal ya namna hii ukiwaza unaweza kujiona genius kumbe hamna kitu

Kuna vitu ni natural resource kuhoj vimetokea wap na nan kaviweka ni Kupoteza nda wa wadau

Sio kwamba uzi umekuzidi uwezo wako wa kufikiri kwahiyo unakutisha na kukuogopesha
 
Sawa, na vipi kuhusu Vegetarians? Na kwanini watu wanaokula nyama sana huzeeka haraka?
Mkuu too much of anything ni kibaya ndio maana kuna balanced diet..., na kumbuka hizi processed meats zina makemikali ambayo ni mabaya..., ingawa sitaki kwenda in detail kwamba kula nyama ni kubaya au watu wasile nyama bila kuwa na 100 % proof and research kwamba even a small amount ni mbaya...., tuongelee vitu ambavyo vipo proven, ni kweli too much meat ni mbaya kiafya (nadhani too much of anything ni mbaya) hata ukila mchicha kwa sana na some leafy green (zina oxalate acids nyingi ) kwahio ukila kupita kiasi unaweza kupata kidney stones..., Na kwa sasa kimazingira hata hizo nyama / maziwa unayokunywa yanatokana na ngombe wanaokula too much grains/energy feeds amabazo naturally ilibidi wale majani (sio mavyakula ili waweze kukua kwa muda mfupi)...

Ila ukweli ambao haupingiki kula nyama ni mbaya kwa mazingira... ? Kwanini ? Inachukua Kama Kilo Saba za Grains ku-raise 1 Kg ya Nyama...., kwahio kila mtu akila nyama kwa sana hii dunia haiwezi kukidhi..., Brazil wanalima mahekari ya Soya sababu ya kulisha mifugo..., marekani kuna mahekali na mahekali ya mahindi kwa ajili ya kulisha mifugo....., ingawa ardhi hio hio ingeweza kutumika kutoa kilo nyingi zaidi za mazao kuliko kilo za nyama....

Kwahio hapo Nature inakwambia nyama sio za kula kila siku labda mara moja moja au tuwaachie nyama wale carnivores ambao wanazihitaji zaidi for their survival sisi tuna options.... Na hii dunia ambayo binadamu wanazidi na kuongezeka kila dakika exponentially (kwa macho ya dunia / nature) binadamu pia ni an invasive specie ambaye ni mbaya sana kwa mazingira na ni muharibifu kupita kiasi (ameshindwa kuishi vema na species wengine)
 
Je, ina maana binadamu anaweza kuishi bila kula nyama, mayai, wala maziwa na akapata protein zote anazohitaji toka kwenye vyakula vya mimea (vegetable based)?

Mkuu mbona easy sana hili swali lako.
Iko hivi binadamu ana vimeng’enya yaani enzymes ambazo ni tofauti na ng’ombe kwa mfano enzyme inayoweza kumeng’enya cellulose (uncooked starch) ipo kwa ng’ombe ndio maana wewe ukijaribu kula uncooked starch utaishia kuharisha tu maana hakuna enzyme ya kumeng’enya hizo cellulose ndani yako.

Kwa ufupi ni hivi, kuna vyakula huwezi kuvila bila kupika na kuna vyakula huwezi kupata nutrients zake directly bila kupitia kiumbe kingine maana yake unavyipata vikiwa katika simple form ambayo kwako unaweza digest na kupata nutrients.
 
Kwani kwa mfano ng'ombe chakula chake pekee ni majani?? Na pia usisahau wanyama wanahitaji protein ili wajenge miili yao wakue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom