Inashauriwa kutochanganya Maziwa na Ndizi au Mayai na Kitimoto wakati wa kula

Aug 31, 2022
54
99
sources-protein-dieting.jpg

Wataalamu wa Lishe wanashauri kutokula Mayai na Kitimoto kwa pamoja kutokana na kuwa na wingi wa Virutubisho vya Protini ambavyo husababisha Tumbo kutumia muda mrefu kumeng'enya Chakula. Inapendekezwa kula Mayai kwanza na Nyama ifuate angalau baada ya nusu saa.

Matumizi ya Matunda yenye Asidi au Sharubati (Juice) itokanayo na Machungwa haipaswi kutumika kwa pamoja na Maziwa ili kuepusha kuganda kwa Maziwa, hali ambayo husababisha Gesi kujaa Tumboni.

Mchanganyiko wa Maziwa na Ndizi hutumia muda mrefu kumeng'enywa na kusababisha mwili kupata uchovu. Kwa wanaopenda Mchanganyiko wa Ndizi na Maziwa (Smoothie) wanashauriwa kuongeza Unga wa Mdalasini au Kungumanga ili kusaidia umeng'enyaji wa haraka.

=================

Tovuti ya india.com, inabainisha kuna vyakula vikichanganywa huleta madhara katika mwili wa binadamu na haishauriwi kutumiwa kwa wakati mmoja.

Mayai na nyama ya nguruwe kitaalamu hivi haviruhusiwi kutumika kwa wakati mmoja, kwa kuwa atakayetumia kwa kula basi anaweza kupata changamoto ya kiafya.

Vyakula hivi viwili vina protini nyingi na huwa vizito katika tumbo, hivyo itachukua muda mrefu kusaga vyakula vyote viwili.

Hata hivyo, matumizi ya sharubati itokanayo na machungwa pamoja na matumizi ya maziwa havitakiwi kutumika kwa pamoja kwa kuwa huchukua muda kumeng’enywa mwilini.

Unapotumia maziwa na machungwa, maziwa huganda na kusababisha gesi tumboni.

Chakula cha jibini na kinywaji baridi, muunganiko huu huleta madhara katika mwili wa binadamu kwa kuwa mchanganyiko unaweza kusababisha maumivu ya tumbo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Health, vyakula kama ndizi na maziwa, nyama na viazi vinaweza kuleta changamoto endapo vikitumiwa kwa wakati mmoja.

Mfano matumizi ya viazi na nyama kwa wakati mmoja huweza kusababisha matatizo ya umeng’enyaji chakula au matatizo ya tumbo.

Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa Lishe, Sweetbert Njuu anasema nyama na maziwa havitakiwi kutumiwa pamoja kwa kuwa mtu hataweza kupata faida vyote vikitumika pamoja.

“Vyakula hivi vinashauriwa angalau vipishane saa moja endapo mtu atatumia, kwa sababu madini ya chuma na madini ya kalsiamu yanakinzana,” anasema Njuu

Anasema matumizi ya pombe husababisha ufanisi mbaya wa ufyonzaji wa chakula mwilini, hivyo pombe haishauriwi kutumiwa endapo mtu anakula chakula.

“Ikiwa mtu amekunywa pombe nyingi sana na wakati huohuo amekula chakula chenye sifa ya mlo kamili, basi uwezekano wa ufyonzaji chakula unaweza kufika asilimia 50,” anasema Njuu.

Hata hivyo, matumizi ya matunda na nafaka zisizokobolewa kwa wakati mmoja kitaalamu huweza kusababisha baadhi ya changamoto katika tumbo, mfano tumbo kujaa gesi.

Sweetbert Njuu anasema watu wanatakiwa kuzingatia matumizi ya lishe bora ambayo, huwa na mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa, vyakula vitokanayo na mizizi, matumizi ya protini nzuri yaani nyama zisizo na mafuta na bila kusahau kunywa maji ya kutosha.
 
Bana weee!! hayo ni matumbo ya wazungu!!wahindi na waarabu!....ngozi nyeusi sie bana ni utamu ku mudomo tuuu baaasi!! kwanza hatutaki kunenepeana wacha viende huko vigandane weeee! then nita vitoa vyote km mavi!

hii ndo dawa ya mabonge!
Eti wanataka kutupangia tule nini!Hawajui kwamba hata hichi tunachokula tunakipata kwa taabu sana. Watuache bhana waende wakafanye kazi zingine huko.
 
sources-protein-dieting.jpg

Wataalamu wa Lishe wanashauri kutokula Mayai na Kitimoto kwa pamoja kutokana na kuwa na wingi wa Virutubisho vya Protini ambavyo husababisha Tumbo kutumia muda mrefu kumeng'enya Chakula. Inapendekezwa kula Mayai kwanza na Nyama ifuate angalau baada ya nusu saa.

Matumizi ya Matunda yenye Asidi au Sharubati (Juice) itokanayo na Machungwa haipaswi kutumika kwa pamoja na Maziwa ili kuepusha kuganda kwa Maziwa, hali ambayo husababisha Gesi kujaa Tumboni.

Mchanganyiko wa Maziwa na Ndizi hutumia muda mrefu kumeng'enywa na kusababisha mwili kupata uchovu. Kwa wanaopenda Mchanganyiko wa Ndizi na Maziwa (Smoothie) wanashauriwa kuongeza Unga wa Mdalasini au Kungumanga ili kusaidia umeng'enyaji wa haraka.

=================

Tovuti ya india.com, inabainisha kuna vyakula vikichanganywa huleta madhara katika mwili wa binadamu na haishauriwi kutumiwa kwa wakati mmoja.

Mayai na nyama ya nguruwe kitaalamu hivi haviruhusiwi kutumika kwa wakati mmoja, kwa kuwa atakayetumia kwa kula basi anaweza kupata changamoto ya kiafya.

Vyakula hivi viwili vina protini nyingi na huwa vizito katika tumbo, hivyo itachukua muda mrefu kusaga vyakula vyote viwili.

Hata hivyo, matumizi ya sharubati itokanayo na machungwa pamoja na matumizi ya maziwa havitakiwi kutumika kwa pamoja kwa kuwa huchukua muda kumeng’enywa mwilini.

Unapotumia maziwa na machungwa, maziwa huganda na kusababisha gesi tumboni.

Chakula cha jibini na kinywaji baridi, muunganiko huu huleta madhara katika mwili wa binadamu kwa kuwa mchanganyiko unaweza kusababisha maumivu ya tumbo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Health, vyakula kama ndizi na maziwa, nyama na viazi vinaweza kuleta changamoto endapo vikitumiwa kwa wakati mmoja.

Mfano matumizi ya viazi na nyama kwa wakati mmoja huweza kusababisha matatizo ya umeng’enyaji chakula au matatizo ya tumbo.

Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa Lishe, Sweetbert Njuu anasema nyama na maziwa havitakiwi kutumiwa pamoja kwa kuwa mtu hataweza kupata faida vyote vikitumika pamoja.

“Vyakula hivi vinashauriwa angalau vipishane saa moja endapo mtu atatumia, kwa sababu madini ya chuma na madini ya kalsiamu yanakinzana,” anasema Njuu

Anasema matumizi ya pombe husababisha ufanisi mbaya wa ufyonzaji wa chakula mwilini, hivyo pombe haishauriwi kutumiwa endapo mtu anakula chakula.

“Ikiwa mtu amekunywa pombe nyingi sana na wakati huohuo amekula chakula chenye sifa ya mlo kamili, basi uwezekano wa ufyonzaji chakula unaweza kufika asilimia 50,” anasema Njuu.

Hata hivyo, matumizi ya matunda na nafaka zisizokobolewa kwa wakati mmoja kitaalamu huweza kusababisha baadhi ya changamoto katika tumbo, mfano tumbo kujaa gesi.

Sweetbert Njuu anasema watu wanatakiwa kuzingatia matumizi ya lishe bora ambayo, huwa na mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa, vyakula vitokanayo na mizizi, matumizi ya protini nzuri yaani nyama zisizo na mafuta na bila kusahau kunywa maji ya kutosha.
Kibongo bongo unakula tu kila kilicho mbele yako. Mwenye nafasi yake ndo atachora hiyo ramani ya mlo.
 
Mbona ni kama haituhusu sana sisi wa huku vijijini? au mnasahau au mnajifanya hamjui kwamba Sisi huku mara nyingi tunakulaga vyakula kama mnafu,makukuru,ugali(dona) ndizi za kuchemsha,maziwa mgando, mgagani, majumbao, ndulele changa, tembele, mbwembwe(mashonanguo) na maji ya visimani?, Pombe zetu ni Taputapu, kangara, komoni, ufuge n.k. Mambo ya juisi,mayai, cjui nini na nini tunavipata cku tukijawasalimia huko mjini. Kwa hiyo sisi mnatuambiaje kwa mfano.
 
Nilichanganya wanawake tu kidogo nife huku nina kesi ya kumpa mimba hausigeli nyumbani, huku nimefumaniwa na mke wa mkuu wa wilaya, huku kuna kimwanafunzi kina mimba kimetaja watu watatu, na mimi nimo na kimenitolea macho kichizi
sources-protein-dieting.jpg

Wataalamu wa Lishe wanashauri kutokula Mayai na Kitimoto kwa pamoja kutokana na kuwa na wingi wa Virutubisho vya Protini ambavyo husababisha Tumbo kutumia muda mrefu kumeng'enya Chakula. Inapendekezwa kula Mayai kwanza na Nyama ifuate angalau baada ya nusu saa.

Matumizi ya Matunda yenye Asidi au Sharubati (Juice) itokanayo na Machungwa haipaswi kutumika kwa pamoja na Maziwa ili kuepusha kuganda kwa Maziwa, hali ambayo husababisha Gesi kujaa Tumboni.

Mchanganyiko wa Maziwa na Ndizi hutumia muda mrefu kumeng'enywa na kusababisha mwili kupata uchovu. Kwa wanaopenda Mchanganyiko wa Ndizi na Maziwa (Smoothie) wanashauriwa kuongeza Unga wa Mdalasini au Kungumanga ili kusaidia umeng'enyaji wa haraka.

=================

Tovuti ya india.com, inabainisha kuna vyakula vikichanganywa huleta madhara katika mwili wa binadamu na haishauriwi kutumiwa kwa wakati mmoja.

Mayai na nyama ya nguruwe kitaalamu hivi haviruhusiwi kutumika kwa wakati mmoja, kwa kuwa atakayetumia kwa kula basi anaweza kupata changamoto ya kiafya.

Vyakula hivi viwili vina protini nyingi na huwa vizito katika tumbo, hivyo itachukua muda mrefu kusaga vyakula vyote viwili.

Hata hivyo, matumizi ya sharubati itokanayo na machungwa pamoja na matumizi ya maziwa havitakiwi kutumika kwa pamoja kwa kuwa huchukua muda kumeng’enywa mwilini.

Unapotumia maziwa na machungwa, maziwa huganda na kusababisha gesi tumboni.

Chakula cha jibini na kinywaji baridi, muunganiko huu huleta madhara katika mwili wa binadamu kwa kuwa mchanganyiko unaweza kusababisha maumivu ya tumbo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Health, vyakula kama ndizi na maziwa, nyama na viazi vinaweza kuleta changamoto endapo vikitumiwa kwa wakati mmoja.

Mfano matumizi ya viazi na nyama kwa wakati mmoja huweza kusababisha matatizo ya umeng’enyaji chakula au matatizo ya tumbo.

Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa Lishe, Sweetbert Njuu anasema nyama na maziwa havitakiwi kutumiwa pamoja kwa kuwa mtu hataweza kupata faida vyote vikitumika pamoja.

“Vyakula hivi vinashauriwa angalau vipishane saa moja endapo mtu atatumia, kwa sababu madini ya chuma na madini ya kalsiamu yanakinzana,” anasema Njuu

Anasema matumizi ya pombe husababisha ufanisi mbaya wa ufyonzaji wa chakula mwilini, hivyo pombe haishauriwi kutumiwa endapo mtu anakula chakula.

“Ikiwa mtu amekunywa pombe nyingi sana na wakati huohuo amekula chakula chenye sifa ya mlo kamili, basi uwezekano wa ufyonzaji chakula unaweza kufika asilimia 50,” anasema Njuu.

Hata hivyo, matumizi ya matunda na nafaka zisizokobolewa kwa wakati mmoja kitaalamu huweza kusababisha baadhi ya changamoto katika tumbo, mfano tumbo kujaa gesi.

Sweetbert Njuu anasema watu wanatakiwa kuzingatia matumizi ya lishe bora ambayo, huwa na mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa, vyakula vitokanayo na mizizi, matumizi ya protini nzuri yaani nyama zisizo na mafuta na bila kusahau kunywa maji ya kutosha.
 
Kula nitakula na ikiwezekana nitaongeza zaidi
Ndio kabisa. Mwili wa biadamu sio kama injini ya gari eti ukiweka dizeli kwenye injini ya petroli gari haikubali/haiwaki. Kwa mwili wa binadamu(au mnyama yeyote) ni tofauti kabisa. We kula ulacho mwili utajiseti wenyewe kwa kufanya yafuatayo: 1. Ukila kisichofaa utatapika au utaharisha, ukila sumu utapambana kwa kukojoa n.k. ikikuzidi utakufa au utapona kwa polepole. Ukila kilicho chema utaendelea na mishe zako kama kawaida hutoona tatizo.
2. Mwili hupanga(Involuntarily) bila hiari yako yale yaliyo ni muhimu kwa mustakabali wa uhai wako uendelee e.g. kupumua, kupiga chafya, kuhisi njaa, kusinzia/kulala n.k.
Hivi tujiulize, mababu zetu wale walioweza kuishi (Na baadhi yao wapo hai mpaka leo wanadunda) miaka 90 - 120 walifanya hayo jamaa (Wataalam) wanayotuambia?
 
Nilichanganya wanawake tu kidogo nife huku nina kesi ya kumpa mimba hausigeli nyumbani, huku nimefumaniwa na mke wa mkuu wa wilaya, huku kuna kimwanafunzi kina mimba kimetaja watu watatu, na mimi nimo na kimenitolea macho kichizi
Vipi na kale kaUgonjwa, hiyo umeweza kusevu adiabatically? Pole mkuu- komaa na hali yako.
 
Back
Top Bottom