Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Ni kama nchi haina Wizara ya Mifugo au inayo lakini bila Waziri na Watendaji wake.
Kuna tabia imekita mizizi na kuwa sugu ya wasafirishaji wa mifugo (kwenye malori) kwenda machinjioni kutesa wanyama hao kwa viwango vilivyopitiliza na hakuna anayediriki kupaza sauti kupinga ukatili huu unaowafanya binadamu wanaowasafirisha kuwa ni wanyama zaidi na halisi kuliko mifugo hiyo.
Wavuta bangi ya Arumeru hawa wamekuwa wakipiga ng'ombe hawa kwa kutaka sifa kwenye kadamnasi. Wanapopita karibu nami huwa nafunga macho au nakimbia uchochoroni nisishuhudie mateso hayo.
Ile kwamba ng'ombe hao wanaenda kuchinjwa haiwaondolei haki ya kufikishwa sokoni wakiwa katika hali salama kama bidhaa zingine.
Wasukuma hawa, Wagogo hawa na Wamang'ati hawa huwa wanapofika kwenye satellite towns (na mijini huko wapitako) kama Mbezi Msigani, Marambamawili, Kifuru, Kinyerezi, Segerea huwapiga ng'ombe hao kipigo cha Pakamwizi kwa sifa ili waonekane kwa watu waliojaa senta hizo huku wahuni wakiwashangilia kwa nderemo na vifijo utadhani timu fulani imefunga magoli 5.
Ng'ombe wameshonwa kwenye lori bila mpangilio bila nafasi huku wengine wakichomwa na kutobolewa kwa mapembe yale ya Ankole na wengine wakinyea midomo ya wenzao, shingo za ng'ombe zimekunjana hawawezi kuzinyoosha, jua kali la utosini (huenda wana kiu) turubai likiwa limekaliwa na wavuta bangi hawa bila kulifungua kuwakingia jua ili ng'ombe hawa wasiendelee kuwa de-hydrated (kupoteza maji mwilini).
Binadamu tu akiwashwa bila kujikuna anaweza kupiga mayowe (ukunga), vidole vya ng'ombe kujikunia ni mkia wake, sasa anajikunaje kwenye hali ile? Kwa siku nzima ng'ombe hujikuna kwa mkia wake zaidi ya mara 500.
Akisafirishwa kwa siku 2 bila uhuru au ruhusa ya kutumia mkia wake ni mateso kama mateso mengine na ni sawa na kumzuia binadamu kujikuna ukurutu wake unaomuwasha sana.
Wanasafirishwa masafa marefu bila majani kiasi kwamba hata ubora wa nyama yenyewe unapotea, hata uzito wao unapunguzwa na ukatili huu.
Kwa kuwa na mzigo moyoni na jambo hili mara mbili kwa nyakati tofauti niliamua kwenda kuweka ambush Mbezi Msigani (njia wanayoipenda kufika Vingunguti) nikiwa na pikipiki nyuma yao hadi Vingunguti nikabaini kwamba wala ngada hawa huwa wanapanda mori na midadi ya kuwafanyia viumbe hawa ukatili uliopindukia pale wanapofika kwenye maeneo ya senta yenye watu wengi kama nilivyozitaja hapo na maeneo wanayokumbana na foleni.
Waziri wa Mifugo ajuwe kwamba usafirishaji mifugo kwa kutumia malori ni utaratibu ambao dunia imeisha achana nao miongo mingi tu ili kulinda ubora wa mazao ya mifugo hiyo kama nyama, kwato, pembe na ngozi lakini pia kukinga viumbe hawa na mateso wasiyostahili lakini pia kuokoa barabara zetu na shinikizo la shehena kubwa ya mifugo hii zikiwemo bidhaa zingine.
Matrafiki wanashuhudia ukatili huu hawakemei. Maaskari wa doria wanashuhudia ukatili huu hawakemei. Maafisa Mifugo wanashuhudia ukatili huu hawakemei. Waziri na watendaji wake wanayajuwa haya hawakemei, wakati fulani Waziri na watendaji wao wanapishana na malori hayo ya mifugo njiani watokapo au waendapo Dodoma na kuwapigia king'ora tu kuwapa ishara kwamba wawapishe wanawahi.
Kwa staili hii mbovu na kwa sifa kwamba Tz ni ya pili kwa idadi ya mifugo Afrika nyuma ya Ethiopia na ikifuatiwa namba 3 na Cameroon tutaweza kuishi kwenye dunia hii ya ushindani wa ubora wa bidhaa na huduma?
Kutoa tu tamko la kukemea ukatili huu inahitaji kusomea digrii na kuomba bajeti ya posho ya kukemea?
Enzi za Mwl. Nyerere ambapo nchi haikuwa na barabara nzuri mifugo ilisafirishwa kwa garimoshi kwenye mabehewa maalum yenye majani na maji ya kunywa ambapo hawawakiwi jua wala kupigwa mvua ya mawe toka Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kaskazini hadi Dar.
Ni kipindi hicho mazao ya mifugo toka Tz yalitamalaki masoko ya ng'ambo ya bahari kutokana na ubora wake.
Sasa barabara zimekuwa nzuri ili mateso na ukatili vishamiri kwa mifugo?.
Mifugo hii ndiyo inamhudumia kila mtu katika nchi hii anayefuga na asiyefuga. 90% ya kilimo nchini Tz kinalimwa na ng'ombe kwa kuwa wakulima wengi hawewezi kumudu bei kubwa ya matrekta.
Hivyo kwenye kapu la chakula (food basket) nchi hii ng'ombe wanachangia kwa 90% kuliko binadamu wanaolima kwa mikono na kuliko matrekta ambayo ni machache kutokana na bei zake kuwa ghali.
Asilimia kubwa ya maboresho ya afya zetu zinategemea mifugo hii je, tunaweza kuwa na afya bila nyama, maziwa na bila damu za mifugo?
Je, jamii za wafugaji kama Maasai na Datooga (wasiokula nafaka na mazao ya mimea) zinaweza kuwepo kwenye sayari bila mifugo?
Kiwango cha ukatili huu unanifanya wakati fulani kudhani kwamba serikali ipige marufuku kusafirisha mifugo kwa malori ili TRC irejee kwenye biashara hiyo ili pia ijipatie mapato humo lakini pia tupate mazao bora yatokanayo na mifugo hiyo ambayo tunaweza kuuza hata kwenye masoko ya ng'ambo ya bahari.
Sheria kama zipo kudhibiti hali hii na hazifanyi kazi kuna haja gani kuwa nazo?
Nchini Kenya hapo Punda anakatiwa leseni kama gari (anachukuliwa kama chombo cha usafirishaji), leseni ina masharti yake ikiwemo kutobeba shehena (mzigo) uliozidi uwezo wake.
Askari akikuta Punda anafanyiwa ukatili anakuchukulia hatua kali za kisheria. Kwenda kujifunza hapo Kenya tunahitaji mabilioni mangapi ya pesa?
Ujumbe huu ukifikia mamlaka za uteuzi wa watendaji hao naomba uwajibikaji uwepo hima.