Tuna vyuo vya Kilimo lakini hatuna wakulima wakubwa, Tuna SIDO lakini hatuna viwanda vidogo

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
Wakuu

Hili suala nimekua nalifikiria mara kwa mara

Tuna chuo Kikuu cha kilimo SUA lakini kwanini hakuna wanafunzi au walimu wanaotoka pale na kua wakulima wakubwa na bora. Wote wakimaliza pale wanaamini kwamba wanatakiwa waajiriwe maofisini. Ina maana hawa walienda chuo cha kilimo ili waajiriwe au wawe wakulima. Tatizo liko wapi

Pia hata hiko chuo hakina mashamba makubwa na bora yaani plantations au largest ranches za ufugaji Tanzania. Tatizo liko wapi

Tuna Vyuo vya Uvuvi visivyo na meli kubwa sana za Uvuvi Afrika Masharaiki na kati

Tuna Shirka la SIDO lenye jukumku la kuendeleza viwanda vidogo. Lakini sioni hivyo viwanda vidogo vilivyotokana na SIDO. Tatizo liko wapi

Tuna Tume ya Sayansi isiyofanya sayansi yoyote wala isiyo vumbua na kugundua mambo yoyote mapya yakisanayansi. Hawa jamaa hua wanafanya nini

Kwanini chuo cha veta hakina gereji bora kabisa na yabei nafuu sana Tanzania na shirika la ujenzi bora nala bei nafuu sana

Chuo cha Ardhi kwanini hakina student archtects bora nawa bei nafuu sana?

Tuna bodi ya mikopo ya vyuo vikuu inayotegemea rudhuku kutoka serikalini wakati imekua inakopesha watu zaidi ya miaka 20. Kwanini sasa isiwe na fedha zao wenyewe na kujiendesha bila utegemezi wa serikali kifedha

Tuna benki ya wakulima ambayo sijaona wala kusikia success story zao za kuzalisha wakulima wakubwa na plantations

Tuna benki ya TIB Tanzania Invetment Bank ambayo sijasikia success story yoyote kutoka kwa wafanya biashara au wawekezaji kwa jisni ilivyowasaidia na kuzalisha wafanya biashara wakubwa au viwanda vikubwa

List ni ndefu ya taasisi zinazo jinasibu kufundisga taalamu fulani lakini hazina maeneo yakuonyesha hicho wanachofundisha na kusaidia jamii katika nyanja hiyo wenye utaalamu nayo

Tatizo ni nini hasa. Je ni mifumo, au mitaji, au mindest au siasa au nini? Tunakosea wapi?
 
Mawazo mgando kweli. Kwani IFM au TIA wanamiliki mabenki na maduka makubwa kwa sababu ya kufundisha Uhasibu na Biashara? Kazi ya chuo ni kufundisha kupitia maabara, vishamba vidogo vya mafunzo na kupitia ushirikiano na taasisi zingine wakati wa field training na sio kufanya uzalishaji au biashara moja kwa moja. Vyuo havina shida,shida ipo kwenye mipango ya serikali. Mtu anamaliza veta lakini hapewi msaada wa kununua vifaa vya ufundi kwanini asiwe bodaboda! Theres a lot to be done at gvt level than blaming training institutes
 
Elimu ya nadhari bado inatupiga mweleka sana. Elimu kwa vitendo iboreshwe ili wasomi waive kivitendo
 
Elimu ya nadhari bado inatupiga mweleka sana. Elimu kwa vitendo iboreshwe ili wasomi waive kivitendo

Ni kweli kuna uwezekano vijana wengi wa veta wanaosoma machenics wakimaliza wanakua bado hawawezi kutengeza gari iliyoharibika na kufungua gereji. Sidhani kama inahitajika mtaji mkubwa kufungua gereji
 
We jamaa ni kilaza kweli, yaani unaona mawazo ya mtoa mada ni mawazo mgando kuliko ulichocomment hapa?
Mawazo mgando kweli. Kwani IFM au TIA wanamiliki mabenki na maduka makubwa kwa sababu ya kufundisha Uhasibu na Biashara? Kazi ya chuo ni kufundisha kupitia maabara, vishamba vidogo vya mafunzo na kupitia ushirikiano na taasisi zingine wakati wa field training na sio kufanya uzalishaji au biashara moja kwa moja. Vyuo havina shida,shida ipo kwenye mipango ya serikali. Mtu anamaliza veta lakini hapewi msaada wa kununua vifaa vya ufundi kwanini asiwe bodaboda! Theres a lot to be done at gvt level than blaming training institutes
 
Ni kweli kuna uwezekano vijana wengi wa veta wanaosoma machenics wakimaliza wanakua bado hawawezi kutengeza gari iliyoharibika na kufungua gereji. Sidhani kama inahitajika mtaji mkubwa kufungua gereji
Colabo pia inatosha katika kuanza kuinuka ukiwa na mtaji mdogo.

Mara nyingi nafsi zetu pia zinakwama sana katika mambo kama haya ya kushirikiana.
 
Hili ni kweli linafikirisha Sana,nadhani ni muda wa kutafakari na wahusika kuchukua hatua,ikiwa ni wahitimu na serikali mfano wahitimu toka SUA kuungana kuanzisha kilimo Cha kisasa na kupewa vitendea kazi iwe kwa ruzuku au mkopo na wengine kadhalika...ila Nina tashwishwi na utekelezaji wake maana Kuna mwaka vijana Fulani toka chuo jina kapuni walipewa mikopo na benki jina kapuni lakini matokeo yake yalikuwa aibu tupu..NAUNGA MKONO HOJA 100%
 
We jamaa ni kilaza kweli, yaani unaona mawazo ya mtoa mada ni mawazo mgando kuliko ulichocomment hapa?
Nakazia,
Kwenye taasisi kuna shida sana, mbali na serikali kuwa na shida zake, ndio maana serikali inakuwa busy kugawa rudhuku kwenye taasisi kama HESLB, ttcl na atcl, wakati kama kungekuwa na mifumo mizuri zingejiendesha zenyewe.
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Hivyo taasisi hizo hazina tija wala ufanisi zimebaki kua mzigo. Taasisi ikiwa mzigo kwa muda mrefu ni bora zaidi ingebinafsishwa kwa mtindo wa Private Public Partnership PPP
 
Chief binafsi sidhani kama hili ni jukumu la serikali parse. Nadhani wakati umefika tuache kuitegemea sana serikali. Hizo taasisi zina viongozi na wadau yaani stakeholders. Hilo ni jukumu la stakeholders
Serikali inatakiwa itunge sheria na iweke sera ambazo zitaweka huru hizo taasisi zijitegemee na sio kutegemea rudhuku ya serikali.
 
Back
Top Bottom