SoC03 Sido iwe kichochezi katika kilimo cha kisasa hapa nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Tibaiwa

Member
Sep 8, 2021
50
38
Mapinduzi ya viwanda yalileta mwamko mkubwa sana katika mataifa ya magharibi katika uzalishaji mali na kuudondosha mfumo wa “utumwa” baada ya kutengeneza zana bora za kiutendaji ambazo zilianza kufanya kazi zilizokuwa zikifanywa na watumwa pamoja na wanyama na zikaja kuwapiku kwa kuongeza kiwango kikubwa cha uzalishaji wa bidhaa sambamba na mazao yaliyotoka mashambani ukiachilia mbali suala la watetezi wa haki za kibinadamu.

Tanzania yetu hasa kwenye maeneo ya vijijini ambako suala la kilimo halijapewa kipaumbele bado tupo kwenye “utumwa wa kilimo” yaani kilimo cha mkono.

Kilimo cha kutumia jembe la mkono hata pia maksai bado ni utumwa unaohitaji suruhu ya kimapinduzi kama yale yaliyofanywa na mataifa ya magharibi katika karne ya kumi na nane (18) hadi ya kumi na tisa (19), jukumu hili la mapinduzi haya hapa nchini kupitia kilimo kwa kutumia zana za kisasa linapaswa kubebwa na SIDO.
SIDO nini?

Hili ni shirika lililoanzishwa kwa sheria ya bunge namba 28 ya mwaka 1973, lengo likiwa ni kuhudumia viwanda vidogo na kusaidia uzalishaji wa miradi ya viwanda vidogo vijijini. (maelezo haya ni kwa msaada wa mtandao).

Picha kamili ni ujio wa “bodaboda” kupitia Mapinduzi ya viwanda yanayoendelea kuboreshwa siku hadi siku wenzetu waliona ni fursa yao na kuja kwetu katika nyanja ya usafiri na ajira.

Wao waliona matumizi ya nguvu kubwa ni kumchosha mtu kwa kutumia viungo vyake kwenye uzalishaji na yameishapitwa na wakati zama hizi ni zama za teknolojia, akili na nguvu kidogo na wakafanikiwa kututeka, kupitia hualisia huu hiki ndicho kinachoitajika kwenye nyanja ya kilimo na wenye jukumu hili hapa nchini ni SIDO kwa kuja na mashine rahisi za kisasa katika kuboresha kilimo cha kisasa.

Kimbilio la kila kijana anayemaliza elimu ya upili na wale wanaosota kutafuta kazi baada ya elimu vyuo ni bodaboda kwa sababu ya urahisi huo uliopo hapo juu.

Ili na kilimo kiwe miongoni mwa kimbilio la vijana kama ilivyo kwa upande bodaboda ni wakati muafaka wa SIDO kubuni na kundaa “mashine zinazoweza kulima kwa kuendeshwa” kuanzia hekari tano na kuendelea kwa kutumia nishati kidogo ya mafuta.

Mashine hizi zikionekana zinagharimu kiasi kikubwa cha fedha kwa mtu mmoja mmoja katika kumiliki baada ya kutengenezwa basi kupitia serikali walau zipatikane ndani ya kila kata au kijiji.

Vijana wajiunge katika vikundi na kuandaa mpango wa jinsi ya kuiendesha/kuziendesha katika kuyaanda mashamba hayo.

Kupitia mashamba yatakayoandaliwa yalimwe mazao ya aina mbili tu au mashamba yawe mawili kwa kila kundi;
1. Shamba kwa ajili ya chakula.
2. Shamba kwa ajili ya biashara
Shamba kwa ajili ya chakula/ matumizi ya nyumbani/familia
Shamba kwa ajili ya biashara liwe kwa ajili ya kukuza vipato vya vijana hapa nchini na kustawisha urahisi wa mahitaji mengine yanayohitaji fedha.

Vilevile kupitia mashamba haya vijana watafuga mifugo ambapo malikapi kama vile pumba, mashudu na mengineyo yatakuwa chakula cha mifugo hii.

Imani yangu kupita haya tutakuwa na ziada ya chakula kama nchi na kutafuta soko la kuuza chakula nje ya nchi.

Baada ya mashine hizi za kilimo zitakazozalishwa na SIDO, pawepo na mashinde ndogondogo za kuchakata na kusindika baadhi ya mazao. Inashangaza sana kuona nchi yetu yenye shirika kama SISO bado tunatumia bidhaaa kama vile blenda ya kusindika sharubati zinatengenezwa na kuagizwa nje ya nchi wakati kwa kuangalia tu umbo la nje mashine hii inahitaji vitu vitatu vya muhimu ambavyo ni bapa la kukatia, glasi ya udongo au plastiki kwa ajili ya kuhifadhi kimiminika na mota ya kusukuma bapa. “inasikitisha”

Haya ninayoyaanisha hapa jukwaani ni kwa sababu nimeangalia rasilimali ardhi ipo, vijana wapo, mbolea inaweza kupatikana sambamba na mbegu zinaweza kuandaliwa hivyo kabla ya kupiga kelele za kuwa bodaboda ni kazi ya lahana na kuwaamsha walioondelea katika kutuzalishia mashine rahisi za kisasa katika kilimo ni jukumu la “SIDO” kubuni mashine hizi kwa uharaka zaidi na Wizara ya viwanda kwa kushirikiana na wizara ya kilimo wawajibike kwenye mapinduzi ya kilimo kwa kushirikiana na SIDO kwa kuja na mashine hizi.

Ni tumaini langu kubwa kupitia mashine hizi itakuwa kishawishi cha vijana katika kujikita kwenye kilimo chenye tija kitakacho wazalishia chakula na ziada. “kwanza tutengeneze ushawishi wa kuwavuta vijana kwenye kilimo” kama nilivyofurahishwa mpango wa serikali wa kuwapatia vijana mashamba na mbegu chini ya wizara ya kilimo.

Nimeshuhudia mashine ndogo za kukamua mafuta ya alizeti kupitia viwanda vidogo vya hapa nchi, kusindika karanga, kutengeneza matofali kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya kisasa lakini sijaona mashine za kuandaa hayo mashamba “tatizo liko hapa”

Trekta zilizopo ni bei ghari sana na haziwezi kutuondolea tatizo hili kwani wamiliki wake ni wachache sana na wenye uwezo mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom